Thursday, August 14, 2025
MARIAN SCHOOLS MARATHON NI KESHO
Tuesday, August 12, 2025
TBN YAKEMEA 'MANABII' WA MITANDAONI, KWA UTABIRI WAO UNAOLETA TAHARUKI KWA JAMII.
Na Mwandishi wetu, Dar es salaam.
Mtandao wa Bloga Tanzania (TBN) umekemea vikali tabia inayoshamiri ya watu kujinadi kufanya utabiri kwa watu na taifa kupitia mitandao ya kijamii, ukisema vitendo hivyo vinakiuka Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.
Kauli hiyo imetolewa kama azimio katika kikao kazi cha mafunzo ya mabloga kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Mabloga hao wameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) kushirikiana kuwasaka na kuwachukulia hatua kali wale wote wanaohusika na vitendo hivyo.
Katika kikao hicho, mabloga walibainisha kuwa kumeibuka kundi la watu wanaodai kuwa ni manabii na kutoa kauli zinazokiuka sheria za nchi na kuleta taharuki kuelekea uchaguzi mkuu.
Wakitolea mfano wa kauli hizo ni kama vile kusema kutatokea kifo cha kiongozi mkubwa siku za hivi karibuni, au kutatokea machafuko fulani, na kusema kuwa kauli hizo ni za kuleta taharuki kwa wananchi na kukiuka sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi.
Walisisitiza kuwa baada ya kuchambua Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (Personal Data Protection Act), walibaini kwamba 'utabiri' wa namna hiyo unavuruga haki ya msingi ya faragha ya wahusika.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkuu wa Mawasiliani Serikalini, Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, (PDPC) Innocent Mungy, amesema sheria inakataza kutoa Taarifa za mtu binafsi bila ya ridhaa yake.
Aliongeza kwa kusema kuwa, katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wapo watu watatoa taarifa za Afya ya mtu kwa lengo la kumharibia ili asichaguliwe jambo ambalo ni kosa kisheria.
Mungy alisisitiza kuwa sheria hiyo ina adhabu kali na lazima ifuatwe na kila mtu, si tu mabloga na waandishi wa habari.
Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na TCRA, yalilenga kuwaandaa mabloga kuripoti habari za uchaguzi kwa weledi na uadilifu.
Pamoja na mada ya ulinzi wa taarifa binafsi, mada nyingine muhimu zilizotolewa ni pamoja na Mwongozo wa Waandishi wa Habari katika Uchaguzi na Matumizi ya Akili Mnemba (AI) katika uandishi wa habari.
Lengo kuu la mafunzo haya ni kuongeza uwezo wa mabloga kuhakikisha wanafuata sheria na maadili ya uandishi, jambo linalotazamiwa kuchangia mazingira ya uchaguzi yenye amani na utulivu.
Meneja wa Huduma za Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Andrew Kisaka, akiwasilisha mada katika mafunzo maalumu kuelekea uchaguzi mkuu mahususi kwa bloga yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Agosti 11, 2025 Jijini Dar es Salaam
Monday, August 4, 2025
TCRA YAWAFUNDA BLOGA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025
Na Mwandishi Wetu
Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni, wameaswa kutotoa taarifa ambazo zitaleta taharuki na machafuko ndani ya nchi hasa katika kuelekea kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakao fanyika baadaye mwaka huu (2025).
Yamesemwa hayo jana tarehe 3, Agosti 2025 na Meneja Kitengo cha Huduma za Utangazaji,TCRA, Injinia Andrew Kisaka wakati akiwasilisha makala (mada) katika mkutano ulioandaliwa na wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini (INEC) kwa watoa maudhui mtandaoni, amesema kuwa wakati wa uchaguzi kuna mazingira ya migawanyiko, mivutano ya kijamii, na upotoshaji wa hali ya juu hivyo ni muhimu Mabloga waepuke kuepuka kusambaza uvumi, kuripoti kwa umakini, kutopendelea upande wowote na kukemea lugha za chuki.
Kisaka amewataka bloga nchini kote kuimarisha maadili yao na kuchukua jukumu muhimu katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani kwa kupandisha maudhui yenye tija na kama unaona maudhui yataleta taharuki ni bora kuachana nayo.
Aidha Kisaka ametoa mfano wa Historia ya machafuko ya uchaguzi yaliyotea katika nchi Kenya Nigeria (2007) na Kenya (2011), amesema kuwa, katika machafuko hayo zaidi ya watu 800 walipoteza uhai nchini Nigeria mwaka 2011 wakati nchini Kenya zaidi ya watu 1,000 walipoteza uhai na wengine 600,000 kupoteza makazi.
