Wednesday, March 21, 2018

NAIBU WAZIRI SHONZA AONGOZA KUAGA MWILI WA JOHN MPONDA BAGAMOYO.


Naibu Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza ameongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa mwalimu John Mponda, ambae alikuwa Mkufunzi Msaidizi daraja la 2, Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)

Mwalimu Mponda Pia alikuwa ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, ( Bagamoyo International Festival of Arts and Culture) . 
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akizungumza wakati wa kuaga mwili wa Mwalimu John Mponda wa TaSUBa.
.................................................
Naibu Waziri Habari, Sanaa na Utamaduni Juliana Shonza amesema Wizara yake itamkumbuka Mwalimu John Mponda kwani alikuwa kiunganishi kizuri kati ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) na wizara yake katika kufanikisha mambo mbalimbali ya Sanaa hapa nchini.

Naibu Waziri huyo aliyasema hayo leo tarehe 21 Machi 2018 wakati wa kuaga mwili wa mwalimu John Mponda shughuli zilizofanyika ukumbi wa TaSUBa Bagamoyo.

Alisema licha ya kuwa Mwalimu marehemu Mponda Mwalimu Mponda Pia alikuwa ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, (Bagamoyo International Festival of Arts and Culture) . 

Alisema wizara imempoteza mtu muhimu katika tasnia ya sanaa na kwamba mchango wake utakumbukwa katika jamii.

Mtendanji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa) DKT.Herbert Makoye amemualezea mwalimu Mponda kuwa ni mtu mchapakazi aliyekuwa akitoa ushirikiano wa kila namna katika utekelezaji wa kazi za kiofisi.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga alisema Mwalimu mponda ni mtu muhimu katika jamii hali iliyopelekea kila mmoja aweze kushiriki mazishi yake.
Alisema watu wa Bagamoyo na wale wote waliopata taaluma ya sanaa kupitia yeye watamkumbuka kwa jinsi alivyoweza kutoa ushirikiano wake bila ya kubagua.

Nae Mtoto wa Marehemu Mary Mponda alisema kwa niaba ya familia ya Mponda wanatoa shukrani kwa watu wote, TaSUBa na Serikali kwa ujumla kwa namna walivyoweza kushiriki katika msiba huo wa baba yao.

Aidha, alisema kufuatia umati mkubwa ulifurika katika kumuaga Mwalimu Mponda ni dalili tosha ya kuonyesha mapenzi makubwa waliyonayo kwa marehemu huyo.

Mary alisema amepata fundisho kubwa kupitia msiba huo na kuona ni jinsi gani mtu anapaswa kuishi na jamii ili kujenga mazingira mazuri miongoni mwa watu na kwamba hilo atalichukua kama somo katika maisha yake.

Mwalimu Mponda alizaliwa tarehe 10 Novemba 1963 wilayani Ludewa  Mkoa wa Njombe, aliajiriwa Chuo cha Sanaa Bagamoyo (sasa TaSUBa) tangu Tarehe 10  Novemba 1984, hadi mauti yanamfika alikuwa na cheo cha Mkufunzi Msaidizi daraja la 2,.

Aidha, Mwalimu Mponda Pia alikuwa ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, ( Bagamoyo International Festival of Arts and Culture) .

Wakati wa uhai wake Mwalimu Mponda aliwahi kuwa msanii katika kundi la "Bagamoyo Players" lililokuwa linaundwa na wakufunzi wa TaSUBa, Bagamoyo Players lilijipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi kwa kufanya maonyesho katika nchi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kampeni mbalimbali za maendeleo.

Mwili wa Marehemu umesafirishwa kwendaMjini Mbalizi, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoani Mbeya ambapo mazishi yatafanyika tarehe 22 Machi 2018 hukohuko Wilaya ya Mbeya Vijijni.

Marehemu ameacha mjane na watoto watatu.


