Mkuu wa
wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga amempa siku moja kamanda wa polisi wilaya
ya Kipolisi Chalinze SSP Janeth Magomi,
kumuondoa mkuu wa kituo cha polisi cha
Wami kufuatia tuhuma za kuwapendelea
wafugaji na kuwanyanyasa wakulima
na kupelekea kushindwa kuwachukulia hatua wafugaji
wanaoingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima.
Agiza hilo
amelitoa kwenye Mkutano wa
hadhara uliofanyika katika kijiji cha
Mandela kata ya Mandela ambapo awali wananchi walipata nafasi ya kutoa malalamiko yao mbele ya mkuu wa wilaya na kufanya kero kubwa iliyotawala katika mkutano huo ni
kuhusu wafugaji kuingiza mifugo kwenye
mazao ya wakulima na kwamba polisi
waliopo kituo cha polisi Wami
wameshindwa kuwasimamia ili kudhibiti hali hiyo.
Akizungumza mbele ya mkuu
wa wilaya mzee mmoja alisema
aliwahi kufika kituo cha PolisiWami
kutoa Taarifa ya kuliwa mazao yake,
lakini hatua waliyochukua Polisi ni
kumwambia huyo mzee akatafute mgambo ili
amkamate mfugaji aliyeingiza mifugo kwenye shamba lake jambo
limemsikitisha mzee huyo.
Aidha, wananchi mbalimbali walizungumza katika mkutano huo, wamelalamikia kitendo cha
wafugajikuwa na uwezo wa kuharibu mazao ya wakulima bila ya kuchukuliwahatua
yoyote.
Kero hizo za wafugaji kwa wakulima ni pamoja na
mifugo kula mazao ya wakulima na hata
wanapotakiwa kutoa fidia ya mazao hayo
wamekuwa hawatimizi kwa kile
kinachodaiwa kulindwa na Polisi, mkuu wa
wilaya anachukua jukumu la kuomba namba za simu za wafugaji wanaodaiwa
na wakulima na kuwapigia simu ili walipe fidia za wakulima.
Mkuu wa Polisi wilaya ya Kipolisi Chalinze. Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP
Janeth Magomi akimsikiliza mkuu
wa wilaya wakati wa mkutano
uliofanyika kijiji cha Mandela kata ya Mandela Halmashauri ya Chalinze, kulia ni mkuu
wa kituo cha Polisi Wami ambae
mkuu wa wilaya ameagiza ahamishwe.
Wazee wa Kijiji cha Mandela
wakipiga makofi mara baada ya
mkuu wa wilaya kutoamaamuzi ya
kuhamishwa kwa mkuu wa kituo cha polisi
Wami.
Wananchi wa kijiji cha Mandela wakimsikiliza mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga alipofanya mkutano wa hadhara na kusikiliza
kero mbalimbali za wananchi wa kata ya Mandela, Halmashauri ya Chalinze
wilayani Bagamoyo.