Friday, November 11, 2022

MKUU WA IDARA YA UJENZI KIBAHA MJINI ACHUKULIWA HATUA ZA KINIDHAMU- NDOMBA

No description available.

No description available.

No description available.

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

BARAZA la madiwani Halmashauri ya Mji wa Kibaha ,limemchukulia hatua ya kinidhamu mkuu wa idara ya ujenzi Brighton Kishoa kwa kumkata mshahara wake asilimia 15 ndani ya miaka mitatu , kutokana na uzembe kwenye usimamizi  wa ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi na kuisababishia hasara Halmashauri hiyo.

Hatua hiyo ni fundisho kwa wakuu wa idara na watendaji wengine endapo watazembea na kushindwa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha,Mussa Ndomba alieleza maazimio hayo katika kikao cha robo mwaka baada agenda iliyojadili makosa ya kinidhamu ya mtumishi huyo ambae amekutwa na makosa ya uzembe na kushindwa kusimamia mradi huo.

Alifafanua, kamati za uchunguzi zimefanya kazi yake na kujiridhisha kuwa mkuu huyo wa idara amefanya uzembe.

“Hakuna anaependa kuchukuliana hatua kama hizi ,Ila inafikia hatua unachoka kutoa maagizo na kuelekeza kila wakati, adhabu hii anastahili  kutokana na makosa aliyopatikana nayo ikiwemo usimamizi mbovu kwenye ununuzi wa vifaa na kusababisha gharama kubwa ya manunuzi wa vifaa kwenye ujenzi huo”aliongezea Ndomba .

Ndomba alitoa wito kwa watumishi wote hadi ngazi ya mtaa kufanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu bila kupingana na miongozo iliyopo.

“Kwa kutofuata miongozo miradi ya Serikali na utoaji huduma haitoonekana wala kuleta tija:” Hivyo asitokee mtumishi yeyote kuturudisha nyuma ,sisi kama Baraza tutakuwa wakali,hatutovumilia,kuona Mtendaji anazorotesha huduma kwa Wananchi,kuanzia sasa tutakuwa wakali, tutachukua hatua kwa wale wote watakaoonyesha utovu wa nidhamu kwenye utendaji kazi wao”alisisitiza Ndomba.

Vilevile, madiwani akiwemo diwani wa Kongowe Hashim Shomari, Diwani wa kata ya Tangini Mfalme Kabuga na diwani wa Visiga Kambi Legeza walieleza, wamechoshwa na changamoto zinazoelekezwa hospital ya Mkoani .

Kufuatia malalamiko hayo ,Baraza hilo limetoa wiki moja kwa idara ya afya kushughulikia baadhi ya changamoto zinazolalamikiwa katika hospital ya Mkoani  .

Walieleza , hospital hiyo imekuwa ikitolewa malalamiko mengi hivyo idara ijitathmini ,na kujitahidi kutatua changamoto zinazoelekezwa katika hospital hiyo na baadhi ya Zahanati .

“Ifikie hatua ya kuona umuhimu wa maagizo na maelekezo mnayopewa na madiwani kila tunapokutana ,nendeni mkajitathmini na kufanya Yale ambayo yatapunguza changamoto zinazotajwa Mara kwa Mara ,”

Tunatoa siku 7 mkatatue mliyoelekezwa”jumatatu kamati ya fedha inakutana iidhinishe hata kama milioni 100 ili utekelezaji uanze”

Nae diwani wa kata ya Pichandege Karim Mtambo ,alihoji sh.milioni 800 zilizoidhinishwa kuendeleza ujenzi wa baadhi ya maeneo katika hospital ya wilaya ya Lulanzi ambayo tayarii imeshaanza kutoa huduma kwa Wananchi.

Mtambo alisema ,imepita muda mrefu ,fedha hizo zipo Lakini hakuna muendelezo wa ujenzi, swali ambalo lilimuibua mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mshamu Munde na kusema awali zikitoka milioni 500 ambazo zimeshafanyiwa kazi.

Munde alibainisha kwamba ,milioni 800 ni fedha nyingine ambazo zipo kwenye hatua ya Ununuzi na kuanzia wiki ijayo zitafanyiwa kazi kulingana na maelekezo ya fedha hizo kwenye Maeneo ambayo ujenzi unaendelea ili kukamilisha hospital hiyo.

Alisema ,kamati ilihofia kutoa fedha kutokana na tatizo la maji ,Lakini alikaa nao na kuwaambia maji Ni moja ya vifaa vinavyotumika kwenye ujenzi hivyo haiwezekani ujenzi ukasimama kutokana na malipo ya maji.