Aidha amesema kuwa katika mazingira magumu yenye shinikizo la juu la uchaguzi, vyombo vya habari vinaweza kujikuta vikichangia machafuko kwa kueneza uvumi au kuchochea upendeleo wa kisiasa.
Amesema ili kukabiliana na maafa wakati wa uchaguzi na baada kuna miongozo ya kuripoti ambayo inatatua changamoto hizo.
"Uvumi ndiyo chanzo kikuu cha vurugu hivyo Vyombo vya habari vinapaswa kuchunguza kwa kina uvumi na kutoa taarifa sahihi haraka iwezekanavyo ili kuzuia mzunguko wa vurugu za kulipiza kisasi." amesema Mhandisi Kisaka.
Pia amehimiza Mabloga kukataa lugha na vichwa vya Habari vya Kichochezi.
"Msiripoti kila kauli ya uchochezi kutoka kwa wanasiasa ,hata kama kauli hizo zinaonekana kuwa habari kwenu na zenye kuvutia msomaji acha kabisa ni muhimu kutokuzirudia kwenye vichwa vya habari, " amesema Mhandisi Kisaka na kuongeza kuwa lugha inayodhalilisha inaweza kuchochea wananchi kutenda vitendo vya kikatili.
Aidha amesema kuwa katika kipindi hiki cha uchaguzi, ni vyema Bloga kuchukua tahadhari binafsi kutoa matangazo ya moja kwa moja 'live' ya mikutano ya kampeni za wagombea kwa sababu yanaweza leta machafuko.
Aidha amesema kuwa vyombo vya habari vinapaswa kuzuia kuonesha picha zinazochochea vurugu na ikiwa ni lazima, kusimamisha matangazo ya moja kwa moja ili kuzuia hali kuwa mbaya zaidi.
WAZALISHAJI WA MAUDHUI MTANDAONI WAHIMIZWA KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU 2025
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutanio wa Tume na Wazalishaji Maudhui Mtandaoni kuhusu uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kikao hicho cha siku moja kilifanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 03 , 2025.
Baadhi ya wawakilishi wa serikali waliohudhuria mkutano huo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg.Kailima Ramadhani akitoa mada wakati wa ufunguzim wa mkutanio wa Tume na Wazalishaji Maudhui Mtandaoni kuhusu uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kikao hicho cha siku moja kilifanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 03 , 2025.
Picha ya pamoja ya washiriki
NA WAANDISHI WETU, DAR ES SALAAM.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele, amewahimiza wazalishaji wa maudhui mtandaoni kutumia majukwaa yao ya kidijitali kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Akizungumza leo tarehe 03 Agosti, 2025, jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kitaifa kati ya Tume na Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni, Mhe. Mwambegele amewapongeza wazalishaji hao kwa ushirikiano walioutoa kwa Tume katika hatua mbalimbali za maandalizi ya uchaguzi.
Mhe. Mwambegele amewasihi wazalishaji hao wa maudhui kuendelea kuwa daraja muhimu kati ya Tume na wananchi kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati.
“Tuna imani kuwa tutazidi kushirikiana nanyi kwa karibu zaidi, na mtatumia nafasi zenu kuwapatia wananchi taarifa sahihi kuhusu maendeleo ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2025 na kuwahamasisha kushiriki kikamilifu kwa kupiga kura,” amesema Mhe. Mwambegele.
Amebainisha kuwa Tume inatambua mchango wa wazalishaji wa maudhui mtandaoni katika njia mbili kuu. Kwanza, kama daraja la mawasiliano kati ya Tume na wadau, na pili, kama wadau wa moja kwa moja wa mchakato wa uchaguzi.
“Tume inathamini kazi yenu ya kuandaa, kuchapisha na kusambaza taarifa kupitia majukwaa mbalimbali ya kidijitali kama mitandao ya kijamii, blogu, tovuti na majukwaa ya video kama YouTube,” ameongeza.
Akizungumzia nafasi ya vijana katika uchaguzi, Mhe. Mwambegele amesisitiza umuhimu wa mawasiliano ya kidijitali kwa kundi hilo, akiwahimiza wazalishaji hao wa maudhui kutumia ubunifu wao kwa kutumia michoro, video na ujumbe wenye mvuto ili kuwafikia wapiga kura kwa njia rahisi na ya kuvutia.
Amesema lengo kuu la mkutano huo ni kujadili hatua zilizofikiwa katika maandalizi ya uchaguzi, kubadilishana mawazo, na kusikiliza changamoto zinazowakabili wazalishaji wa maudhui mtandaoni ili kutafuta suluhisho kwa wakati.
