Posts

TANESCO YATOA TAHADHARI KWA WANANCHI

Image
Meneja Mahusiano wa Shirika la Umeme nchini, (TANESCO), Leila Muhaji akizungumza na waandishi wa habari. ..................................... Na. Farida Saidy, Morogoro. Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limewataka wananchi wanaofanya shughuli mbalimbali za kibinadamu jirani na miundombinu ya umeme kuacha mara moja ili kujiepusha na madhara yatakayotokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwenye maeneo mbalimbali nchini. Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Kaimu Meneja Mahusiano TANESCO, Leila Muhaji amesema wale wote wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwemo kuegesha magari, kulima, kujenga makazi ya kuishi, na kufanya biashara katika miundombinu ya umeme wanatakiwa kuacha. Amewatahadharisha wananchi kutoshika au kukanyaga nyaya za umeme zilizoanguka hususan katika kipindi hiki cha mvua. “Ni vyema kutoa taarifa Tanesco kitengo cha dharura kwa msaada zaidi,”alisema. Katika hatua nyingine amesema kuwa iwapo mvua itaam...

ALIYEKUTWA UCHI YEYE NA MTOTO WAKE ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MOROGORO

Image
Kamanda wa Polisi mkoa wa morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Wilbroad Mutafungwa, akiwaonyesha wanahabari (hawapo pichani ) panga na msumeno alivyokutwa navyo, bwana Benson Benard (31) aliekutwa Uchi wa Mnyama yeye na Mtoto wake katikati ya Maporomoko ya Maji eneo la Mlimani, Nguzo Camp. ............................................ Na farida saidy morogoro Jeshi La Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia Benson Benard (31) aliyekutwa Uchi wa Mnyama yeye na Mtoto wake katikati ya Maporomoko ya Maji eneo la Mlimani Nguzo Camp ndani ya manispaa hiyo.  Mtu huyo alipoamuliwa kuondoka eneo hilo hatarishi akajirusha na kujizamisha kwenye Maji yaliyokuwa yakitiririka kwa kasi kabla ya kushikiliwa na Polisi. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Wilbroad Mutafungwa Askari wake walipokea taarifa toka kwa raia mwema juu ya uwepo wa tukio hilo na baada ya kufika eneo la tukio ambap...

OCODE YATOA ELIMU JUMUISHI KWA WALIMU NA WANAFUNZI NA WAZAZI MANISPAA YA UBUNGO

Image
Meneja wa  Uwezo Tanzania  Zaida Mgalla akizungumza na washiriki hawapo pichani wa  mdahalo wa uwajibikaji wa pamoja katika kuleta elimu bora na jumuishi  katika manispaa ya Ubungo uliowashirikisha wazazi, walimu, wanafunzi, viongozi wa dini pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali za mitaa pamoja na wadau wa maendeleo katika sekta ya elimu.  ............................................ VICTOR MASANGU, DAR ES SALAAM. KATIKA kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuboresha sekta ya elimu hapa nchini hususan kwa wanafunzi wa shule za msingi hasa kwa wale wenye mahitaji maalumu  Shirika la Organization for Community Development (OCODE) limeamua kuja na mpango wa kutoa mafunzo kwa walimu, wanafunzi na wazazi kuhusiana na umuhimu wa elimu bora na elimu  jumuishi pamoja na kujadili changamoto zilizopo ili kuzitafutia ufumbuzi. Hayo yamebainishwa na  Afisa miradi kutoka shirika  hilo la OCODE Tunu Sanga ...