Tuesday, August 30, 2016

AJALI, SANZALE BAGAMOYO, GARI LA PEPSI LAGONGANA NA ROLI KUBWA LA MIZIGO.

Magari mawili ya mizigo yamegongana mchana huu eneo  la Sanzale kichem  chem kati ya Roli kubwa lenye tera namba T.682 DFF la Kampuni ya  PWANI HAULIERS LTD. (PHL) lililokuwalimebeba mzigo, na Canter ya pepsi  yenye namba T. 912 DCC ambalo  lilikuwa limebeba soda.

Kwa mujibu wa dereva Roli lenye Tera, Shomari Shomari aliiambia Bagamoyokwanza kuwa yeye alikuwa anakunja kuingia kiwandani kuingiza mzigo ambapo kutokana na  urefu wa gari alilazimika kuzidi upande wa kulia  ili apate kona ya kukunja kuingia kushoto kwenye Kiwanda.

Shomari aliendelea kusema kuwa, mara baada yeye kuzidi upande wa kulia akiwa ameshaakunja kuingia kusho  kiwandani, mwenye gari ya soda amekuja nyuma yake na kupitia kushoto  ambapo gari ya soda ilikwenda kugonga moja kwa moja kwenye mlango Roli kubwa na kusababisha Ajali iliyopelekea Dereva  wa Gari la Soda kuumia na kukimbizwa Hospitali huku  soda zikiwa zimevunjika.

Wananchi mbalimbali walioongea na bagamoyokwanza, walisematukio limesababishwa na Dereva wa gari la soda kwani yeye hakupaswa kupita  kushoto na badala yake alitakiwa kusubiri  gari ya mbele yake imalize kukata kona ndipo yeye aendelee na safari yake.




VIONGOZI WA CHADEMA WAHOJIWA POLISI NA KUACHIWA KWA DHAMANA.

index
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Mbowe amehojiwa Central Polisi  kwa saa zaidi ya 5 na kutoka kwa.dhamana,akiwa na viongozi wakuu wengine  walielekea Makao Makuu ya Chama hicho yaliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam, jana Jumatatu.29/8/2016.

Viongozi waliokwenda polisi kwa mahojiano ni M/kiti wa Chadema Taifa, Mhe. Mbowe, Katibu Mkuu, Mhe. Vincent Mashinji, Mhe. Edward Lowassa, Mhe. John Mnyika,Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Mhe. Said Issa Mohammed, Mhe. Tundu Lissu,Profesa Baregu ambapo walisindikizwa na Waheshimiwa Wabunge ambao walibaki nje wakiwasubiri, viongozi hao wametoka kwa dhamana na wametakiwa kuripoti polisi tarehe 1 Septemba 2016.

MKURUGENZI WA FULLSHANGWEBLOG AKABIDHIWA TAARIFA YA UCHAGUZI MKUU 2015.

1
Bw . Mohamed Seif Ofisa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tume hiyo  akikabidhi kwa  Bw. John Bukuku Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangweblog Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2015, Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye mgahawa wa Mokka City Mtaa wa Samora jijini Dar es salaam.
 2
Bw. John Bukuku Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangweblog Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2015 mara baada ya kukabidhiwa rasmi.
 3
Bw. John Bukuku Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangweblog Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2015.