Monday, July 18, 2016

MWENYEKITI WA KITONGOJI BAGAMOYO ATIWA MBARONI, KWA TUHUMA ZA KUTAKA KUOZESHA MWANAFUNZI.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga, mwenye miwani kushoto, akiongea na viongozi wa kimasai kuhusu mikakati ya kuwapeleka watoto shule.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Lulenge kata ya Ubena wilayani Bagamoyo, Lukasi Sultani, amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kula njama za kutaka kumuozesha mwanafunzi wa kidato cha kwanza.

Mwenyekiti huyo wa Kitongoji, ambae piya ni mwenyekiti wa wafugaji wilaya ya Bagamoyo, amekamatwa kufuatia  taarifa kutoka kwa raia wema waliovujisha siri  huku mwanafunzi akiwa amepatikana kabla ya ndoa kufungwa.

Akizungumza na waandishi wa Habari mkurugenzi wa shirikan la kupinga unyanyasaji wa kijinsia na ndoa za utotoni, ESUPAT (CHEMA) Ester Labani Moreto, alisema mara baada ya mwanafunzi Margret Minaura kufaulu mwenyekiti huyo alimuombea uhamisho kutoka shule ya Ubena kwenda shule ya Mikumi.

Aliongeza kuwa, mara baada ya kufuatilia katika shule ya Mikumi iligundulika kuwa hakufika shuleni na kwamba alifichwa kwa lengo la kuozeshwa kwa mtoto wa mwenyekiti huyo wa kabila la jamii ya wafugaji.

Ester, alisema kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ikiongozwa na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, iliandaa mtego na baadae kukamatwa mwenyekiti huyo na kumfikisha mahakani.

Aidha, alisema mwanafunzi huyo yupo chini ya Shirika lake la ESUPAT (CHEMA) na kwamba kwa sasa anafanyiwa utaratibu wa kupelekwa shule ili kuendelea na masomo ambapo aliwaomba wadau mbalimbali, kusaidia shirika lake kwakuwa linakabiliwana na changamoto kadhaa katika kulea watoto wenye mazingira magumu na wajane.

Akielezea hali hiyo, mwanafunzi aliyenusurika kuolewa Margret Minaura, alisema yeye aliambiwa anahamishwa shule na hakutakiwa kwenda kwenye shule aliyochaguliwa ambapo mwenyekiti huyo akishirikiana na mama mzazi wa msichana huyo, walipanga njama zakumuozesha kwa mtoto wa mwenyekiti anaetuhumiwa.

Hata hivyo, Margret, ambae ni yatima wa kufiwa na baba yake, alisema bado anatamani kusoma na kwamba anahitaji msaada kwa wadau mbalimbali ili aweze kuendelea na masomo.

Aidha, Margret alimshukuru mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga, kwa kufanikisha kumnusuru na ndoa ya utotoni, na kwamba amemuomba mkuu wa wilaya kuendeleza msako huo kwakuwa wapo watoto wengine ambao wanaolewa hali ya kuwa bado ni wanafunzi shule za msingi au Sekondari hasa katika kabila wamasai.

"Yupo mwanafunzi mwenzangu tumemaliza wote darasa la saba na yeye amefaulu, lakini ameolewa, namuomba mkuu wa wilaya awanusuru wasichana wengine kama mimi ili wapate elimu"  Alisema Margret.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga, alitoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kuwaozesha watoto wadogo hasa wale wenye umri wa kwenda shule ili kila mtoto apate haki ya kupata Elimu ambayo inatolewa bure.

Aliongeza kuwa msako utapita wa nyumba hadi nyumba hasa kwa jamii wa wafugaji ambao  wanaonekana kutopenda kuwapeleka watoto shule ili kuwakamata wazazi ambao watoto wao hawakuwapeleka shule.

Mkurugenzi wa shirika linalopinga ukatili wa kijinsia, na ndoa za utotoni, ESUPAT, Ester  Labani Moreto
Msichana aliyenusurika kuolewa hali ni mwanafunzi, Margret Minaura, ambae bado anahitaji kusoma.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga, akisikiliza hoja za kina mama wa kimasai katika kitongoji cha Kivuga kata ya Ubena ambao watoto wao hawajapelekwa shule.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, akiwa na watoto wakimasai ambao hawajapelekwa shule, katika kitongoji cha Kivuga, kata ya Ubena.
Wananchi wa jamii jamii ya kimasai wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, katika mkutano uliofanyika kijiji cha  Pongwe Msungura.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga, akikabidhiwa mtoto wa kimasai mara baada ya kuwatembelea katika makazi yao kitongoji cha Kivuga.

