Wednesday, July 6, 2016

SHEIKH NURDINI KISHKI, NA SWALA YA EID KATIKA VIWANJA VYA MBAGALA ZAKIEM JIJINI DAR ES SALAAM.

Sheikh Nurdini Kishiki akizungumza mara baada ya swala ya Eid el fitri leo katika viwanja vya Mbagala zakiem jijini Dar es Salaam.

Waislamu wakiwa katika viwanja vya Mbagala zakiem leo kwaajili ya swala ya Eid elftri.

Sehemu ya waislamu waliohudhuria ibada ya swala ya Eidi leo Jumatano  06/07/2016

Katika viwanja vya Magala zakiem jijini Dar es Salaam waislamu walitekeleza swala ya Eid el fitri leo.

PICHA ZA SWALA YA EID ILIYOSWALIWA LEO TAREHE 06 JULY 2016. MAENEO MBALIMBALI HAPA NCHINI.

Kushoto ni Diwani wa kata ya Nianjema Bagamoyo mjini Abdu Pyala akijumuika na waislamu wengine kwenye swla ya eidi iliyoswaliwa katika viwanja vya Istiqaama, Bong'wa mjini Bagamoyo.
Naibu Amiri wa Taasisi ya SirajulMunir Islamic Center (SIMIC) ya Bagamoyo Sheikh Fadhili Haji, akitoa hutuba ya swala ya eid iliyoswaliwa katika viwanja vya msikiti wa istiqaama Bagamoyo mjini
Mkuu wa wilaya ya Longido Bw. Daniel Chongolo (wa tatu kulia) akikabidhi zawadi za Idd kwa Masheikh wa misikiti ya mji wa Namanga na Longido mjini wilayani Longido leo,mkoani Arusha. Mh Chongo amekabidhi  zawadi hizo kwa misikiti 6 iliyopo wilayani Longido mapema Leo.
Mkuu wa wilaya ya Longido mkoani Arusha Bw. Daniel Chongolo akikabidhi zawadi za sikukuu ya Idd kwa Masheikh wa Misikiti ya Namanga na Longido mjini leo. Mkuu huyo wa wilaya pia ametumia nafasi hiyo kujitambulisha kwao.
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kasimu Majaliwa akisalimiana na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum, mara baada ya kuwasili katika viwanja vya mnazi mmoja leo kwaajili ya swala ya Eid el ftri.
Kutoka kushoto ni waziri mkuu Kasim Majaliwa, wapili ni Rais mstaafu wa awamu ya pili Aliy Hassan Mwinyi, watatu ni Sheikh mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum, na wanne ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Aliy Salum Hapi

Sheikh mkuu wa Tanzania, Mufti, Sheikh Aboubakari Zuberi akioa nasaha zake.
Waziri mkuu Kasim Majaliwa akielezea machache mara baada ya swala ya eid iliyoswaliwa katika viwanja vya mnazi mmoja jjijini Dar es Salaam.

Tuesday, July 5, 2016

DISCO TOTO BILA YA KIBALI MARUFUKU NCHI NZIMA.


WATAKAOFANYA FUJO BAGAMOYO SIKU YA SIKUKUU WAONYWA.

Kamati ya ulinzi na usalama Bagamoyo ikiwa kwenye kikao cha cha kujadili sherehe za siku kuu ya Eid el fitri.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Bagamoyo Majid Hemed Mwanga, wa pili kulia, wa tatu kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Aliy Aliy na wakwanza kulia ni Katibu tawala wa wilaya ya Bagamoyo Bi Elika Liyegela, wakiwa kwenye kikao cha kujidili hali ya usalama kipindi cha sikukuu ya Eid.

Monday, July 4, 2016

SOBA HOUSE BAGAMOYO YAFUTURISHA.

Baadhi ya vijana wanaopata huduma na kulelewa katika kituo cha Life and Hope Sober House Bagamoyo wakijiandaa kupata futari katika kituo hicho kilichopo Ukuni wilayani Bagamoyo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid Hemed Mwanga, akijumuika na wadau mbalimbali kupata futari katika kituo cha Life and Hope Sober House Bagamoyo.
Diwani wa kata ya Dunda Diksoni Makamba akipata futari Sober House.
Kutoka kulia ni mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga, wakatikati ni Mkurugenzi wa Green Park Slim A. Slim na kushoto ni Mkurugenzi wa Life and hope Sober House Bagamoyo, Karim Banji wakipata futari pamoja.
Katikati ni Katibu tawala wa wilaya ya Bagamoyo bi Elika Liyagela akipata futari pamoja na wananchi katika kituo cha Life and Hope Sober House Bagamoyo.

Mkurugenzi wa Life and Hope Sober House Bagamoyo, Karim Banji akitoa neno la shukrani kwa wadau walioshiriki futari


Afisa tawala wa Green Park Village, Hasim Juma,kushoto akiwa na Mkurugenzi wa Green Park Village Slim A. Slim ambao Hoteli yao ya Green Park ndiyo iliyoshughulika na mapishi ya futari.










Sunday, July 3, 2016

RAIS, DKT. JOHN MAGUFULI ATOA SALA ZA RAMBI RAMBI KWA FAMILIA YA BEATRICE SHELUKINDO.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kufuatia kifo cha Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Kilindi Mkoani Tanga Mhe. Beatrice Shelukindo kilichotokea jana tarehe 02 Julai, 2016.

