Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus
Mwangela akinawa mikono kabla ya kuingia katika Zahanati ya Saza itakayotumika
kutibu endapo atapatikana mgonjwa wa Corona wilayani hapo wakati Kamati ya
Ulinzi na Usalama ilipofanya ukaguzi wa utayari katika mapambano dhidi ya
Virusi vya Ugonjwa wa Corona kwa Wilaya ya Songwe.
Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samuel Jeremia
Opulukwa akinawa mikono kabla ya kuingia katika Zahanati ya Saza itakayotumika
kutibu endapo atapatikana mgonjwa wa Corona wilayani hapo wakati Kamati ya
Ulinzi na Usalama ilipofanya ukaguzi wa utayari katika mapambano dhidi ya
Virusi vya Ugonjwa wa Corona kwa Wilaya ya Songwe.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus
Mwangela akizungumza na bodaboda wa kituo cha Stendi ya Mkwajuni Songwe ambapo
amewaelekeza kukaa mbalimbali, kunawa kwa maji na sabuni ili kuchukua tahadhari
dhidi ya Virusi vya Ugonjwa wa Corona.
..........................................
Watu wote ambao hawachukui hatua za
tahadhari za kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya maambukizi ya Virusi vya
Ugonjwa wa Corona kwa kutofuata maelekezo ya wataalamu wa Afya, watatozwa faini
kwakuwa wana hatarisha maisha yao na ya wengine.
Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samuel
Jeremia Opulukwa amebainisha hayo jana mara baada ya Kamati ya Ulinzi na
Usalama Mkoa wa Songwe kufanya ukaguzi wa utayari wa kukabiliana na maambukizi
ya Virusi vya Ugonjwa wa Corona katika Wilaya hiyo.
Opulukwa amesema, “Sasa tunaanza
kutoza faini wote wasiofuata maelekezo ya wataalamu wa Afya kuhusiana na
Corona, mfano tukipita dukani au sehemu ya biashara na hakuna maji na sabuni,
tuta toza faini na kufunga kwa mda biashara hiyo mpaka mtu huyo azingatie
maaelekezo hayo”.
Ameongeza kuwa lengo la Wilaya hiyo
ni kuhakikisha kuwa mahali pa kufanyia biashara ni salama kwa wafanyabiashara
na watumiaji wa huduma hizo huku akieleza kuwa wanawa fuatilia wageni wote
wanao toka nje ya wilaya waliopo katika nyumba za kulala wageni na kuchukua
maelezo yao kwa ajili ya tahadhari endapo wana dalili za Ugonjwa wa
Virusi vya Corona.
Opulukwa ameongeza kuwa elimu
inaendelea kutolewa kwa wananchi wote wa Wilaya ya Songwe hususani katika
maeneo ya migodi ambapo kuna mikusanyiko ya watu wengi pia ameielekeza kamati
inayohusika kutoa elimu ifanye ufuatiliaji wa kina endapo wananchi wanazingatia
wanayo waelekeza.
Aidha amesema mara baada ya Kamati ya
Ulinzi na Usalama Mkoa kufanya ukaguzi wa utayari wa Wilaya hiyo katika
mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Virusi vya Corona, Kamati hiyo imebaini baadhi ya
mapungufu ambayo kama wilaya itasimamia kuyarekebisha.
Amefafanua kuwa yote yaliyoonekana
kama mapungufu yapo ndani ya uwezo wa Wilaya ikiwa ni pamoja na kuhakikisha
eneo la kuwatenga washukiwa wa Corona lina vitanda vya kutosha na kujenga
kichomea taka katika Zahanati ya Saza ambayo itatumika kutibu wagonjwa wa
Corona.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Songwe
Dkt Humphrey Masoke amesema wameshaagiza vifaa kinga na tiba vyote muhimu
katika Bohari kuu ya Dawa ili kuongezea katika vifaa vichache walivyo navyo
tayari.
Dkt. Masoke ameongeza kuwa wana endelea
kutoa maelekezo na elimu kwa jamii juu ya tahadhari ya ugonjwa wa Virusi
vya Corona kwakuwa bado baadhi ya wananchi wanaamini ugonjwa wa Corona ni wa
wazungu hivyo hauwahusu.
Estin Nyangito Mkazi wa Mkwajuni
Songwe amesema wamesha pewa elimu ya kuchukua tahadhari ya kujikinga na Virusi
vya Corona na elimu hiyo wataisambaza kwa wananchi wengine ili nao waweze
kuchukua tahadhari.
Kwa upande wake Jakson Mwampashi
Mkazi wa Songwe amemuomba Mkuu wa Wilaya hiyo kuweka utaratibu wa kutoa elimu
mara kwa mara na kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutumia magari ya
matangazo ya barabarani ili wananchi wote waweze kupata elimu ya Corona.
No comments:
Post a Comment