Monday, September 26, 2016

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI, AZINDUA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI, KITAIFA MJINI GEITA LEO, AAGIZA MATUTA KWENYE BARABARA KUU YAONDOLEWE.

mass6
Washiriki wa maonesho (waendesha bodaboda) wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyozinduliwa katika Viwanja vya CCM Kalangalala, mjini Geita leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Hatutaki ajali tunataka kuishi salama”. Maadhimishjo hayo yalizinduliwa na Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni ambapo Katika hotuba yake Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe.
 mass1

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akitoa hotuba ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani aliyoizindua Kitaifa mjini Geita leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “HATUTAKI AJALI, TUNATAKA KUISHI”. Katika hotuba yake, Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 mass2

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimsikiliza Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka Makao Makuu, Koplo Faustina Ndunguru wakati alipokuwa anatoa maelezo jinsi magari mbalimbali yanavyovunja sheria za barabarani. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa maonyesho hayo yanayofanyika Kitaifa mjini Geita, Mhandisi Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 mass3

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiyaangalia maandamano ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo yanafanyika Kitaifa katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita, yalipokuwa yanaingia katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuadhimisha wiki hiyo. Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 mass4

Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimpa zawadi ya Kombe la Ushindi wa kwanza Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam, Veronica Innocent, ambaye alishinda nafasi ya kwanza katika uchoraJi wa picha zinazoonyesha usalama barabarani ambayo zilipambanishwa katika shule za Mkoa wa Dar es Salaam na Geita. Masauni aliyazindua Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, ambayo yanafanyika Kitaifa, katika Viwanja vya CCM Kalangalala, mjini Geita. Masauni katika hotuba yake aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 mass5

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Kamishna, DCP-Mohamed Mpinga akizungumza katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inayofanyika Kitaifa katika Viwabya vya CCM Kalangalala mjini Geita. Maadhimisho hayo yalizinduliwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni.

WAZIRI MKUU AMPA AFISA ELIMU PWANI WIKI MOJA KUPELEKA WALIMU RUFIJI

kh01
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiingia  kwenye uwanja wa michezo wa Kibiti wilayani Kibiti ambapo Waziri Mkuu alihutubia mkutano wa hadhara , Septemba 26, 2016.   . Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 kh3

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akimshukuru Mzee Abadallah Ngwele  baada ya kupokea madawati 10 yaliyotolewa  na wazee wa Kibiti katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa michezo wa Kibiti, Septemba 26, 2016.  Kushoto ni mkewe Mary na watatu kulia ni Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
...................................


WAZIRI MKUUkuu ,Kassim Majaliwa ametoa wiki moja kwa Afisa Elimu Mkoa wa Pwani, Yussuph Kipengele kupeleka walimu wa kufundisha masomo ya kidato cha tano na sita katika shule za sekondari za Mkongo na Utete wilayani Rufiji.

Ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Septemba 26, 2016) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Jumba la Maendeleo wilayani Rufiji.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya Mbunge wa Rufiji, Muhammed Mchengelwa kumwambia kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa walimu wa kidato cha tano na sita licha ya kuwa na shule.

“Hatuwezi kuwa na shule ambazo hazina walimu, nasikia hapa anayefundisha ni Mkuu wa shule na mwalimu mmoja tu, wakati kule Kibaha kuna walimu walmerundikana ,sasa fanya realocation tarehe 4,Oktoba uniletee taarifa walimu wamefika Rufiji.”,alisema Waziri Mkuu.

Akizungumzia suala la upungufu wa watumishi wa umma kwenye sekta mbalimbali, Waziri Mkuu alisema baada ya kazi ya uhakiki watumishi hewa itakapokamilika, serikali itaangalia kwenye maeneo yenye upungufu na hivyo kutangaza ajira.

“Hivi sasa serikali inakamilisha masuala ya uhakiki wa watumishi, tukimakamilisha na kujua idadi ya watumishi na maeneo yenye upungufu tutaanza tena kuajiri, tulisitisha kupisha kwanza kazi hii,alisema Waziri Majaliwa.

Kuhusu migogoro ya wakulima na wafugaji Waziri, Mkuu alisema  watendaji wa halmashauri na vijiji wanapaswa kutenga maeneo ya wafugaji na wakulima na kutaka mifugo isiongezwe kwenye maeneo ambayo hayajaruhusiwa.

Alisema wenyeviti wa vijiji wanapaswa kusimamia utekelezaji wake katika mpango wa matumizi bora ya ardhi na kwamba atakayeruhusu idadi kubwa ya mifugo kuingia kijijini zaidi ya ile iliyokubalika atawajibishwa ikiwemo kufukuzwa kazi na hatua nyingine za kisheria.

“Hatuwezi kuendelea kuwa na watumishi wasio na nidhamu, wale wote watakaoingia mifugo zaidi ya uwezo wa kijiji wafukuzwe kazi na kuchukuliwa hatua, lakini pia wafugaji ni marufuko kuingiza mifugo kwenye mazao ya wakulima”alisema Waziri Mkuu.

Kuhusu ujenzi wa barabara ya lami kwenda makao makuu ya wilaya ya Rufiji, Utete, Waziri Mkuu aliahidi kuchukua ombi hilo na kusema bajeti ijayo litatengewa fedha kuwa ajili ya kufanya maandalizi ya upembuzi kuona gharama yake kabla ya kutangaza zabuni ya ujenzi.

Kuhusu utengenezaji wa madawati, Waziri Mkuu alisema ifikapo Oktoba 30, mwaka huu kila wilaya nchini inapaswa iwe imekamilisha utengenezaji wa madawati hayo kwenye shule nchini.

Aidha, alisema ipo miradi mingi inayoendeshwa kwa maslahi binafsi ukiwemo mradi wa Bonde la Rufiji(RUBADA), ambao wamebaini kuna ubabaishaji mkubwa, hivyo wamepeleka timu ya wataalamu kuhakiki ili wale wabadhirifu wachukuliwe hatua.