Tuesday, November 6, 2018

AMANA BANK KUWEZESHA MADEREVA WA TAXI KUMILIKI GARI ZAO KUPITIA TAXIFY.

 Meneja Mkuu wa Biashara wa Amana Bank, Dasu Musa, (kulia) wakipeana mikono na kubalishana hati za mkataba na Meneja wa Taxify Tanzania, Remmy Eseka.
 
Meneja Mkuu wa Biashara wa Amana Bank, Dasu Musa, (kulia)akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Serena Hoteli jijini Dar es Salaam, kushoto ni Meneja wa Taxify Tanzania, Remmy Eseka.
...............................................
 
Amana Bank Tanzania imekuja na njia mpya ya mikopo isiyo na riba ambapo mara hii watatoa mikopo kwa madereva wa Taxi ili waweze kumiliki Gari zao.

Akizungumza wakati wa kutiia saini mkataba wa makubaliano kati ya Amana Bank na Kampuni ya usafirishaji ya Taxify Tanzania, Meneja Mkuu wa Biashara wa Amana Bank, Dasu Musa alisema vijana wengi wamkuwa hawana vigezo vya kukopesheka kwenye Taasisi za kifedha hali inayopelekea kushindwa kufikia malengo yao.

Alisema Amana Bank, ni Benki inayokwendaa na wakati kwa kuangalia changamoto zilizopo kwenye jamii na kuzitafutia ufunmbuzi ikiwa ni njia moja wapo ya kuwajali wateja wake na jamii kwa ujumla.

Dasu aliongeza kwa kusema kuwa, kwa sasa Benki hiyo kwa kushirikiana na Kampuni ya usafirishaji ya Taxify itawawezesha madereva kupata mkopo wa magari ambayo wakimaliza mikopo yao magari hayo yatabaki kuwa ya kwao.

Alisema Amana Bank, kama Benki inayoendeshwa kwa kuzingatia misingi ya kiislamu hatua hiyo ni sehemu ya mikakati ya kuifanya Benki hiyo kuwa kiongozi katika kutoa huduma za kibunifu zinazolenga kuinua jamii kiuchumi.

Aidha, alisema mikopo hiyo itatolewa kwa vikundi, hivyo madereva wanapaswa kuunda kikundi cha madereva kumi ambao watajidhamini wenyewe.

Alifafanua kuwa, Dereva atatakiwa kuweka amana isiyopungua asilimia kumi 10% ya thamani ya Gari anayohitaji kuwezeshwa ili kiasi hicho cha asilimia kumi kiwe kama dhamana mapaka atakapomaliza kufanya marejesho ya mkopo wake.

Sambamba na hilo, Dasu alisema kuwa, Dereva atatakiwa kuweka akiba kiasi cha shilingi elfu kumi na tano 15,000 kwa wiki ambayo ndiyo itakayomsaidia kukusanya kiurahisi marejesho yake.

Hata hivyo alisisitiza kuwa, moja ya sifa za kupata mkopo huo ni Dereva kuwa na Akaunti Amana Bank ili kujenga ukaribu kati ya Amana Bank na mteja husika.

Alisema miongoni mwa vigezo vitakavyozingatiwa katika kutoa mkopo huo ni pamoja na Dereva kuwa na uzoefu wa kutosha na rekodi nzuri katika kazi yake na jamii kwa ujumla.

Amana Bank, ni Benki pekee hapa Tanzania inayotoa huduma zake kwa kuzingatia sheria ya kiislamu katika miamala ya kifedha haibagui mteja kwa dini yake na kwamba hata mikopo hiyo haitabagua Dereva kwasababu ya dini yake bali vigezo ndio kitu pekee kitakachomuwezesha mtu kupata mkopo huo usiokuwa na riba.

Alisema kuwa Amana Bank katika kutua huduma zake mwaka huu wa 2018 inatimiza miaka saba ambapo katika kipindi chote hicho imeweza kuwa na wateja wa dini zote na kushirikiana nao katika biashara kwa karibu zaidi jambo ambalo wateja wenyewe wanaotumia Amana Bank wamethibisha namna wanavyofarijika kuhudumiwa na Amana Bank.

Hata hivyo Dasu alifafanua kuwa, katika sheria ya kiislamu imeharamishwa riba na imehalalishwa biashara kwahiyo Amana Bank itanunua magari na kuyauza kwa faida kidogo kwa njia ya mkopo.
Alisema katika uislamu hakuna biashara ya fedha kwa fedha bali ni lazima biashara ifanyike kwa kubadilishana fedha na kitu ambapo hilo ni katika mambo yanayozingatiwa na Amana Bank ili kuepuka kupokea na kutoa riba.

