Friday, March 17, 2017

RAIS DKT. MAGUFULI ATOA MAELEKEZO BAGAMOYO KUHUSU WAFUGAJI NA WAKULIMA

fuka3
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maagizo kwa Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid Mwanga  baada ya kuongea na wanakjijiji wa  Fukayosi wilayani humo aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji   akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017.
fuka1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza changamoto za  wakulima na  wafugaji kutoka  kwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid  Mwanga katika kijiji cha Fukayosi akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017.
 fuka2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wanakjijiji wa  Fukayosi  wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji 
 akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017
 fuka4
Baadhi ya wananchi wakishangilia hotuba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli wakati alipoongea nao katika kijiji cha Fukayose wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
fuka5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na wanakjijiji wa  Fukayosi wilayani humo aliposimama  kwa muda na hatimaye kutoa maelekezo ya namna ya kutatua migogoro kati ya wakulima na wafugaji  akiwa njia kuelekea Dar es salaam akitokea  katika ziara ya kikazi ya Dodoma leo Machi 17, 2017.
PICHA NA IKULU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Alhaji Majid Mwanga kuwasaka, kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wafugaji wote wanaodaiwa kuhusika katika matukio ya kuwashambulia kwa viboko wananchi wa Kijiji cha Fukayosi kilichopo Wilayani humo.

Mhe. Dkt. Magufuli aliyekuwa akisafiri kwa gari kutoka Dodoma kwenda Jijini Dar es Salaam ametoa agizo hilo leo tarehe 17 Machi, 2017 aliposimama katika kijiji hicho baada ya kuona wananchi wengi wakiwa wamekusanyika kando ya Ofisi ya Kata.

Baada ya kusimamisha msafara wake, Mhe. Rais Magufuli aliwaita wananchi waliokuwa wamekusanyika huku wakiwa wameshika mabango yaliyoandikwa ujumbe wa kutaka wafugaji wa jamii ya Wamang’ati waondolewe na kisha akatoa nafasi kwa baadhi yao kueleza dukuduku lao.

Wananchi hao ambao ni wakulima na mfugaji mmoja aliyejitokeza wakaeleza kuwa Wamang’ati wamekuwa wakiwanyanyasa kwa kuingiza mifugo katika mashamba yao ya mazao na wakithubutu kuwakataza wamekuwa wakichapwa viboko na baadhi kuuawa.

Katika majibu yake, pamoja na kutaka wote wanaodaiwa kuwashambulia wananchi kwa viboko wakamatwe Mhe. Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kukomesha mara moja vitendo vya wafugaji kuwapiga wakulima na wakulima kuwapiga wafugaji, na pia kukomesha vitendo vya wafugaji kulisha mifugo yao katika mashamba ya wakulima.

“Kuanzia leo isitokee mfugaji kumpiga mkulima, mkulima kumpiga mfugaji wala mfugaji kulisha mifugo yake kwenye mashamba ya wakulima, na suala hili nitalifuatilia mimi mwenyewe.

“Kwa hiyo Mkuu wa Wilaya na Viongozi mlishughulikie hili kabla mimi sijawashughulikia nyinyi, wale waliopiga watu, nataka wote wakamatwe na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria” amesema Mhe. Dkt.Magufuli.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

17 Machi, 2017

Thursday, March 16, 2017

MARUFUKU KUFUNGISHA NDOA BILA YA CHETI CHA KUZALIWA.

Image result for Harrison Mwakyembe images
Waziri wa katib na Sheria,  Harrison  Mwakyembe amepiga marufuku kufungisha ndoa  bila ya wanandoa kuwa na vyeti vya  kuzaliwa.

Waziri  Mwakyembe amesema  ni  marufuku  kwa sheikh,  Ustadhi, Mchungaji au  Padri  kufungisha  ndoa  bila  ya wahusika  kuwa na vyeti  vya  kuzaliwa.

Aidha,  aliwataka  wakuu  wa wilaya  kusimamia  agizo hilo  ili kila mtu  awe na cheticha kuzaliwa kabla ya  kufunga ndoa.

Aliongeza kwakusema kuwa hilo ni agizo  linapaswa kutekelezwa na kwamba utekelezaji  wake  utaanza  rasmi tarehe 01 May  2017 nchi nzima.