Monday, April 23, 2018

MAHAFALI YA 16 KIDATO CHA SITA BAGAMOYO SECONDARY.

Wanafunzi kidato cha sita 2018 Sekondari ya Bagamoyo wakiingia Ukumbini kwa mtindo huu siku ya Mahafali ya 16.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Alhaj, Majid Mwanga akizungumza wakati wa mahafali ya 16 ya kidato cha sita 2018.

..........................
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga amesema serikali inafanya juhudi ya kuinua kiwango cha ufaulu shuleni hivyo  walimu, wanafunzi na wazazi wanapaswa kuunga mkono juhudi za serikali ili kufanikisha malengo hayo.

Hayo aliyasema alipokuwa akizungumza katika mahafali ya 16 ya kidato cha sita shule ya sekondari Bagamoyo 

Alisema kila mmoja anatakiwa kutambua maukumu yake katika kufanikisha malengo ambapo serikali tayari inatekeleza majukumu yake ya kuingiza fedha za elimu bure shuleni pamoja na kuajiri walimu wa kutosha wa masomo mbalimbali.

Aliongeza kwa kusema kuwa kufuatia sera ya elimu bure shule ya sekondari Bagamoyo imepokea zaidi ya milioni mia mbili katika kipindi cha miezi sita ambapo ndani yake zipo fedha za ukarabati ili kuweka mazingira mazuri kwa wanafunzi.

Mkuu wa shule hiyo Khalfani Milongo alisema shule hiyo imejipanga katika kuwajengea uwezo wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuwapa mitihani ya majaribio ya mara kwa mara .

Aidha alisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mmomomonyoko wa maadili unaosababishwa na utandawazi.

Alisema wanafunzi wamekuwa wakiiga tabia ambazo hazina maadili kutokana na kumiliki simu ambapo wanaweza kuona vitu mbalimbali kwenye mitandao vinavyowashawishi mambo yasiyofaa.

Jumla ya wanafunzi 328 wametunukiwa vyeti vya kuhitimu kidato cha sita 2018 ambapo wote ni wavulana.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alha, Majid Mwanga na Mwenyekiti wa Bodi ya shule sekondari ya Bagamoyo, wakiangalia jarida ambalo limeanzishwa kwa ubunifu wa wanafunzi wa sekondari ya Bagamoyo.


Monday, April 16, 2018

MKURUGENZI HIGHLAND ESTATES ACHANGIA MILIONI 10 UJENZI WA ZAHANATI UBENA.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Highland Estates Limited akizungumza kwenye mkutno kijiji cha Lulenge na kutoa ahadi ya Vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni 10.
.......................................................

Mkurugenzi wa Kampuni ya Highland Estates Limited, Naweed Mulla, amechangia vifaa vya ujenzi vyenye thamanai ya shilingi milioni 10 kwaajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Lulenge kata ya Lugoba.

Naweed ametoa ahadi hiyo mbele ya Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga katika Mkutano wa kijiji cha Lulenge ambapo Mkuu wa wilaya alifika kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Lulenge.

Awali akizungumza katikaa Mkutano huo, Diwani wa kata ya Ubena  Nicholaus Mluwa alisema kijiji cha Lulenge kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa Zahanati hivyo wananchi huttembea umbali mrefu kufuata huduma ya Afya.

Alisema makundi yanayopata shida katika kutafuta huduma ya Afya ni kina mama na watoto ambapo kijiji hicho kingekuwa na zahanati kero ingewaondoka.

Kufuatia hali hiyo Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo alitoa wazo la uanzishwaji wa ujenzi kwaajili ya Zahanati na kuwataka wananchi kuchangia ili Serikali kupia Halmashauri ya Chalinze iweze kuongeza nguvu pale watakapoishia.

Mkuu wa wilaya alimuagiza Mwenyekiti wa kijiji hicho kuitisha mkutano na wenyeviti wa vitongoi ili kuangalia uwezekano wa kuanza ujenzi huku wakitakiwa kuchangia vifaa, nguvukazi na fedha kufanikisha ujenzi huo

Kutokana na hali hiyo Mkurugenzi wa Highland Estates Limited Naweed Mulla meahidi kutoa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni 10 ikiwa ni sehemu ya mchango wake kama muwekezaji katika kata hiyo ya Ubena.

