Monday, June 19, 2017

DAKTARI FEKI AKAMATWA MUHIMBILI.

DK FEKI
Kulia ni daktari feki ambaye amekuwa akijitambulisha kwamba ni Dk Abdallah Juma ambaye amekuwa akifanya kazi katika Maabara Kuu, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kushoto ni mmoja wa askari wa Muhimbili aliyemkamata daktari huyo.
...................
Hospitali  ya Taifa Muhimbili (MNH) imemtia mbaroni kijana mmoja aliyekuwa akijifanya daktari na alikuwa akijitambulisha kwa wagonjwa kwamba anaitwa Dk Abdallah Juma.

Mtu huyo alikuwa akijifanya kutoa huduma katika Maabara Kuu. Uongozi wa hospitali hiyo umesema kuwa kijana huyo ni daktari feki na si daktari kama alivyokuwa akijitambulisha na kwamba amekamatwa baada ya kuwekewa mtego na askari wa hospitali hiyo.

Uongozi wa hospitali hiyo umesema kuwa walinzi walikuwa wakimtilia shaka na kuanza kumfuatilia hadi walipofanikiwa kumkamata.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha amesema hospitali imeweka mikakati mbalimbali ya kupambana na wahalifu wakiwamo watu wanaojiita ni madaktari kama huyo ambaye amekamatwa leo.

ZIARA YA RAIS MAGUFULI MKOANI PWANI.

ZIA

Sunday, June 18, 2017

NGURUWE MARUFUKU MJI WA KIBAHA KUINGIA NA KUCHINJWA.

NGURU
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

HALMASHAURI ya Mji wa Kibaha ,mkoani Pwani imepiga marufuku uingiaji na uchinjaji wa nguruwe ili kukabiliana na ugonjwa wa homa ya nguruwe African Swine Fever,ambao  unadaiwa kuingia .

Tangu ugonjwa huu uingie jumla ya nguruwe 71 wameshakufa na baada ya kufanyiwa uchunguzi wa awali kupitia dalili za wanyama hao na kwa wale waliokufa viashiria vilionyesha ni ugonjwa huo.

Ofisa Habari wa Halmashauri ya Mji wa wa Kibaha ,Innocent Byarugaba alipozungumza na mwandishi hizi alisema halmashauri hiyo pia imezuia kuingiza nguruwe .

Byarugaba alieleza ugonjwa huo uliingia mwanzoni mwa mwezi may kwenye kata mbili za Picha ya Ndege na Viziwaziwa eneo la Mikongeni.

“Wananchi wawe na tahadhali ,ugonjwa huu tayari umesababisha vifo vya nguruwe 71 na baada ya kufanyiwa uchunguzi wa awali kupitia dalili za wanyama hao na kwa wale waliokufa viashiria vilionyesha ni ugonjwa huo,” alisema Byarugaba.

Alisema hatua za awali zilizochukuliwa ni pamoja na kuzuia nguruwe kuingia na kutoka katika maeneo yaliyokuwa na viasharia .

“Sampuli mbalimbali za nguruwe waliokufa zilichukuliwa na kupelekwa maabara kuu ya mifugo Temeke Jijini Dar es Salaam kwa uchunguzi na kubaini uwepo wa ugonjwa huo ,” alisema Byarugaba.

Hata hivyo ugonjwa wa African Swine Fever,ambao  unadaiwa kuingia  kwa nguruwe hauwezi kuambukiza binadamu ila madhara yake makubwa ni kuteketeza nguruwe wengi asilimia 100,kwa muda mfupi na kusababisha hasara kwa mfugaji.

Byarugaba alitaja dalili za ugonjwa huo ni kuvuja na kusambaa kwa damu kwenye viungo vya mwili , homa kali, kupumua kwa shida, kutapika, vifo ndani ya siku mbili hadi 10 na muonekano wa damu kuvilia kwenye viungo mbalimbali vya ndani vya nguruwe baada ya kumpasua.

Alieleza kufuatia ugonjwa huo ,idara ya mifugo na uvuvi katika halmashauri ya mji wa Kibaha ,wataalamu wake inatoa elimu kwa wafugaji ili kudhibiti,kwa kupita kata na mitaa .

Ugonjwa huo hushambulia nguruwe na hauna tiba kwa wanyama wanaoupata na husababisha vifo vingi unapotokea hasa kwa wanyama wakubwa.

MAGAZETI YA LEO TAREHE 18 JUNI 2017.