 

Monday, September 19, 2022

MUFTI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA OFISI YA BAKWATA MKOA WA SINGIDA

 No description available.

Mufti wa  Tanzania Sheikh Dk.Abubakar Zubeir (wa pili kushoto) akiongoza kuomba dua baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Baraza Kuu la Waislam  Mkoa wa Singida (BAKWATA) inayojengwa katika msikiti wa Masjid Taqwa mjini hapa katika hafla iliyofanyika Septemba 18, 2022. Kutoka kulia Katibu wa Bakwata Mkoa wa Singida, Sheikh Burhan Mlau, Sheikh wa Mkoa wa Singida Issah Nassoro na Rais wa Taasisi wa Majmaul Ahbaab, Sharif Muhamad Bin Said Al-Beidh.

..........................................

Dotto Mwaibale, na Philemon Mazalla-Singida

 

MUFTI wa  Tanzania sheikh, Dkt. Abubakar Zubeir, Septemba 18, 2022 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Baraza Kuu la Waislam (BAKWATA) Mkoa wa Singida


inayojengwa katika msikiti wa Masjid Taqwa mjini hapa.

Akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe hilo la msingi alisema amefurahishwa na kuridhishwa na hatua iliyochukuliwa ya kuanzisha ujenzi huo


kwani hayo ndiyo maendeleo yanayotakiwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)

“Mimi na msafara wangu masheikh wote waliofika katika kutekeleza mambo yetu hapa Singida tumefurahishwa sana na jambo hili na haya ndio mambo yetu ya bakwata tunayoyazungumza sana kuhusu maendeleo” alisema Mufti Zuberi.

Mufti Zuberi alisema changamoto zote zilizotolewa katika hafla hiyo alisema baraza na viongozi wapo hivyo wanaona namna ya kuzishughulikia na kuwekana sawa kwani kila jambo lina taratibu zake namna ya kuzitatua.

Aidha Mufti Zuberi alisema jambo lililokubwa ni kwa waislam mkoani hapa kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu awawezeshe kufanya mambo yao vizuri na kuondosha magomvi baina yao.

Taarifa ya ujenzi huo ikitolewa mbele ya Mufti ilieleza kuwa Mwezi Marchi 2022 Sheikh wa Mkoa wa Singida na Baraza la Masheikh waliunda kamati maalumu ili kuongeza nguvu ya ufuatiliaji wa eneo la ujenzi  na kufanikiwa kuipata ndani ya Masjid Taqwa


kwa idhini ya uongozi wa msikiti huo.

Ujenzi wa ofisi hiyo hivi sasa umefikia hatua ya linta kwa gharama ya Sh.8.2 Milioni, na kazi iliyobaki ni upauaji na umaliziaji ambapo fedha zilizokadiriwa kumalizia kazi hiyo ni Sh.14 Milioni.

Mufti akiwa njiani kwenda Singida mjini alisimama  wilayani Ikungi na kuomba dua kwenye eneo ambalo waislam wa wilaya hiyo wanatarajia kujenga Kituo


cha afya na baada ya uwekaji wa jiwe hilo la msingi la ofisi ya Bakwata alikwenda kutembelea  Taasisi ya Majmaul Ahbaab iliyopo eneo la Unyakhindi Manispaaya Singida ambapo alipata fursa ya


kuzungumza na wanawake wa kiislam na kutunukiwa Tuzo ya heshima ya Kimataifa na Rais wa Taasisi hiyo Sharif Muhamad Bin Said Al-Beidh.

No description available.

Mufti wa  Tanzania Sheikh Dk.Abubakar Zubeir akizungumza na Waislam wakati alipotembelea   Taasisi wa Majmaul Ahbaab.

No description available.

Mufti wa  Tanzania Sheikh Dk.Abubakar Zubeir akionesha Tuzo ya heshima baada ya kutunukiwa  na Rais wa Taasisi wa Majmaul Ahbaab, Sharif Muhamad Bin Said Al-Beidh (kushoto).

No description available.

Mufti wa  Tanzania Sheikh Dk.Abubakar Zubeir (kushoto) akiwa na viongoziwengine katika hafla hiyo. Kutoka kulia ni  Sheikh wa Mkoa wa Singida Issah Nassoro na Rais wa Taasisi wa Majmaul Ahbaab, Sharif Muhamad Bin Said Al-Beidh.