Diwani wa kata ya Ubena Nicholaus Mluwa alimshukuru muwekezaji huyo kwa misaada mbalimbli anayotoa kwenye kata hiyo.

Mluwa alisema Naweed amekuwa akijitolea mambo mbalimbali ya kimaendeleo ndani ya kata hiyo ikiwemo kuchonga barabara za vijiji vya kata hiyo na mengineo

Aidha, Diwani Mluwa aliwataka ananchi wake kumpa ushirikiano muwekezaji huyo na kutoa wito kwa wawekezaji wa kata hiyo kujitokeza katika kuchangia miradi ya maendeleo ambayo faida yake inarudi kwa wananchi.
 
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mh. Alhaj, Maid Mwanga akizungumza katika kijiji cha Lulenge. 

 
Diwani wa kata ya Ubena  Nicholaus Mluwa akizungumza katika mkutano kijiji ch Lulenge.


MAGAZETI YA LEO APRIL 16, 218.

FEDHA ZA ELIMU BURE WANANCHI WAZIJUE.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhaj, Majid Mwanga amewaagiza maafisa Elimu kata wilayani Bagamoyo kutoa taarifa za fedha za Elimu bure wanazopokea kila kata.

Mwanga aliyasema hayo kwa nyakati tofauti katika ziara yake ya kuweka mawe ya msingi miradi ya maendeleo Halmashauri ya Chalinze na Bagamoyo.

Alisema Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imetangaza elimu bure ambapo kila shule inapewa fedha za kuwezesha mpango huo wa elimu bure.

Aliongeza kwa kusema kuwa wananchi hawaui kama serikali inagharamia elimu hivyo ni vyema fedha hizo zikawa wazi kwa kila mwananchi na matumizi yake yabanishwe kwenye vikao vya Halamashauri za vijiji.

Aliwataka Maafisa Elimu kata kutoa tarifa kwenye vikao vya kata ili kujua kila kata imepokea kiasi gani huku fedha zilizotengwa kwaajili ya ukarabati zikztumika kama ilivykusudiwa na wananchi wapewe taarifa juu ya fedha hizo.

Alisema serikli inatumia fedha nyingi katika kuwezesha elimu bure ambapo alitolea mfano wa kata ya Lugoba iliyopokea milioni 200 katika kipindi cha Oktoba 2017 hadi Machi 2018 na kwamba kila kata imepewa fedha hizo kulingna na mahitaji yake.

Aidha, aliwaonya wakuu wa shule wanaoendelea kuchangisha fedha katika shule zao kwamba wakibainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao kwa kukiuka agizo la Rais la kufuta michango ya aina zote.

Alisema wananchi wanayo nafasi ya kuchangia katika elimu lakini michango hiyo ni lazima ipate kibali cha Mkuu wa Mkoa na kwamba Mwalimu hatakiwi kujisisha na aina yoyote ya mchango na badala yake Bodi na kamati za shule zihusike kukusanya michango hiyo na kusimamia matumizi yake wao wenyewe bila ya kungiliwa na walimu.

Mkuu huyo wa wilaya alisisitiza fedha za ukarabati zitumike vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa kwa kubadilisha mandhari ya majengo ili wanafanzi wapate ari ya kupenda kusoma.

Katika ziara hiyo aliweza kuweka mawe ya msingi ujenzi wa madara katika shule za Kiwangw, Vigwaza, Msoga, Msata Miono na Ubena ambapo katika kata hizo zipo shule mpya zilizoanzishwa kutokana na hamasa yake na kupelekea shule moja inayojengwa kata ya Ubena kupewa jina la MAJID MWANGA.

