Tuesday, August 16, 2016

MBUNGE WA MKURANGA AKABIDHI MADAWATI 537 KWA HALMASHAURI YAKE.



Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega (katikati alie simama) akiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya mkuranga Msham Munde, mkuu wa wilaya hiyo Filberto Sanga, na mdau wa maendeleo Hamisi Njomoke mara baada ya kukabidhi madawati 537 ya mbunge wilayani humo.

Sehemu ya madawati hayo

Walimu wa shule ya msingi Misasa wakimsikiliza mbunge wa Jimbo la mkuranga Abdallah Ulega mara baada ya kuzuru shuleni hapo kwa lengo la kuwahamasisha kufanya kazi kwa bidii na kwamba yeye kama kiongozi wao yupo pamoja nao .

Akina mama wa kijiji cha Misasa kilichopo kata ya Likanga wakimsilikiliza mbunge wa Jimbo hilo Abdallah Ulega kwa makini wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru uliofanyika kijiji hapo ambapo pia walipata nafasi ya kuwasilisha changamoto zao hususani kukosekana kwa Zahanati na maji safi.

..............................................................................................................................................


Mbunge wa jimbo la mkuranga Abdallah Ulega amekabidhi madawati 537 kwa halmashauri ya wilaya hiyo, huku akiwataka viongozi wakiwamo madiwani wa kata mbalimbali kusimamia vizuri madawati hayo ili kutambua mchango mkubwa wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi alisema kuwa madawati hayo yametokana na fedha zao ambazo zilibaki baada ya kubana matumizi katika ofisi ya bunge na kwa kauli moja walikubali kumkabidhi Rais Dkt. Magufuli, ambapo naye kwa kutambua changamoto ya madawati akaelekeza fedha hizo zipelekwe kutengeneza madawati hayo.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Msham Munde alimshukuru Mbunge huyo na kudai kuwa uchangiaji wa madawati hayo ni mchakato endelevu hivyo wadau waendelee kujitokeza kuchangia huku akisisitiza kwamba kwa asilimia kubwa yamekwenda kutatua kero hiyo.

Wakati huohuo mdau wa maendeleo Hamisi Njomoke alimkabidhi mbunge wa jimbo hilo Ulega Madawati 50 kama sehemu ya kumuunga mkono mbunge paoja na Rais Dkt Magufuli huku akiwataka wadau wengine kujitokeza kuchangia ili watoto wasome katika mazingira rafiki.



MAZISHI YA MZEE ABOUD JUMBE MWINYI.



 MAJ5
Viongozi wa kitaifa wakishiriki katika sala ya kumwombea Ras wa Awamu ya Pili wa Zanzibar, marehemu Alhaj Abood Jumbe iliyofanyika kwenye msikiti, Mwembeshauri Zanzibar Agosti 15, 2016.  Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais, Mstaafu, Dkt. Mohammed Bilal, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Karume, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)MAJ6
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar, Alhaj Abood Jumbe katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu, Migombani Zanzibar Agosti 15, 2016. (Picha na Ofisi a Waziri Mkuu)MAJ7
Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Karume, Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Ghalib Bilai wakiwa katika mazishi ya Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar, Alhaj  Abood Jumbe yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu Migombani, Zanzibar Agosti 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu_)MAJ9
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka udongo kwenye kaburi la Rais wa Awamu ya Pili wa   Zanzibar Alhaj Abood Jumbe katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Marehemu Migombani Zanzibar, Agosti 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)MAJ4