Sunday, July 17, 2016

DC. BAGAMOYO, AREJESHA HEKA 900 KWA WANANCHI ZILIZOCHUKULIWA NA WAWEKEZAJI BILA YA KUFUATA SHERIA.

Mkuu wa wilaya  ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga, (aliyesimama) akiongea na wananchi katika kijiji cha Pongwe Msungura, Kata ya Msata, wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Saidi Omari Zikatimu, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze, Edesi Philip Lukoa, wa pili kulia ni Diwani wa Kata ya Msata, Selestin Cham Semiono.


Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo MajidHemed Mwanga, amerudisha heka 900 kwa wananchi, zilizokuwa zinamilikiwa na wawekezaji bila ya kufuata sheria ya umiliki Ardhi, katika kijiji cha Pongwe Msungura kata yaMsata.

Uamuzi huo aliutangaza katika mkutano wa hadhara ulioitishwa kijijini hapo ili kukjadili kero mbalimbaliza wananchi ikiwemo tuhuma zaubadhilifu wa fedha kwa viongozi wa Halmashauri ya kijiji hicho pamoja na kufanya maamuzi ya kugawa Ardhi bila ya kufikisha taarifa kwenyemkutanomkuu wa kijiji.

Majid alisema wawekezaji hao wawili ambao kila mmoja anadai  kumiliki heka 500 hali ya kuwa taratibu za kisheria hazijafutwa, huku wananchi wa kijiji cha Pongwe Msungura ambao ndio wajumbe wa mkutano mkuu wa kijiji,walithibitisha kupitisha umiliki wa heka 50 tu,kama sheria inavyowataka na kwamba swalalakumiliki heka 500 kila mmoja hawalitambui.

Kufuatia hali hiyo Mkuu wa wilaya aliwataka wawekezaji hao kutoa maelezo namna walivyopata maeneo hayo ambapo walionyesha mihutasari ya kijiji ambayo imewapitishia kumiliki heka 500 kila mmoja.

Ili kujiridhisha na mihutasari hiyo, mkuu wa wilaya alilazimika kusoma muhutasari wa tarehe 08 julai 2013 unaodaiwa kuandaliwa na mkutano wa kijiji ili kupitisha heka 500 kwa muwekezaji ambapo aliita jina moja baada lingine ambapo wananchi  wote waliukataa muhutasari huo kwamba hawaujui.

Baada ya hali hiyo, mkuu wa wilaya aliamuru kila muwekezaji mmoja kati ya hao wawili kurudisha heka 450 na kubaki na 50 kama walivyopitishiwa na mkutano wa kijiji  na hivyo kufanikiwa kurudisha heka 900 kwa wananchi.

Aidh,baada ya kasoro mbalimbali zilizobainika katika mkutano huo, wajumbe wa Halmashauri ya kijiji walipiga kura ya kumuondoa mwenyekiti wa kijiji hicho Mbaraka Rajabu Mwelekwa,nakwamba baada ya siku 90 mkurugenzi ataitisha mkutano utakaomchagua mwenyekit mpya wakijiji cha Pongwe Msungura

Wawekezaji walionyakanywa jumla ya heka 900, kwa kuzipata bila ya kufuata sheria ya umiliki wa Ardhi vijijini, wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Bagamoyo katika kijiji cha Pongwe Msungura kata ya Msata.
Wananchi wa kijiji cha Pongwe Msungura wakiinua mikono juu, ikiwa ni ishara ya kuunga mkono maamuzi ya mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, kuwarudishia Ardhi mikononim mwao ili ikitolewa itolewe kwa kufuata utaratibu.



Mwenyekiti wa kijiji cha Pongwe Msungura, Mbaraka Rajabu, aliyeondolewa madarakani na wajumbenwa Halmashauriya kijiji na kuungwa mkono na wananchi ambao ndio wajumbe wa mkutano mkuu, kwa matumizi mabaya ya madaraka.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Bagamoyo,wakifuatilia mkutano wa Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama, ambae ni mkuu wa wilaya.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Bagamoyo,wakifuatilia mkutano wa Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama, ambae ni mkuu wa wilaya.