 
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhaj, Majid Mwanga(kulia) akikagua ujenzi wa vyumba viwili vya maabara na chumba kimoja cha maktaba katika shule ya Sekondari Mboga iliyopo kata ya Msoga Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo, picha ya juu ni muonekano wa jengo hilo.
 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhaj, Majid Mwanga akikagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule mpya inayoanzishwa kijiji cha Diozile kata ya Msoga Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo, Picha ya juu Mkuu wa wilaya akiongea na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho waliofika kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi wa shule hiyo.
 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhaj, Majid Mwanga akiweka jiwe la msingi ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule mpya inayoanzishwa kijiji cha Diozile kata ya Msoga Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo, Picha ya juu Mkuu wa wilaya akiongea na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho waliofika kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi wa shule hiyo.
 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhaj, Majid Mwanga akiweka jiwe la msingi ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Vigwaza Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo.

 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhaj, Majid Mwanga akizungumza na wananfunzi wa shule ya Msingi Lulenge iliyopo kata ya Ubena Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo.

Sunday, April 15, 2018

DC PANGANI APOKEA VITANDA 10 VYA KUJIFUNGULIA KUTOKA BANDARI TANGA..

Meneja wa Bandari ya Tanga,Percival Salama kushoto akimkabidhi vitanda 10 Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kwa ajili ya kujifungulia wakina mama wajawazito ambavyo vimetolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) ambavyo vinagharimu kiasi cha milioni 12.2 kushoto anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Pangani.
 

Meneja wa Bandari ya Tanga,Percival Salama kushoto akimkabidhi vitanda 10 Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kwa ajili ya kujifungulia wakina mama wajawazito ambavyo vimetolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) ambavyo vinagharimu kiasi cha milioni 12.2 kulia anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Pangani,Daudi Mlahangwa

Meneja wa Bandari ya Tanga,Percival Salama kushoto akimpongezwa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso mara baada ya kukabidhi vitanda hivyo katika anayeshughudia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah.
 

Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa katika akimkabidhi Vitanda 10 vilivyotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini TPA kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Pangani,Daudi Mlahangwa kwa ajili ya wilaya ya Pangani kulia ni Meneja wa Bandari ya Tanga,Percival Salama akishughudia

Sehemu ya vitanda 10 vilivyotolewa na TPA wilayani Pangani.

FATUMA KARUME RAIS MPYA TLS


Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) kimemchagua Fatuma Karume kuwa Rais mpya  wa Chama hicho kwa kupata kura 820. 

Nafasi hiyo ya Urais  ilikuwa ikigombewa na Mawakili wengine watatu ambao ni, Simba Ngwilimi ambaye amepata 363, Musa Mwapongo kura 12 na Godfrey Wasonga kura 6.

Katika uchaguzi huo, Dkt Rugemeleza Nshala amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa TLS kwa kupata kura 1170. Fatma anachukua nafasi ya Tundu Lissu ambaye amemaliza muda wake.

Kwa upande wa Zanzibar Wakili Omar Said Shaaban amechaguliwa kuwa Rais Mpya wa chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS)

Saturday, April 14, 2018

ZAIDI YA MILIONI 600 KUJENGA MIRADI YA MAENDELEO CHALINZE.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhaj, Majid Mwanga akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa kituo cha Polisi Lunga kata ya Lugoba Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo.
  
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhaj, Majid Mwanga alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika Zahanati ya Buyuni kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze, ambapo alikuwa na ziara ya wiki nzima kuweka mawe ya msingi miradi mbalimbali ya maendeleo.
..................................................................

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhaj, Majid Mwanga ameweka mawe ya msingi miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya milioni 600 katika Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo.

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika vijiji vya Halmashauri ya Chalinze katika zoezi la uwekaji wa mawe hayo ya msingi, Mkuu huyo wa wilaya mwenye kauli mbiu inayosema UONGOZI UNAOCHA ALAMA, alisema lengo la serikali ni kutatua kero za wananchi katika kila kijiji kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Alisema kila mwananchi anayo haki ya kupata huduma bora za Afya, Elimu, miundombinu mizuri ya Barabara, Umeme na Maji hivyo ni wajibu wa serikali kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa.

Aidha, aliwataka wananchi kutoa ushirikiano katika kufanikisha ujenzi wa miradi hiyo ili kufikia lengo la serikali ambalo ni kuwasogezea wananchi huduma muhimu za jamii.