Akizungumzia sifa za ujumla zitakazomuwezesha Dereva kuingi kwenye mkopo huo alisema Kampuni ya Taxify ndio itakayowatahini madereva kulingana na sifa wanazotaka na baadae kuwasilisha majina ya madereva hao kwa Amana Bank.

Dasu alimalizia kwa kusema kuwa, kitendo hicho cha kutoa mikopo kwa madereva kitawasidia katika kuongeza kipato kwa mtu mmoja mmoja na kuongeza pato la serikali litakalotokana na ulipaji wa kodi.

Akizungumza mara baada ya kutia saini mkataba wa makubaliano, Meneja wa Taxify Tanzania, Remmy Eseka alisema anaishukuru Amana Bank kwa kuanzisha wazo hilo ili kuwasaidia vijana kiuchumi.

Alisema ni vigumu kwa Taasisi za kifedha kumuamini mtu kumpa mkopo bila ya kuwa na dhamana inayolingana na kitu anachokopeshwa lakini kwa Amana Bank inawezekana.

Alisema ushirikiano huo kati ya Amana Bank na Taxify umekuja kufuatia changamoto zinazowakabili madereva wengi wanaofanya kazi na Taxify kwakuwa madereva wengi hawamiliki magari yao binafsi.

Remmy alisema madereva wa Taxify kwa sasa asilimia 40 ya kipato chao kinakwenda kwa wamiliki wa magari jambo ambalo linawarudisha nyuma kiuchumi.

Akizungumzia utoaji wa huduma wa Taxify alisema Taxify ipo katika nchi 25 duniani ambapo hapa nchini ipo katika miji mitatu tu ambayo ni Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma.

Alisema katika kutuo huduma ya usafiri Taxify inatumia Gari za kawaida, Bajaji na Bodabodo.
 
Meneja Mkuu wa Biashara wa Amana Bank, Dasu Musa, wakitiliana saini na Meneja wa Taxify Tanzania, Remmy Eseka kuhusu utoaji wa mikopo ya magari isiyokuwa na riba  kwa madereva wa Taxify Tanzania. 
Meneja wa Masoko wa Amana Bank, Jamali Issa (kushoto) akiwaongoza waandishi wa Habari katika kuuliza maswali kwenye hafla hiyo fupi ya kutiliana saini mkataba wa makubaliano kati ya Amana Bank na Taxify Tanzania uwawezesha madereva wa Taxify Tanzania kukopeshwa magari bila ya riba, wanaotia saini mezani ni Meneja Mkuu wa Biashara wa Amana Bank, Dasu Musa, (kulia) na Meneja wa Taxify Tanzania, Remmy Eseka.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakishuhudia na kuchukua kumbukumbu ya tukio hilo.

WAZIRI MKUU AMPA SIKU SABA WAZIRI MWIJAGE KUSIMAMIA KIBALI CHA BM MOTORS

 WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, (kulia) alipokuwa Mkoa wa Pwani kufunga maonesho ya viwanda mwishoni mwa wiki iliyopita, kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, katikati ni  Mkuu wa Mkoa wa Pwani,  Evarist Ndikilo.
..........................................

Na scolastica Msewa, kibaha

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amempa siku saba Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kuhakikisha Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linatoa kibali kwa kampuni ya BM Motors cha kutengeneza na kuunganisha bodi za magari. 

Waziri Mkuu alisema hayo wakati akifunga maonesho ya Wiki ya Viwanda yaliyomalizika mkoa wa Pwani, katika Uwanja wa Sabasaba, Picha ya Ndege,  Kibaha.

Alimtaka Waziri Mwijage, ifikapo Ijumaa wiki ijayo ampe taarifa ya maendeleo ya kampuni hiyo kuhusiana na kibali hicho kutoka TBS.
Alisema wakati mwingine huo ni urasimu, kama ana tatizo ambiwe aboreshe hawezi awe amekaa tangu mwaka jana analalamika hajapata kibali cha kutengeneza mabodi.”

Na kwa nini msimpe hiyo fursa atengeneze bodi halafu mmwambie  arekebishe na mkiwa mmejiridhisha kama ana uwezo wa kutengeneza hayo mabodi na Watanzania waendelee kutengeneza hapa nchini,  badala ya kuagiza nje kwa gharama kubwa haina maana” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Aliongeza kuwa  “ulisema unaogopa kutumbuliwa (Mwijage), sasa sikutumbui nakupa wiki moja nipate taarifa ya mwenendo wa kampuni yetu ya ndani inayotaka kuunganisha mabasi.”