Saturday, July 16, 2016

RAIS DKT. JOHN MAGUFULI AWAPANDISHA VYEO MAAFISA WA POLIS, NA KUTEUA VIONGOZI NA WATENDAJI WA TAASISI MBALIMBALI ZA SERIKALI.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka aliyopewa amefanya uteuzi wa viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za Serikali, na pia amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;
1.   Mhe. Augustino Lyatonga Mrema.
·        Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia leo tarehe 16 Julai, 2016.
·        Mhe. Augustino Lyatonga Mrema anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mstaafu Mhe. Eusebia Nicholaus Munuo ambaye muda wake umemalizika.
2.   Prof. William R. Mahalu
·        Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.
3.   Prof. Mohamed Janabi
·        Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
4.   Prof. Angelo Mtitu Mapunda
·        Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
5.   Bi. Sengiro Mulebya
·        Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
6.   Bw. Oliva Joseph Mhaiki
·        Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
7.   Mwl. Winifrida Gaspar Rutaindurwa
·        Ameteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
8.   Dkt. Charles Rukiko Majinge
·        Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.
9.   Dkt. Julius David Mwaiselage
·        Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
Kupandishwa Vyeo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa 25 wa Jeshi la Polisi kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) na kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP).
Waliopandishwa vyeo hivyo ni kama ifuatavyo;
1.      Essaka Ndege Mugasa
2.      Adamson Afwilile Mponi
3.      Charles Ndalahwa Julius Kenyela
4.      Richard Malika Revocatus
5.      Geofrey Yesaya Kamwela
6.      Lucas John Mkondya
7.      John Mondoka Gudaba
8.      Matanga Renatus Mbushi
9.      Frasser Rweyemamu Kashai
10.  Ferdinand Elias Mtui
11.  Germanus Yotham Muhume
12.  Fulgence Clemence Ngonyani
13.  Modestus Gasper Lyimo
14.  Mboje John Shadrack Kanga
15.  Gabriel G.A. Njau
16.  Ahmed Zahor Msangi
17.  Anthony Jonas Rutashubulugukwa
18.  Dhahir Athuman Kidavashari
19.  Ndalo Nicholus Shihango
20.  Shaaban Mrai Hiki
21.  Simon Thomas Chillery
22.  Leonard Lwabuzara Paul
23.  Ahmada Abdalla Khamis
24.  Aziz Juma Mohamed
25.  Juma Yussuf Ally
Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi wengine 34 kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP).

Waliopandishwa vyeo hivyo ni kama ifuatavyo;
1.      Fortunatus Media Musilimu
2.      Goyayi Mabula Goyayi
3.      Gabriel Joseph Mukungu
4.      Ally Omary Ally
5.      Edward Selestine Bukombe
6.      Sifael Anase Mkonyi
7.      Naftari J. Mantamba
8.      Onesmo Manase Lyanga
9.      Paul Tresphory Kasabago
10.  Dadid Mshahara Hiza
11.  Robert Mayala
12.  Lazaro Benedict Mambosasa
13.  Camilius M. Wambura
14.  Mihayo Kagoro Msikhela
15.  Ramadhani Athumani Mungi
16.  Henry Mwaibambe Sikoki
17.  Renata Michael Mzinga
18.  Suzan Salome Kaganda
19.  Neema M. Mwanga
20.  Mponjoli Lotson
21.  Benedict Michael Wakulyamba
22.  Wilbroad William Mtafungwa
23.  Gemini Sebastian Mushi
24.  Peter Charles Kakamba
25.  Ramadhan Ng'anzi Hassan
26.  Christopher Cyprian Fuime
27.  Charles Philip Ulaya
28.  Gilles Bilabaye Muroto
29.  Mwamini Marco Lwantale
30.  Allute Yusufu Makita
31.  Kheriyangu Mgeni Khamis
32.  Nassor Ali Mohammed
33.  Salehe Mohamed Salehe
34.  Mohamed Sheikhan Mohamed
Maafisa hawa wa Jeshi la Polisi Tanzania wamepandishwa vyeo kuanzia tarehe 15 Julai, 2016.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
16 Julai, 2016