Saturday, October 14, 2017

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AONGOZA SHEREHE ZA KUZIMA MWENGE,KUMBUKUMBU YA HAYATI BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE NA WIKI YA VIJANA ZANZIBAR OKTOBA 14,2017



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea Mwenge wa uhuru kutoka kwa kiongozi wa mbio za Mwenge 2017, Amour Hamad Amour, wakati wa  sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana katika uwanja wa Amaan mjini Magharibi Zanzibar Oktoba 14, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikvishwa skafu baada ya kuwasili kuongoza sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar Oktoba 14, 2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akielekea kwenye jukwaa kwaaajili ya salamu ya heshima mara baada ya kuveshwa skafu katika sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar Oktoba 14, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar baada ya kuwasili kuongoza sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar Oktoba 14, 2017



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na mwakilishi wa familia ya Mwalimu, Mhe. Makongoro Nyerere wakati akiwasili kwenye sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar Oktoba 14, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt. Ali Mohamed Shein wakifurahia maonyesho ya halaiki kutoka kwa watoto wakati wa sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar Oktoba 14, 2017.



Vijana shupavu  sita wakijiandaa kumkabidhi Mwenge Mhe,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli wakati wa  sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana katika uwanja wa Amaan mjini Magharibi Zanzibar Oktoba 14, 2017

 


KIKUNDI CHA MSHIKAMANO CHA MBWENI CHATOA MSAADA KWA WAZEE WA NUNGE KIGAMBONI.

Mwenyekiti wa kikundi cha Mshikamano cha mbweni, Beatrce Njanda pamoja na katibu wa kikundi hicho Florence lema, wakigawa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni moja kwa wazee wanaoishi katika kambi ya Nunge Kigamboni jijini Dar es Salaam, vitu hivyo vilivyotolewa ni pamoja na Sabuni za kufulia na kuogea, Dawa za meno na miswaki, mafuta ya kupaka, nguo, juisi Nk. 
Ojuku Mgedz ni Msimamizi wa kituo katika kambi hiyo ya wazee Nunge Kigamboni jijini Dar es Slaam, akiwakaribisha kinamama ambao ni wananchama wa kikundi cha mshikamano cha Mbweni walipofika katika kambi hiyo kutoa misaada ya viyu mbalimbali leo Tarehe 14 Oktoba 2017.
Mmoja wa wazee hao akipokea msaada uliotolewa na kinamama wa kikundi cha Mshikamano cha Mbweni, katikati ni Mwenyekiti wa kikundi hicho, Beatrce Njanda pamoja na katibu wa kikundi hicho Florence lema, walipotembelea kambi ya wazee iliyopo Nunge Kigamboni jijini Dar es Aalaam.

Mmoja wa wazee hao waliopata msaada wa vitu mbalimbali kwa kinamama wa kikundi cha Mshikamano cha Mbweni.
 Kinamama wa kikundi cha Mshikamano cha Mbweni wakiwa katika harakati za kugawa msaada wa vitu mbalimbali kwa wazee wanaoishi katika kambi ya wazee Nunge Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Kikundi hicho kinaongozwa na Mwenyekiti Beatrce Njanda, Makamo Mwenyekiti Grace Magembe, Mweka hazina Judithi manongi, Katibu Florence lema, Katibu msaidizi Veronica Mchele.