“Kwanza ni kampuni pekee inayotaka kuunganisha magari nchini, apewe fursa atujengee magari ya luxury (ya starehe) hapa Tanzania, alifafanua.
Mapema Waziri Mwijage akisalimia wananchi, alisema kwamba mashirika yaliyo chini ya wizara yake yakifanya kinyume yanahatarisha ajira yake, na yeye hayuko tayari kwa hilo.

Waziri Mkuu, aliutaka uongozi wa mkoa wa Pwani kujipanga kwa kuandaa maonyesho ya viwanda kama hayo kila mwaka, ili wajasiriamali wapate fursa ya kuonyesha bidhaa zao.

Pia aliagiza miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali kutumia bidhaa zinazotengenezwa nchini zikiwemo saruji, nondo na mabomba.

Akizungumzia eneo linalomilikiwa na Shirika la Elimu Kibaha lililopo Kibaha, Pwani, Majaliwa alisema shirika hilo liendelee kutafuta wawekezaji zaidi kwa eneo hilo.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Pwani,  Evarist Ndikilo wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya mkoa  huo,  alisema shirika hilo limepata mwekezaji ambapo limetenga eneo la hekta 38.8  kwa ajili ya ujenzi wa shughuli za kibiashara kama hoteli na maduka makubwa,  na hekta 100 ambazo zimetengwa kwa ajili ya makazi.

MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 06, 2018.

Monday, November 5, 2018

BALOZI MAHIGA AFUNGUA MAONESHO YA KIMATAIFA JIJINI ARUSHA

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki Balozi Agustine Mahiga akitoa hotuba kabla ya kuyafungua maonyesho hayo ya siku moja mwishoni mwa wiki jijini arusha picha na mahamoud ahmad arusha.
............................

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kikanda, Dk, Agustine Mahige amesema kuwa Tanzania haijamfukuza balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania, Reoland van de Geer bali ameitwa nyumbani na Umoja wa nchi hizo kw mshauriano. 

Aidha amepongeza mashirika ya Kimataifa yaliyopo nchini kwa kuandaa siku maalum ya kuwaonyesha wananchi fursa na kazi wanayofanya katika kukuza uchumi ikiwemo kuhakikisha muuaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda hayajirudii tena. 

Akizungumza Leo Novemba 3, Jijini Arusha katika maonyesho ya mashirika ya kitaifa yenye makao makuu yake Jijini Arusha  Dk, Mahige alisema kuwa ni jambo la kawaida kwa mabalozi wanaowakilisha nchi zao kuitwa na nchi zao kwaajili ya kupewa majukumu mengine au kutoa tathimini ya masuala waliyoyafanya. 

Dk, Mahige alisema uwepo wa Mahakama inayoshugulikia muuaji ya kimbari (MICT) ni kuhakikisha muuaji ya kimbari hayatokei tena katika nchi za Afrika na kutoa rai kwa mashirika ya Kimataifa yaliyopo nchini kutunza kumbukumbu muhimu ikiwemo za muuaji ya kimbari. 

Alisema maneno au vitendo yanayotolewa na wananchi katika nchi mbalimbali yanatakiwa kupingwa kwa nguvu zote kwani yanaweza kuibua hisia na kupeleka muuaji au kuleta chuki baina ya watu na watu au hata kupeleka mauaji. 

Alisisitiza kuwa ni vyema sasa mahakama hiyo ikawajengea uwezo wanazuoni wa masuala ya kisheria kwa Tanzania na nchi za Afrika ikiwemo kuzingatia utawala wa sheria na demokrasia pamoja na haki za binadamu. 

Awali Mkuu wa shughuli za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez alisema kuwa Tanzania inajitahidi kukahakikisha malengo endelevu yanazingatiwa ikiwemo kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa kila mtanzania. 

Naye Afisa Mwandamizi wa Utafiti kutoka Taasisi ya  Sheria za Kimataifa, Profesa Mathias Sahinkuye alisema masuala ya sheria  ni muhimu ili kuhakikisha nchi zinakuwa na amani 

Awali Meya wa Jiji la Arusha Kalist Lazaro,ambaye ndiye mwasisi wa Maonyesho hayo amesema tangu kuanza kwa Maonyesho hayo mwaka Jana kumekuwa na mafanikio makubwa kwa jamii kujifunza fursa mbalimbali za Kimataifa.

“Mjumuiko wa wananchi katika Maonyesho hayo ya Kimataifay umekuwa na manufaa makubwa kwani kumekuwepo na mabadiliko na mafanikio makubwa kwa wananchi kujifunza na kujionea fursa za kibiashara” Amesema Meya.