Tuesday, July 23, 2024

CTI WADAU WA VIWANDA WATETA KUHUSU DIRA YA TAIFA 2050.

 


Na Mwandishi Wetu


SHIRIKISHO la Wenye Viwanda (CTI), limependekeza maendeleo ya viwanda yapewe kipaumbele kwenye Dira ya Taifa ya 2050.


 


Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa CTI, Leodegar Tenga wakati wa mjadala wa wadau wa viwanda wakijadili Dira ya 2050 na kuzungumzia maendeleo ya viwanda kwa ujumla.


 


Mkutano huo ulioandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI), pia ulizindua tuzo za Rais za Mzalishaji Bora Viwandani PMAYA ambazo hufanyika kila mwaka kwa wenye viwanda.


 


Tenga alisema hakuna  nchi duniani hata moja ambayo iliwahi kupiga hatua kubwa kiuchumi bila kuwekeza kwenye viwanda kwa hiyo lazima kuwe na mikakati madhubutu ya kukuza viwanda.


 


“Kuna msemo wa Kiswahili kwamba kupanga ni kuchagua kwa hiyo tuchague kuwekeza kwenye viwanda ili tusonge mbele na ili viwanda vifanye kazi vizuri lazima tuwe na watalamu wetu kwa hiyo tena lazima tuwekeze kwenye elimu bora,” alisema Tenga


 


Alisema ili viwanda viweze kufanya kazi vizuri, lazima serikali iwekeze pia kwenye ujenzi wa miundombinu ya barabara na reli na kuwekeza kwenye rasilimali watu.


 


“Maono ya nchi ni kujipanga ili tutimize tulichopanga kwa hiyo sisi CTI tunaamini viwanda ni muhimu na ili kupata rasilimali lazima tuwe na kilimo kwa hiyo lazima tuwekeze pia kwenye kilimo,” alisema


 


“Tumefungua masoko mengi upande wa Afrika Mashariki (EAC),  kusini mwa jangwa la sahara (SADC) sasa tujipange kuuza bidhaa zetu za viwandda nje ya nchi badala ya sisi kuwa soko la bidhaa za wenzetu,” alisema Tenga


 


 Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Prof Kitila Mkumbo alisema katika maandalizi ya Dira ya Taifa  2050 imeweka kipaumbele kikubwa kwenye maendeleo ya ya viwanda nia ikiwa ni  kuondoa utegemezi wa kununua bidhaa nyingi nje ya nchi.


 


Profesa Mkumbo alisema wasomi mbalimbali wamesema kwenye maandiko yao kuwa tofauti kubwa baina ya nchi tajiri na zile maskini ni kwamba nchi tajiri zina viwanda vingi wakati nchi maskini hazina viwanda na zinategemea kununua bidhaa nje ya nchi.


 


“Itakuwa vigumu sana kutengeneza Dira ya Taifa bila kuweka viwanda katikati ya dira hiyo kwasababu hilo ni la msingi na tafiti nyingi zinaonyesha kuwa hatuwezi kuendelea kwa kuendelea kununua bidhaa nje ya nchi, lazima tuwe na viwanda vingi tuuje  nje,” alisema


 


Alisema katika utafiti ambao umefanywa na serikali katika maandalizi ya dira hiyo uliohusisha watu 7,668 nchi nzima waliochaguliwa kisayansi walitaka vipaumbele vitano viwepo kwenye dira hiyo.


 


Alitaja moja ya kipaumbele kilichotajwa na wananchi hao kuwa ni suala la viwanda na kwamba asilimia 65 ya malighafi zinazotumika viwandani zinatokana na kilimo  hivyo kilimo nacho kitaendelea kuwa kipaumbele kwenye dira hiyo.


 


Alisema kipaumbele kingine kilichotajwa kwenye utafiti huo ni uwekezaji mkubwa kwenye rasilimali watu kwani uchumi wa viwanda unahitaji watu waliosoma vizuri.


 


“Lazima dira yetu ituelekeze kuwekeza kwenye elimu na siyo elimu tu bali elimu iliyobora,” alisema Profesa Mkumbo.


 


Monday, July 22, 2024

RAIS DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI NA KUHAMISHA NA KUTENGUA BAADHI YA VIONGOZI.

 





DC OKASH AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM BAGAMOYO.

 

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Halima Okash tarehe 20 Julai, 2024 amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM mbele ya Halmashauri Kuu  ya CCM Wilaya ya Bagamoyo kuanzia Januari hadi Juni 2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze.


