TBN. YANG'ARA KIMATAIFA, VERONICA MREMA AINGIA JOPO LA MDAHALO MKUTANO MKUU WA DUNIA WA WAANDISHI WA SAYANSI.
PRETORIA, AFRIKA KUSINI Kilele cha utambuzi wa uandishi wa habari za kidijitali nchini Tanzania kimethibitishwa baada ya Bi. Veronica Mrema, Mwanzilishi wa chombo cha habari cha M24 TANZANIA MEDIA na mwanachama mahiri wa Tanzania Bloggers Network (TBN), kuingia rasmi kwenye jopo la mdahalo katika Mkutano wa 13 wa Kimataifa wa Waandishi wa Habari za Sayansi (WCSJ2025) unaofanyika jijini Pretoria. Hili si tu fahari kwa Mrema binafsi, bali ni heshima kubwa kwa TBN na tasnia nzima ya habari nchini, ikionesha kuwa kazi ya uandishi wa kidijitali inatambulika katika majukwaa makuu duniani. Mrema yuko Afrika Kusini kuhudhuria mkutano huo mkuu unaotarajiwa kudumu hadi Desemba 5, 2025, baada ya kukabidhiwa udhamini maalum wa safari (Travel Grant) na Wizara ya Sayansi, Teknolojia, na Ubunifu ya Afrika Kusini (DSTI). Udhamini huu ulikuja kama matunda ya utambuzi wa utendaji wake wa kipekee katika uandishi wa habari za kisayansi na afya, akibainishwa kuwa miongoni mwa wachache barani Af...