 Jeneza liliobeba mwili wa Marehemu Mwalimu John John Mponda.
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza (wa pili kulia) wa kwanza kulia ni Mtendanji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) DKT.Herbert Makoye wa kwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TaSUBa, George Daniel Yambesi.
Baba mzazi wa marehemu Mzee John Mponda watatu kushoto na wadogo zake marehemu
Mke wa Marehemu Mponda wa pili kushoto na watatu kushoto  ni mtoto wa marehemu, Mary Mponda.

Sehemu ya umati wa watu waliofika Ukumbi wa TaSUBa kuaga mwili wa Mwalimu Mponda.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu, Mwalimu John John Mponda katika Ukumbi wa TaSUBa, Mjini Bagamoyo
 Mshauri wa Mgambo wilaya ya Bagamoyo, Meja.....akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu, Mwalimu John John Mponda katika Ukumbi wa TaSUBa, Mjini Bagamoyo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM)  Dr Siston Masanja Mgullah, akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu, Mwalimu John John Mponda katika Ukumbi wa TaSUBa, Mjini Bagamoyo.
 Mtendanji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) DKT.Herbert Makoye akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu, Mwalimu John John Mponda katika Ukumbi wa TaSUBa, Mjini Bagamoyo.
 Meneja Mkuu wa Efm Radio Dennis Ssebo akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu, Mwalimu John John Mponda katika Ukumbi wa TaSUBa, Mjini Bagamoyo.



Watoto wa Mwalimu John John Mponda wakiongozwa na dada yao Mary Mponda wakati wakitoa salamau zao za mwisho kwa baba yao mpendwa katika Ukumbi wa TaSUBa.

MAFISA HABARI TANGAZENI MAFANIKIO YA SERIKALI.


Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Rodney Thadeus akizungumza na Maafisa Habari na Mawasiliano kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Morogoro, Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga yaliyofunguliwa jana jumanne Machi 20, 2018. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
..............................................
MAAFISA Habari na Mawasiliano katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini wametakiwa kuacha kufungia katika makabati na makabrasha taarifa chanya za utekelezaji wa mikakati, miradi na programu mbalimbali za Serikali na badala yake watangaze mafanikio hayo kwa umma.

Hayo yamesemwa jana (Jumanne Machi 20, 2018) Mkoani Morogoro na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Rodney Thadeus wakati wa ufunguzi wa mafunzo kuhusu mwongozo wa uandishi wa habari za tovuti kupitia Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).

Thadeus alisema Serikali inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini, hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano katika maeneo hayo watangaze mafaniko hayo badala ya kusubiri maswali na hoja mbalimbali za wananchi wakihoji katika kupata uelewa kuhusu miradi hiyo.

“Maafisa Habari, msifungie taarifa katika makabati yenu toeni taarifa kwa Umma, wananchi wanapenda kufahamu nini kinafanywa na Serikali yao hivyo jukumu la Afisa Habari ni kupiga picha kuandaa taarifa na wekeni vielelezo hivyo katika tovuti zenu ili kujibu hoja za wananchi” alisema Thadeus.

Aidha, alisema ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano kuhakikisha kuwa wanaweza taarifa mpya kila wakati ili kuhakikisha kuwa zinakidhi mahitaji ya msingi ya wananchi ambao wamekuwa wakitumia muda mrefu kwa ajili ya kutafuta huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali katika maeneo yao ya kazi.

Akifafanua zaidi alisema Maafisa Habari na Mawasiliano katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini ndiyo wataalamu wa masuala ya Mawasiliano katika maeneo yao ya kazi, hivyo wana wajibu wa kutoa ushauri kwa viongozi wao wa kazi kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa mara kwa mara kuhusu hoja mbalimbali zinazoulizwa na kujitolea majibu kwa wakati.

Aliongeza kuwa matumizi ya tovuti ndiyo njia ya haraka zaidi ya kurahisisha mfumo wa utoaji wa habari na taarifa mbalimbali za Halmashaauri na Mikoa, hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano kuwa mabalozi ili kuhakikisha kunakuwepo na daraja la mawasiliano baina ya Serikali na wananchi katika kupata suluhu ya masuala mbalimbali ikiwemo migogoro inayotokea mara kwa mara.