“Mkutano huu si wa upande mmoja; ni jukwaa la mawasiliano ya pande mbili ambalo linawapa fursa ya kueleza changamoto zenu na kusaidia kuboresha utekelezaji wa shughuli za uchaguzi,” ameeleza Mhe. Mwambegele.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani, amehimiza waandaaji wa maudhui mtandaoni kutumia majukwaa yao kutoa habari sahihi, na zilizothibitishwa na kufanyiwa utafiti.
Ameongeza kuwa majukwaa hayo ya kidijitali yanasaidia kurahisisha upokeaji wa taarifa za Tume na kuwafikia wananchi kwa haraka.
Aidha, Bw. Kailima amewahimiza wazalishaji wa maudhui mtandaoni kutoa taarifa za mara kwa mara kuhusu mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa 2025, ikiwa ni pamoja na kuitumia kauli mbiu ya uchaguzi “Kura Yako Haki Yako, Jitokeze Kupiga Kura” ili kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi tarehe 29 Oktoba, 2025.
Mkutano kati ya Tume na Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni ni mfululizo wa mikutano ya Tume na wadau wa uchaguzi ambayo ilianza tarehe 27 Julai, 2025. Mikutano hiyo inatarajiwa kuhitimishwa tarehe 04 Agosti, 2025 kwa wahariri na waandishi wa vyombo vya habari kupatiwa mafunzo.
Picha mbalimbali za washiriki wa Mkutano huo.
Tuesday, July 8, 2025
DIRA 2050 INA KINGA YA BUNGE -PROF MKUMBO
Na Mwandishi wetu
SERIKALI imewatoa hofu Watanzania kuhusu hoja ya kuwa utekelezaji Dira 2050 unaweza kukumbwa na changamoto ya uhalali wa kisheria na hivyo mpango huo muhimu kwa taifa ukawa na ombwe la kiufanisi hapo baadae
Akiongea katika kikao maalum na Wahariri kutoka jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Waziri wa nchi ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaii Profesa Kitila Mkumbo amesema Dira ya taifa 2050 imewekewa ulinzi kwa kupelekwa bungeni na kwamba hakuna Rais atakayeweza kwenda kinyume na uamuzi huo
Profesa Mkumbo amesema Dira 2050 itatekelezwa na Marais watatu,na kwa atakaetaka kuibadilisha atatakiwa kupeleka bungeni na kwamba Dira hii imekuwa tofauti kwa kuwa ya 2025 iliishia hatua ya kuidhinishwa na Baraza la Mawaziri tu.
Waziri huyo amesema mchakato wa kutengeneza Dira 2050 umepitia hatua 13 ambazo ni kuandaa na kuidhinisha miongozo ya Dira.
Mkakati wa kuandika Dira ulianza Aprili mwaka 2023, kwa kuunda vyombo vya kutathimini mchakato wa Dira na kufanya tathimini ya utekelezaji wa Dira 2025.
Pia kukusanya maoni ya wananchi na wadau juu ya maudhui gani yaingie kwenye Dira, kujifunza kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Asia na Marekani kwa hatua zilizopigwa.
Alizitaja baadhi ya nchi walizojifunza ni Botswana, Moroco, Mauritius, Afrika Kusini na Kenya.
Kwa Asia wamejifunza Kusini mwa Asia za China, Indonesia, Korea Kusini, Singapore na India, na kwamba kwa Ulaya wamejifunza kidogo kutokana na kwamba historia yao si ya muda mrefu kama nchi zenye historia 1,000.
Hatua nyingine ni uchambuzi, uandishi na uhariri wa taarifa na kutoa Rasimu ya kwanza ya Dira 2050.
Pia kulinda rasmu ya kwanza ya Dira 2050 iliyozinduliwa Desemba 2024,na kuchukua Rasimu kupeleka tena kwa wadau ili kupata maoni ya kihariri.
"Tulikutana na wadau mbalimbali kama waandishi wa habari na vyama vya siasa ili kupata makubaliano ya pamoja.
Tulivyokutana na vyama vya siasa tulikubaliana tusibishane juu ya tunakwenda wapi ila tukubaliane tuende huku, Ilani zetu ziakisi tunaenda wapi, "amesema.
Hatua nyingine, ni kutoa rasimu ya pili ya Dira ya Taifa na kukabidhiwa kwa Waziri Mkuu, Juni 2025 iliidhinishwa na Baraza la Mawaziri na kufuatiwa na Bunge.
Aidha, amesema hatua ya mwisho ni kuutaarifu umma kuwa mchakato wa Dira umekamilika na itajulikana kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza Dira 2050 Tanzania Tuitakayo, na hatua ya mwisho ni Rais Samia Suluhu Hassan kuizindua Julai 17, mwaka huu.
