Thursday, August 18, 2016

IGP MANGU, AWAAGA ASKARI 14 WA KIKOSI MAALUM CHA POLISI (S.F.U) WANAOKWENDA JORDAN



 MNG1
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akimuuaga PC Prosper Yenda yenda wa kikosi maalum cha Jeshi la Polisi ( S.F.U) ambaye ni miongoni mwa askari 14 wanaokwenda nchini Jordan kwa kozi maalum ya kupambana na uhalifu na wahalifu.

 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akiwa katika picha ya pamoja na askari 14 wa kikosi maalum cha Jeshi la Polisi (S.F.U) ambao wanaokwenda nchini Jordan kwa kozi maalum ya kupambana na uhalifu na wahalifu. (Picha na Tamimu Adam- Jeshi la Polisi)

MRISHO GAMBO ATEULIWA KUWA MKUU WA MKOA ARUSHA, FELIX NTIBENDA ATENGULIWA.

Mkuu wa Mkoa mpya wa Arusha,Mrisho Gambo aliyeteuliwa na Rais,kuapishwa kesho ijumaa Ikulu jijini Dar.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, ambae uteuzi wake umetenguliwa leo na Rais.
..................................................................................................................
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya uongozi na kumteua Bw. Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuanzia leo (Alhamisi, Agosti 18,2016).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Bw. Gambo anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Felix Kijiko Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Amesema Bw. Ntibenda anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa majukumu mengine.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha. Ataapishwa kesho (Ijumaa, Agosti 19, 2016) saa 3 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
ALHAMISI, AGOSTI 18, 2016.


MAGAZETINI LEO TAREHE 18-08-2016

MAK

Wednesday, August 17, 2016

FEDHA ZA WANAFUNZI HEWA VYUO VIKUU, WAZIRI ATOA SIKU 7 FEDHA HIZO ZIREJESHWE.

index
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof.  Joyce Ndalichako ametoa siku saba kuanzia Agosti 17, 2016 kwa vyuo vikuu kurejesha fedha zilizopokea ambazo ni za wanafunzi ambao hawapo chuoni.

Prof.  Ndalichako ameyasema hayo leo, jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya taarifa la zoezi la uhakiki wa wanafunzi wanufaika wa mikopo vyuo vya Elimu juu.

Prof.  Ndalichako amesema kuwa uhakiki wa wanafunzi hao umefanyika katika vyuo 31 kati ya vyuo 81 vilivyopo nchini, Katika utafiti huo wanafunzi 2,192 wameshindwa kuhakiki majina yao, hivyo kushindwa kuthibitisha uwepo na uhalali wa wanafunzi hao.

“Mikopo ya Wanafunzi hao imesitishwa na kwa wale ambao ni wanafunzi halali lakini walishindwa kujihakiki itabidi waombe tena mkopo,” alifafanua Mhe. Ndalichako.

Ameendelea kwa kusema kuwa, kwa mwaka wa fedha 2015/16 wanafunzi hao hewa wameigharimu Serikali kiasi cha shilingi 3,857,754,460, kiasi ambacho kinatakiwa kurejeshwa na vyuo ambavyo wanafunzi hao wamebainika.

Aidha, Prof.  Ndalichako amesema kuwa taarifa hiyo imekabidhiwa kwenye vyombo vya sheria ili kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kufanya  udanganyifu na kusababisha Serikali hasara ya mabilioni ya fedha.

Vile vile Prof. Ndalichako amewataka wakuu wa vyuo kuweka mfumo wa kuhakiki usahihi wa matokeo ya wanafunzi yanayotumwa Bodi ya Mikopo  kutokana na vyuo vingi kubainika kuwepo kwa udanganyifu mkubwa kwenye matokeo ya wanafunzi ambao hawakufanya mtihani au waliofeli na kuandikiwa wamefaulu ili waendelee kupata mikopo.