 Akiwasilisha taarifa hiyo mkuu huyo wa wulaya, alisema kuwa, kwa ujumla Halmashauri zote mbili  zimeendelea kufanya vizuri katika nyanja zote hasa upande wa ukusanyaji wa mapato, miundombinu ya Elimu na Afya.


 "Waheshimiwa wajumbe kwa upande wa ukusanyaji mapato mfano Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo kwa Mwaka wa fedha 2023/24 ilipanga kukusanya bilion 5.8 lakini kwa ujumla imefanikiwa kukusanya Sh bilioni 6.3 sawa na aslimia 106 haya ni mafanikio  makubwa.Alisema Mhe. Okash.


 Hata hivyo,Mhe Okash alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa wa Tanzania Dkt. Samia  Suluhu Hassan kuwapatia Fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo pamoja na uboreshaji wa huduma za afya, maji na umeme.


 Halmashaurji Kuu ya CCM Wilaya ya Bagamoyo iliridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha kuanzia January hadi June 2024.











Thursday, July 18, 2024

GLOBAL EDUCATION LINK YADAHILI WANAFUNZI MAONYESHO YA VYUO VIKUU ZANZIBAR.

 






Na Mwandishi Wetu


WAKALA wa Elimu ya Vyuo Vikuu nje ya Nchi Global Education Link (GEL), imeanza kudahili wanafunzi papo hapo kwenye maonyesho yanayoendelea kwenye viwanja vya Maisala visiwani Zanzibar.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa GEL, Abdulimalick Mollel, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonyesho hayo yanayoendelea visiwani humo.


Alisema kwenye maonyesho hayo kuna vyuo vya nje ya nchi ambavyo vimetoa udhamini wa asilimia 50 kwa wanafunzi wanaotaka kwenda kusoma kwenye vyuo hivyo na vingine vimetoa ufadhili wa asilimia 100.


“Tumeleta wawakilishi wa vyuo 20 kutoka Irani kuna ufadhili wa asilimia 100 analipiwa kila kitu na kuna vyuo ambavyo mwanafunzi atalipiwa asilimia 50 ya ada kwa hiyo mwanafunzi akija kwenye maonyesho haya akichagua kozi GEL tunamdahili hapahapa,” alisema


Alisema lingine la manufaa kwenye maonyesho hayo ni uhusiano wa vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi kwani uzoefu unaonyesha kuwa asilimia kubwa ya wahitimu wa vyuo vya nje ya nchi wanaajiriwa mara tu wanapomaliza vyuo.


Alisema mara nyingi wanafunzi wanaohitimu vyuo vya hapa nchini huanza kuhangaika kutafuta ajira kwenye maeneo mbalimbali na kulalamikia ugumu wa ajira wakati vyuo vya nje hali ni tofauti kwa wahitimu wao.


“Vyuo vya nje vinafanikiwa kutoa wahitimu ambao wanaajiriwa mara tu wanapohitimu ndiyo maana tumewakutanisha na vyuo vya ndani ili waweze kubadilishana maarifa, wao wanafanyaje kuwaaandaa wanafunzi tunaangalia je ni suala la mitaala au ushirikiano mwema na taasisi za ajira,” alisema


“Kwa hiyo tulicholeta hapa ni ushirikiano baina ya vyuo hivi kama kuna chuo kikuu cha hapa ndani kilichoko tayari kushirikiana na chuo chochote cha nje watakutana na kubadilishana ujuzi na maarifa mbalimbali ili waweze kutoa wahitimu bora,” alisema


Alisema lingine ni fursa ya kupata udahili kwani baadhi yao wamekuwa wakikosa nafasi za kujiunga na vyuo vikuu kutokana na ufinyu wa nafasi kwenye baadhi ya kozi wanazoomba hasa zile za afya na uhandisi.


Mollel alisema idadi ya wanafunzi wanaoomba nafasi za kozi za afya na uhandisi ni wengi kuliko nafasi zilizopo hivyo kuna umuhimu wa kuwatafutia nafasi kwenye vyuo mbalimbali nje ya nchi.


“Tumekuja na vyuo hapa ambavyo vinaruhusu wanafunzi kudahiliwa hapa nchini akasoma kwenye chuo cha nje kwa miaka kadhaa kisha akarudi kumalizia elimu yake hapa Tanzania kwa hiyo sisi tunaona hii ni fursa kwa vijana wetu,” alisema.