Friday, June 13, 2025
ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUPIGWA NA WAFUGAJI.
Na Omary Mngindo,u
ELIAS Madinga mkazi wa Kitongoji cha Mlelani, Kijiji cha Visezi Kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, amenusurika kifo baada ya kushambuliwa na Wafugaji.
Mkazi huyo akiwa na mkewe katika nyumba ya bosi wake Kitongojini hapo, siku ya tukio akipulizia dawa mazao aliona makundi ya ng'ombe yaliyogawanyika mara tatu yakiingia ndani ya shamba hilo.
Alisema kuwa alipoona hivyo alianza kuiswaga ili itoke shambani, wakati huo akiwepo kijana mdogo jamii ya Wafugaji na kwamba wakati akiendelea na zoezi ilo ghafla yule kijana alitoweka.
"Kwakuwa nilikuwa na zoezi la kupulizia dawa, nikachukua baskeli nikaenda kisimani kuchota maji, wakati narudi nikamuona mke wangu amembeba mtoto wetu wa miezi mitatu wamemzingirwa na Wafugaji hao", alisema Madinga.
Aliongeza kuwa"Nikiwa nakaribia aliniambia nisifike kwani ameshashambuliwa na Wafugaji hao, sikumuelewa wakati nikaribia nikajikuta mimezingrwa na kundi la Wafugaji wakaanza kunishambuliwa kwa silaha mbalimbali za jadi," alisema.
Alieleza kuwa wakati wanamshambulia mke wake aliwaomba wamwachie akamvalishe mtoto nguo, akatumia nafasi hiyo kukimbilia kijijini kutoa taarifa kwa Mwenyekiti, ambapo alifika Askari Mgambo akamchukua wakamkimbiza Zahanati.
"Nilipoteza fahamu niliposhtuka nikajikuta niko Zahanati natibiwa, nilipochukuliwa pale nyumbani sikujitambua, pamoja na kwamba nilikimbilia ndani lakini waliingia wakaendeleza mashambulizi," aliongeza Mhanga huyo.
Aliongeza kwamba "Baada ya kupelekwa kesi Polisi Chalinze walimfuata wakataka kumpatia kiasi cha shilingi laki tatu nikakataa, nafuatilia ili suala ili niende Mahakamani," alimalizia mkazi hiyo.
Swala la wafugaji kudharau mashamba ya wakulima wilayani Bagamoyo limekuwa ni jambo la kawaida hali inayotishia usalama wa wakulima.
Wananchi walioongoe na BAGAMOYO KWANZA BLOG wameiomba Serikali kuchukua hatua dhidi ya wafugaji ili kukomesha vitenda vya dharau na unyanyasaji wanavyofanyiwa wakulima.
Thursday, June 5, 2025
Thursday, March 20, 2025
TCRA KUSHIRIKIANA NA TBN KUSADIA KUZALISHA MAUDHUI YENYE TIJA
Monday, March 17, 2025
MFUMO WA USAJILI WAANDISHI WA HABARI KIDIJITALI UPO MBIONI KUKAMILIKA- MSIGWA
Monday, February 24, 2025
WAZIRI KIKWETE KUFANYA ZIARA YA SIKU TATU MKOANI SONGWE.
Anatarajiwa kukagua na Kuzindua Miradi ya Maendeleo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu -Mhe. Ridhiwani Kikwete Februari 23, 2025 amewasili mkoani Songwe kwa lengo la ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo ikiwemo ya sekta ya Elimu, Afya na Miundombinu kwa ajili ya ustawi wa maendeleo ya wananchi .
Mhe. Waziri Kikwete anatarajiwa kukagua na kuweka Mawe ya msingi katika miradi hiyo ambayo inakadiriwa kugharimu zaidi ya shilingi Bilioni 700 katika Halmashauri zote za mkoa huo.
Mara baada ya kuwasili katika mkoa huo , Waziri Kikwete alipokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Ndg. Daniel Chongolo ambaye alimpa hali ya maendeleo ya Mkoa huo na maandalizi ambayo yameshafikiwa kwa ajili ya ziara hiyo.
Vile vile Mhe. Kikwete anatarajiwa pia kukagua Maendeleo ya Kituo cha Vijana cha Sasanda wilayani Songwe ambapo atakagua mradi wa Shamba la vijana lililopo kituo hicho.
Mhe Waziri Kikwete ameambatana na watendaji mbalimbali ambapo amemhakikishia Mkuu wa mkoa huo kuwa timu yake ipo tayari kwa ajili ya kazi iliyowaleta.

























.jpeg)





