Kwa upande wake, Kiongozi wa Timu ya Utawala Bora kutoka PS3, Dkt. Peter Kilima alisema uboreshaji wa tovuti ni sehemu muhimu ya utekelezaji wa dhana halisi ya utawala bora hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano katika Mikoa na Halmashauri nchini kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa zinazozingatia muda na mahitaji yaliyopo.

Aliongeza ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano kuzingatia mafunzo kuhusu mwongozo wa uandishi wa habari katika tovuti za Serikali katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini kwa kuwa wananchi wana matarajio makubwa na Serikali yao katika kuwapatia huduma mbalimbali.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za tovuti kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Morogoro, Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo hayo yaliyofunguliwa jana Jumanne Machi 20, 2018 Mkoani Morogoro. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID)
Afisa Tehama kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro, Alfred Chali akichangia hoja wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za tovuti kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Morogoro, Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga yaliyofunguliwa jana Jumanne Machi 20, 2018. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).

MPINZANI WA YANGA CAF KUJULIKANA SAA 8:30 MCHANA LEO.


Yanga SC imeangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambako watamenyana na moja ya timu zilizofuzu hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo.

Hiyo ni baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Township Rollers Jumamosi jioni Uwanja wa Taifa mjini Gaborone nchini Botswana.

Timu ambazo zimefuzua hatua ya mtoani ambazo Yanga anaweza kukutana nazo ni Fosa Juniors kutoka Madagascar,CARA Brazzaville (Con),Costa do Sol ya Msumbiji,Akwa United na Enyimba za Nigeria,Deportivo Niefanga ya Equatorial Guinea,Welayta Dicha ya Ethiopia,,El Masry ya Misri,Hilal El  Obied ya Sudan,Raja Casablanca na Berkane za Morocco,Djoliba ya Mali,CR Belouizdad ,USM Alger za Algeria,La Mancha ya Congo Brazaville na Supersport United ya Afrika Kusini.

Timu ambazo zimetolewa Ligi ya Mabingwa na kuangukia Shirikisho ni Yanga ya Tanzania,Aduana Stars ya Ghana,Al-Hilal Omdurman  ya Sudan,Rayon Sport ya Rwanda,ASEC Mimosas na WAC  za Ivory Coast,Gor Maria ya Kenya,As Vita Club ya DRC,Plateau  United na MFM FC za Nigeria,Generation Foot ya Senegal,Bidvest Wits ya Afrika Kusini,CF Mounana ya Gabon,St,George ya Ethiopia ,Zanaco United ya Zambia na US Songo ya Msumbiji.

Droo ya ratiba ya mechi za mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho inatarajiwa kupangwa Leo majira ya saa 8:30 Mchana kwenye makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Mjini Cairo huku inatarajiwa kuwa Live kupitia ZBC2 kwa mjibu wa taarifa ya Shirikisho hilo

AJALI YA GARI YA MKURUGENZI WA TBC, WAWILI WAFARIKI.


Watu wawili wamekufa wilayani Kasulu mkoani Kigoma katika ajali ya gari la Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Dkt. Ayub Rioba lililokuwa likitokea wilayani Kibondo kwenda Kigoma Mjini.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema chanzo cha ajali hiyo ni utelezi uliosababisha gari kuacha njia na kuwagonga waenda kwa miguu watatu.

Gari la Mkurugenzi Mkuu wa TBC lililopata ajali lenye namba za usajili  STK 8769 lilikuwa na abiria wawili akiwemo mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba na Mkuu wa kanda ya magharibi TBC Mhandisi Zebron Mafuru ambao  wote wametoka salama na hali zao ni nzuri.

Dkt. Rioba yuko katika ziara ya kukagua vituo vipya vya matangazo vilivyojengwa katika maeneo ya mipakani.

RAIS DKT. MAGUFULI AIVUNJA BODI YA NHC.