Aidha, alitoa wito kwa wanafunzi wa Zanzibar na wadau wa elimu kuwa dunia imekuwa kama kijiji hivyo wanatakiwa kutumia fursa za nje kwani hata gharama za masomo kwenye vyuo vya nje zinalingana na za masomo ya hapa nchini.


“Watanzania wachangamkie fursa za ufadhili wa vyuo vikuu wasidharau kwasababu tuna mtindo wa wa kudharau kwasababu ya kuogopa kujaza fomu zenye maelezo mengi lakini sisi tuna ofisi hapa Zanzibar waje tutawatafsiria maelezo hayo,”


“Unaweza kukuta fomu moja ya scholarship inakaratasi hadi 13 sasa kwa mwanafunzi ni mara yake ya kwanza kuomba ufadhili anakata tama lakini kwa kuwa tuko hapa waje tuwaelekeze na tuko hapa kufungua fursa zilizoko duniani ili wanafunzi waweze kusoma nje,” alisema


Aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Dk. Hussein Mwinyi kwa kuonyesha utayari wa kushirikiana na Global Education Link kuendelea kuwatafutia fursa za elimu ya juu nje ya nchi.


Tuesday, July 16, 2024

MABASI 100 MWENDOKASI YANAKUJA

 

Na Mwandishi wetu 



SERIKALI iko mbioni kuleta mabasi 100 ya mwendokasi nia ikiwa ni kuongeza nguvu kwenye eneo la huduma ya usafiri kwa Jiji la Dar es Salaam 


Msajili wa Hazina Nehemiah Kyando Mchechu amesema hayo jana kwenye kikao maalum na Wahariri kuwa mabasi 100 yatanunuliwa kwa fedha za mkopo kutoka Benki ya NMB.

 


Mchechu amesema kwa kipindi cha miezi miwili amekuwa akifanya vikao na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART), Kampuni ya Mabasi Yendayo Haraka (UDART), Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) na sasa wamefikia ukingoni.


"Nimekuwa na vikao nao vya mara kwa mara na wadau hawa ili kuokoa hii hali  maana tumeona inaenda kuleta crisis (maafa) na kuathiri taswira nzuri ya Serikali kwenye mradi huu” amesema Mchechu.


Kwa mujibu wa Mchechu mabasi hayo yatakuwa yamewasili nchini ndani ya miezi sita ijayo ili kusaidia kutatua changamoto ya usafiri wa mabasi yaendayo kasi kwa mkoa wa Dar es Salaam.


Kauli ya Mchechu imekuja wakati kukiwa na malalamiko kwa wadau na wananchi juu ya ubora wa mabasi hayo kutokana na mrundikano wa watumiaji pamoja na uchache wa usafiri huo kulinganisha na mahitaji yaliyopo.


Mbali na changamoto hizo baadhi ya mabasi hayo pia ni machakavu na pia yapo katika mfumo wa kizamani kwa  kutokidhi mahitaji ya watumiaji ikiwemo wenye ulemavu na wazee.


Pia msajili wa hazina amesema ni muhimu sana kwa mji kama Dar es Salaam kuwa na kampuni za usafiri zaidi ya moja zitakazosaidiana kutoa huduma hiyo kwa wananchi.


Mwaka jana Oktoba 24, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed  Mchengerwa aliuelekeza uongozi wa Dart kuongeza watoa huduma ili kuboresha huduma ya usafiri huo.


Aidha, Mchechu ameitaka Dart ifikapo Agosti mwaka huu kuhakikisha wametengeneza mifumo ya ukusanyaji fedha ili kudhibiti mapato na kupunguza wizi. 


“Kuna wizi mwingi unafanyika kwenye cash, mimi huwa nasema ni ‘headache’ kusimamia huu mradi kwenye suala la malipo. Tumekubaliana na Dart kuwa hadi Agosti 2024 wawe wamekamilisha mfumo wa nauli kwa njia ya mtandao.” amesema Mchechu


WAZIRI MKUU AZINDUA MITAMBO YA KISASA YA KURUSHIA MATANGAZO.

 





Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Julai 15, 2024 amekagua na kuzindua mitambo na vifaa vipya vya kurushia matangazo vya kampuni ya Azam Media Limited.


Vifaa hivyo ni pamoja na Magari ya kisasa ya kurushia matangazo (OB Van), kamera za kisasa pamoja na mfumo wa kusaidia maamuzi viwanjani (VAR).


Vifaa hivyo vilivyogharimu shilingi bilioni tano vitatumika katika kurushia matangazo ya mpira wa miguu wa ligi Kuu Tanzania bara na Zanzibar pamoja na michezo mingine.