Alisema sio dhambi kwa wananchi kuchangia ujenzi wa miradi ya maendeleo hivyo serikali inapotenga fedha kwaajili mradi fulani ni vyema wananchi wakachangia baadhi vifaa au nguvukazi ili kurahisisha utekelezaji wake.

Aliongeza kwa kusema kuwa wananchi kwa kushirikiana na serikali wanaweza kufanikisha ujenzi wa miradi muhimu kama zahanati na shule.

Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wenyeviti wa vijiji kutoa elimu kwa wananchi juu ya ushirikishwaji wa maendeleo na kupata muafaka wa pamoja katika kuchangia maendeleo kwa hiyari ambapo serikali inaendelea kutekeleza kila kijiji.

Kwa upande wao wenyeviti wa vijiji vya Halmashauri ya Chalinze kwa nyakati tofauti wamempongeza Mkuu huyo wa wilaya kwa kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inaleta tija kwa wananchi.

Walisema baadhi ya vijiji kwa miaka mingi vimekuwa havina huduma za Zahanati na Shule laikini kupitia uhamasishai wake wananchi wameweza kuanzisha na Halmashauri kuongeza nguvu na hatimae kufanikisha miradi kadhaa katika vijiji mbalimbali katika Halmashauri hiyo.

Katika kila kijiji wenyeviti hawakusita kumshukuru mkuu huyo wa wilaya licha ya kuwa chanzo cha ujenzi wa miradi kadhaa lakini pia ni mchangiaji wa fedha na vifaa katika kufanikisha miradi hiyo.

Miradi hiyo iliyowekwa mawe ya msingi na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo katika halmashauri ya Chalinze na gharama zake kwenye mabano ni pamoa na Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Kiwangwa kata ya Kiwangwa,(15,539,800/=) Zahanati ya Kihangaiko kata ya Msata, (30,401,400/=) Zahanati ya Buyuni kata ya Vigwaza (98,420,000/=) Madarasa 6 shule ya Msingi Vigwaza kata ya Vigwaza (198,000,000/=)

Miradi mingine ni Madarasa nane shule ya Msingi Bwilingu A na B kata ya Bwilingu (86,809,000/=) Vyumba viwili vya madarasa shule ya Msingi Lulenge kata ya Ubena ( 21,946,000/=) Nyumba ya Daktari Zahanati ya Mboga kata ya Msoga (50,000,000/=) Sekondari ya Mboga kata ya Msoga (90,000,000/=) Vyumba viwili vya madarasa shule ya Msingi Changa kata ya Msoga (20,000,000/=)  Kituo cha Polisi Lunga kata ya Lugoba (60,000,000/=)

Miradi yote hiyo imetekelezwa kwa ushirikiano wa serikali, wananchi, wafadhili na wadau mbalimbali wa maendeleo wa kata husika na wilaya kwa ujumla.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo alitoa wito kwa wadau wa maendeleo wilayani Bagamoyo kujitokeza kuchangia miradi hiyo ambayo baadhi yake haijakamilika.

Aidha, aliwataka wananchi wazaliwa wa Bagamoyo popote walipo kuchangia maendeleo ya vijiji walivyotoka ikiwa ni njia ya kuenzi vjiji vyao huku wakiisaidia serikali katika kuleta maendeleo.
 
 Muonekano wa jengo la kituo cha Polisi Lunga kata ya Lugoba Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo ambapo Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ameweka jiwe la msingi ili kukamilisha kituo hicho cha Polisi zinahitajika Milioni 30.

 
Muonekano wa Zahanati ya Buyuni kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze, ambayo imekamilka kwa sasa zinahitaika samani za ndani ili kuanza kazi rasmi.
 
 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Alhaj, Majid Mwangaakiweka jiwe la msingi nyumba ya Daktari katika Zahanati ya Mboga iliyopo kata ya Msoga Halmashauri ya Chalinze.

Friday, April 13, 2018

RAIS DKT. MAGUFULI AWAPANDISHA VYEO MAAFISA WA JWTZ


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo akitangaza majina ya Maafisa mbalimbali wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopandishwa vyeo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.
........................................