Tuesday, March 20, 2018

VIJANA 20 WAOZESHWA SIKU MOJA MOROGORO.


Taasisi ya The Islamic Foundation kwa kushirikiana na Taasisi ya Sharjah Charity International katika falme za kiarabu UAE pamoja na Mabwana harusi 20 wamefanikiwa kwa pamoja kukamilisha zoezi la ibada ya ndoa ya kiihistoria nchini Tanzania kwa vijana wa kislamu 20.

Ndoa hiyo imefanyika katika makao makuu ya #Taasisi ya the Islamic foundation mjini Morogoro na kuhudhuriwa na watu mbalimbali kutoka katika mkoa wa Morogoro na maeneo ya jirani huku taasisi ya TIF ikiweza kuratibu shughuli hiyo na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Akizungumza katika Ndoa hiyo ya kihistoria mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya barabara na usafirishaji Dubai UAE Dkt. Yusuph Mohamed Abdalla Hassan AL-ALI ambaye ndiye mgeni Rasmi katika ibada hiyo ya ndoa amewataka vijana kuoa kwa kufuata mafundisho ya Mtume Mohammad (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aaalihi Wa Sallam)

Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya The Islamic Foundation Aref Nahdi amesema kuwa TIF itaendelea kusimamia na kudhamini vijana mbalimbali wa kiislamu ili kuweza kufikia malengo yao ya kutekeleza ibada ya ndoa.

Hata hivyo MAMLAKA ya barabara na usafirishaji Dubai RTA Dubai UAE imeikikabidhi kituo cha yatima cha Darul Imaan kinachomilikiwa na taasisi ya The Islamic Foundation Basi la Abiria aina ya Ashok Leyland lenye uwezo wa kubeba abiria 50.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya barabara na usafirishaji Dubai UAE Dakta Yusuph Mohamed Abdalla Hassan AL-ALI katika ziara yake kwa taasisi ya the Islamic foundation mkoani Morogoro na kusema kuwa mamlaka hiyo imeikabidhi kituo hicho ili kuweza kurahisisha huduma za usafiri kwa watoto ya tima wanaolelewa na TIF.

Aidha mamlaka hiyo imekabidhi mabegi 200 kwa watatoto yatima wanaolelewa katika kituo cha taasisi ya the Islamic foundation cha Darul Imaan na kusema kuwa mabegi hayo yatawasaidia watoto hao kwa kiasi kikubwa.

Katika hatua nyingine mamlaka ya barabara na usafirishaji Dubai UAE imetoa baiskeli 25 kwa watoto hao yatima.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa taasisi ya the Islamic foundation Aref Nahdi ameishukuru mamlaka hiyo kwa kuona umuhimu wa kuisaidia tif katika kitengo cha Yatima na kusema kuwa tif imefarijika na msaada huo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya The Islamic Foundation Aref Nahdi akizungumza wakati wa hfla hiyo ya kuwaozesha vijana 20 wa kiislamu mjini Morogoro.

Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka ya barabara na usafirishaji nchini Dubai UAE, Dakta Yusuph Mohamed Abdalla Hassan AL-ALI akizungumza katika hafla hiyo ya kuwaozesha vijana 20 wa kiislamu iliyofanyika Mjini Morogoro nchini Tanzania.

Katibu Mkuu wa Taasisi ya The Islamic Foundation, Sheikh Ibrahim Twaha (kulia) na Mkurugenzi wa vyombo vya Habari vya Imaan, Ahmed Bawaziri (kushoto) wakiwaongoza vijana 20 wa kiislamu katika zoezi la kuwafungisha ndoa wote kwa siku moja zoezi ambalo limesimamiwa na Taasisi ya 
The Islamic Foundation kwa kushirikiana na Taasisi ya Sharjah Charity International kutoka falme za kiarabu UAE. 
Upande wa chakula mambo yalikuwa hivi.
Sehemu ya umati wa watu waliofika kushuhudia ndoa hiyo ya kihistoria hapa nchini.

MAGAZETI YA LEO TAREHE 20 MACHI 2018.

Monday, March 19, 2018

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI UJENZI WA SEKONDARI MICHEWENI.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki ujenzi wa skuli ya Sekondari Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki ujenzi wa skuli ya Sekondari Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba.

Picha ya kuchora inayoonyesha muonekano wa skuli hiyo pindi itakapokamilika.

 Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.

RAIS DKT MAGUFULI AENDESHA MKUTANO WA 11 WA BARAZA LA TAIFA LA BIASHARA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO



 Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel  akisoma muhtasari wa mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018.

 Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisalimiana na Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Dkt. Reginald Mengi  alipowasili kuendesha mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018.


Mwenyekiti wa Baraza la  Taifa la Biashara ITNBC) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa meza kuu  na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na walemavu Mhe. Jenista Joakim Mhagama na kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Elisante Ole Gabriel  na Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Dkt. Reginald Mengi  akijiandaa kufungua  mkutano wa 11 wa baraza hilo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018. 


Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018.


Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dkt Reginald Mengi akiongea katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018 




Viongozi wa taasisi mbalimbalui wakiwa katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara unaoendeshwa na Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 19, 2018


MAZISHI YA JOHN MPONDA TaSUBa YATOA RATIBA.



SERIKALI KUSAMBAZA UMEME VIJIJI VYOTE VILIVYO KWENYE MPANGO WA REA KISHAMPU.


Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu (kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Taraba wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipotembelea mradi wa umeme kijiji cha Negezi.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipotembelea miradi ya umeme.
........................................

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu amesema Serikali itaendelea na usambazaji wa nishati ya umeme katika vijiji vyote 50 katika Wilaya ya Kishapu kama ambavyo iliahidi.

Amesema hayo wilayani humo wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipofanya ziara wilaya Kishapu kukagua miradi ya umeme inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Kamati hiyo ikiwa kwenye vijiji vya Negezi na Bulimba ikiambatana pia na uongozi wa Mkoa na Wilaya, Mhe. Mgalu alisema kuwa mpango wa usambazaji umeme ni wa awamu na kuwa wananchi wasiwe na hofu kila kijiji kitafikiwa na mradi.

Aliongeza kuwa vijiji 33 kati ya 50 vitapata umeme wa REA awamu hii ya tatu wakati 17 vitapata nishati hiyo kupitia njia kuu inayounganisha mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida na Tabora.

Kwa upande wake, Kamati hiyo ya Bunge ilisema wataendelea kuikumbusha Serikali iendelee kutimiza ahadi zake kwa wananchi za kukamilisha miradi ya umeme.

Iliwataka wananchi ambao wamepitiwa na miradi hii katika vijiji vyao kuichangamkia fursa na kuomba kuunganishiwa ili kupata huduma hiyo na kujiletea maendeleo.

Aidha iliwataka wananchi kuboresha aina za makazi yao kadiri ya uwezo wao na kuezeka nyumba zao kwa bati na kuachana na matembe na hatimaye kuwa na nyumba zilizo bora.

Katika ziara hiyo kijiji cha Bulimba kilichopo kwenye kata ya Ukenyenge kumezinduliwa rasmi huduma ya umeme mradi uliokamilshwa kupitia REA na hivyo kutarajiwa kuwanufaisha wananchi.
Baadhi ya wajumbe Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa kwenye mkutano wa hadhara kijiji cha Negezi wakati ilipotembelea miradi ya umeme vijijini wilayani Kishapu.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu (kushoto) akishirikia kucheza ngoma ya Kisukuma akiwa akiwa kijiji cha Bulimba mabako umeme uliwashwa rasmi baada ya kukamilika usambazaji.