Akizungumza na wafanyakazi wa Azam Media pamoja na wadau wa michezo Mheshimiwa majaliwa amesema manunuzi ya vifaa hivyo ni mapinduzi makubwa katika tasnia ya habari kwani kunaifanya Tanzania kuwa nchi ya kipekee kuwa na vifaa vya kisasa vya aina yake katika ukanda wa Afrika Mashariki.


Mheshimiwa Majaliwa pia ameshuhudia uzinduzi wa chaneli mpya ya Azam 4 HD ambayo itatumika kurusha ligi kuu ya Ufaransa (Legue 1) na ligi kuu ya Ujerumani (Bundesliga)

MCHINJITA AWAVUNA VIGOGO CHADEMA LINDI KUHAMIA ACT

 




NA HADIJA OMARY 



JUMLA ya wanachama 45 wa chama cha Demockasia na Maendeleo CHADEMA na viongozi wao Mkoani Lindi wamekihama chama chao na kujiunga na chama cha ACT wazalendo



Wanachama hao wamejiunga na chama cha Act kwa kurejesha Kadi zao za uanachama  na kupewa Kadi mpya za ACT, zoezi lililoongozwa na makamu Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo bara Bwana Isihaka Mchinjita 



Viongozi waliojiunga ACT ni pamoja na  aliekuwa Mwenyekiti Mkoa wa Lindi, Zainab Lipalapi; Mwenyekiti BAVICHA Mkoa wa Lindi, Said Mzee; Katibu wa Jimbo, Musa Rwegoshora; Mwenyekiti wa Wazee Jimbo, Bakari Likaku; Mweka Hazina wa Jimbo, Mohamed Mandoyo; na Mwenyekiti BAVICHA Jimbo, Doa Omari.



Akizungumza mara baada ya kuwakabidhi Kadi zao mpya za ACT wazalendo  Mchinjita amewapongeza wanachama kwa uamuzi wao wa kujiunga  na chama hicho  na kwamba wamechagua  jukwaa sahihi


Nae  Bwana Mussa Rwegoshora  ambae alikuwa katibu wa chama cha Demockasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya ya Lindi amesema,  wameamua kujiunga na ACT kwa ajili ya kuunganisha nguvu ya pamoja ili kutetea maslah na Maendeleo ya Wana Lindi hivyo ni wajibu wao kuwa na jukwaa la pamoja la upinzani



" Sisi wote tumeamua kujiunga na ACT kwa ajili ya ukombozi wa Jimbo la Lindi na wala haya hayakuja kwa ghafla  ni mpango wa mwenyezimungu, wakati tunaendelea kudhoofika na madalali wa siasa mungu akasema hili haliwezekani ngoja wenya haki wakae huku na wenye dhulma waendelee kudhulumu wenzao"


TFCG YAWEZESHA UPATIKANAJI WA HATI MILIKI ZA KIMILA 738 HALIMASHARI YA MTAMA 

 



Na Hadija Omary 


Katika kuiwezesha jamii kwenye usimamizi shirikishi wa misitu ya asili na kuondoa migogoro ya umiliki wa Aridhi shirika la kuhifadhi misitu Tanzania (TFCG) limewezesha upatikanaji wa hati miliki za kimila 738 kwa  wananchi wa vijiji 10 vya halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi 





Kijiji cha mihima ni miongoni mwa vijiji 10 vya halmashauri ya Mtama vilivyopo kwenye mradi wa  kuongeza usimamizi shirikishi wa misitu chini ya  shirika la kuhifadhi misitu Tanzania (TFCG)  baadhi ya wananchi walinufaika na hati miliki za kimila wanaeleza  faida na manufaa ya hati hizo




Yahaya mtonda ni meneja mradi wa kuongeza usimamizi shirikishi wa misitu kutoka TFCG amesema malengo ya utoaji wa hati hizo  ni kuiwezesha  jamii  kuzingatia misitu ya hifadhi ya vijiji kutoingiliwa na matumizi mengine





Victor shao ni mkuu wa kitengo cha maliasili na  uhifadhi wa mazingira halmashauri ya Mtama amesema tangu mwaka 2020 tfcg ilipoanzisha mradi wa kuongeza usimamizi shirikishi wa misitu katika halmashauri hiyo  vijiji hivyo vimeweza  kuanzisha sheria ndogo ndogo ili kuhakikisha wananchi hawavamii misitu hiyo