Mhe. Beatrice Shelukindo ambaye amewahi kuwa Mbunge Bunge la Afrika Mashariki na baadaye kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vipindi viwili mfurulizo hadi alipostaafu mwaka jana 2015, amefariki dunia akiwa nyumbani kwao Njiro Mkoani Arusha.

Katika salamu zake Rais Magufuli amesema taifa limempoteza mtu aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo hususani alipokuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwawakilisha wananchi wa Jimbo la Kilindi na Mkoa wa Tanga.

“Mhe. Beatrice Shelukindo alikuwa kiongozi shupavu, ambaye siku zote alisimama kidete kupigania maendeleo ya wananchi na kutetea rasimali za taifa.“Kupitia kwako Mhe. Spika Job Ndugai naomba unifikishie salamu zangu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote wa marehemu na pia kwa wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” Amesema Rais Magufuli.

Dkt. John Pombe Magufuli pia amewaombea wote walioguswa na kifo cha Mhe. Beatrice Shelukindo kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki cha kuondokewa na mpendwa wao na amemuombea marehemu apumzishwe mahali pema peponi, amina.


Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam
03 Julai, 201

MPIGA PICHA WA AZAM TV OMARI MASOUD, AZIKWA LEO.

Mpiga picha wa Azam Tv, Omari Masoud, enzi za uhai wake, marehemu amefariki kwa ajali ya pikipiki eneo la makongo akiwa njiani kuelekea kazini/
Marehemu, Omari Masoud akiwekwa kwenye makazi yake ya milele, Mungu ailaze roho ya marehemu Omari mahali pema peponi, Aamiyn, Innaa lillaahi wa innaa ilayhi rajiuuun. Hakika sisi sote ni wa Mwenyezimungu na kwake yeye tutarejea.

GREEN PARK VILLAGE BAGAMOYO YAFUTURISHA.

Yalianza hivi maandalizi ya kufuturu, ndani ya viwanja vya Green Park Village, Mjini Bagamoyo
Wadau wakipata futari ndani ya viwanja vya Green Park Village Mjini Bagamoyo.
Watu mbalimbali wakiwa katika viwanja vya Green Park Village tayari kabisa kwa futari.
Mwendo wa kufuturu unaendelea katika viwanja vya Green Park Village Mjini Bagamoyo.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Green Park Village, Slim A. Slim, kulia ni Afisa tawala wa Hoteli hiyo, Hashim Juma, wakiapata futari leo jumapili tarehe 03 Juni 2016 pamoja na wadau mbalimbali.
Mkurugenzi wa Green Park Village, Slim A. Slim akitoa neno la shukrani kwa wadau wote walioshiriki nae futari.

VIONGOZI WA DINI BAGAMOYO WATAKIWA KUHESHIMIANA.



Viongozi wa dini mbalimbali wilayani Bagamoyo wametakiwa kuheshimiana kila mmoja kwa imani yake, ili kuendelea kudumisha umoja, amani na mshikamano uliopo baina ya wananchi wote.

Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid Hemed Mwanga alipokuwa akizungumza nyumbani kwake mara baada ya kumaliza kufuturu pamoja na wananchi wa wilaya yake.

Majid alisema viongozi wa dini wanayo nafasi kubwa kubwa katika jamii ya kuleta amani na utulivu, hivyo amewataka viongozi hao kuendelea kuhubiri amani miongoni mwa waumini wao ili Bagamoyo iendelee kubaki salama.

Aidha, aliwataka kutoa ushirikiano kwa serikali ya Rais, Dkt. John Magufuli ili kutekeleza azma ya Rais ya kuwaletea wananchi maendeleo pamoja na uwajibikaji.

Kwa upande wao viongozi wa dini wilaya Bagamoyo wamemshukuru mkuu huyo wa wilaya kwa kuwakaribisha katika futari ya pamoja na kumuahidi kuto aushirikiano pale watakapohitajika.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Alhaji Majid Hemed Mwanga, jana jumamosi tarehe 02 Juni 2016, aliandaa futari ya pamoja na wananchi wa Bagamoyo ili kutekeleza ukarimu unaohitajika katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadahani.

DC. BAGAMOYO AFUTURISHA JANA NYUMBANI KWAKE.

Wa kwanza kulia, mwenye koti, ni mmiliki wa Blog ya bagamoyokwanza, Athumani Shomari Mkwama, akijumuika na waislamu na wananchi wengine katika futari iliyoandaliwa na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid Hemed Mwanga.
Mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete wa pili kulia akipata futari.
wa pili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa, akijipatia futari iliyoandaliwa na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Alhaji, Majid Hemed Mwanga, nyumbani kwake.
Kutoka kushoto ni Mjumbe kutoka Zawiani Bagamoyo, Alhaji, Omari bin Yahaya bin Muhamad Raimiya, wa pili kutoka kushoto ni Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa, walipokuwa akipata futari nyumbani kwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo hapo jana jumamosi.
Waislamu mjini Bagamoyo wakipata futari nyumbani kwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo jana siku ya jumamosi tarehe 02 Juni 2016.
Kutoka kulia ni Sheikh mkuu wilaya ya Bagamoyo, Sheikh Abdulkadiri Muhamad Ramiya, wa pili ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid Hemed Mwanga, wa tatu ni Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete, anaefuata ni mjumbe wa BAKWATA wilaya ya Bagamoyo na imamu wa msikiti wa Ramia, Sheikh Simba Abubakari.