Tuesday, April 23, 2024
Monday, April 22, 2024
DKT. ROSE RWAKATARE ATOA MSAADA WAATHIRIKA MAFURIKO MLIMBA.
MWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk. Rose Rwakatare akikabidhi msaada wa mchele kwa waathirika wa mafuriko jimbo la Mlimba mkoani Morogoro.
..................................
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
MWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk. Rose Rwakatare ametoa msaada wa tani tano za mchele kwa waathirika wa mafuriko wa jimbo la Mlimba mkoani humo.
Alikabidhi msaada huo leo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Dunstan Kyoba katika hafla ambayo imefanyika ofisini kwake mkoani Morogoro.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Dk. Rose amesema amezaliwa Mlimba hivyo ameguswa sana kuona wananchi wenzake wanaishi maisha ya shida.
“Mimi ni mzaliwa wa Mlimba, kwa hiyo hapa ni nyumbani kwangu ndiyo maana nimeamua kuja kulia na wanaolia, tufarijiane wakati huu mgumu, sijaja bure nimekuja na mifuko 1,000 ya mchele angalau wapate chakula,” alisema.
Amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuma ujumbe kupeleka msaada wa vitu mbalimbali na kuwaomba wadau mbalimbaali waendelee kupeleka msaada.
“Hata ukiwa na mfuko mmoja wa mchele, unga unakaaribishwa kuja kusaidia watanzania wenzako, sisi ni watanzania na tunajulikana dunia nzima kwa upendo,” amesema.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Dunstan Kyoba amemshukuru Dk. Rose Rwakare kwa upendo aliouonyesha kwa wakazi wa Mlimba na kuwaomba wadau wengine kuiga mfano huo na kwenda kusaidia.
Amesema msaada huo umekuja wakati mwafaka kwani wananchi wa maeneo yaliyoathirika na mafuriko wanahitaji faraja na kushikwa mkono wakati huu.
“Napenda kutoa wito kwa viongozi wengine na wafanyabiashara waige mfano wa Dk. Rwakatare waje kusaidia wananchi ambao wako kwenye wakati mgumu wakati huu,” amesema.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilombero Mohamed Msuya, amempongeza Dk Rose kwa msaada alioutoa kwa wananchi hao.
Alisema msaada huo ni wa kuigwa na wa mfano kwa wananchi wa wilaya yaa Kilombero bila kujali itikadi za kisiasa..
“Tumpongeze sana Dk. Rose kwa kuwa na maono ya kuwasaidia wananchi wa Kilombero, kutoa ni moyo wala skiyo utajiri kwasababu kuna watu wana vingi lakini hawana moyo wa kutoa,” amesema.
“Nawaomba sana watanzania wote bila kujali itikadi kujitokeza kuwasaidia wananchi wa Jimbo la Mlimba waliopata shida ya mafuriko na tutampa ushirikiano wa kutosha yeyote atakayeleta msaada,” amesema.
“Dk Rose Rwakatare ni mfano wa kuigwa kwa wananchi wa Wilaya ya Kilombero, huyu anamoyo wa kipekee kwasababu kila linapotokea tatizo amekuwa msaada mkubwa kwenye Wilaya ya Kilombero,” amesema Msuya.
Alisema kuna watu wanataka kutoa msaada lakini wanaogopa kutokana na sababu za kisiasa hivyo amewatoa hofu kwamba wajitokeze kusaidia kwani CCM na Serikali zitawalinda kwa kuwa siasa ni mpaka 2025.
“Kwa sasa hakuna siasa hapa tunaamini tunamadiwani na wabunge lakini tuko kwenye utendaji hatuko kwenye siasa kwa hiyo Dr. Rose najua una marafiki huko mjini, wewe ni Mwenyekiti wa Wazazi CCM mkoa wa Morogoro, unawadau wengi tunajua unauwezo wa kuhamasisha wananchi wakaja kuleta misaada,” alisema.
Picha zote na Mpiga picha wetu, Morogoro.
Sunday, April 21, 2024
ULEGA ASHIRIKI MKUTANO WA 39 WA BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI WA EAC
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega ameshiriki Mkutano wa 39 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji kuhusu uendelezaji wa viwanda vya ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki hususani katika kuendeleza viwanda vya nguo, ngozi, pamba, madawa, matunda na mbogamboga.
Mkutano huo unaofanyika jijini Arusha kuanzia Aprili 17-20, 2024 umehusisha Mawaziri wengine wa kisekta kutoka Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, Sudan Kusini na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC).
Mawaziri wengine kutoka Tanzania walioshiriki mkutano huo ni Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda kutoka Zanzibar, Mhe. Omar Said Shaaban, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Stephen Byabato, Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe.
Saturday, April 20, 2024
WAJASIRIAMALI WANAWAKE PWANI WATAKIWA KUZINGATIA UBORA WA BIDHAA ZAO.
Mwanasheria wa Halmashauri ya Bagamoyo, Hemedi Malogo (katikati) akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Shauri Selenda, katika kufunga mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Chama cha Wanawake wafanyabiashara (TWCC) ambayo yamefanyika wilayani Bagamoyo.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa TWCC Bi Mwajuma Hamza, Mwenyekiti wa Bodi ya TWCC Taifa, na kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Tred Mark Afrika (TMA) Bi Ester Utamis, Mwenyekiti wa TWCC mkoa wa Pwani, Bi Stela Gwassa.
...........................................
Na Athumani Shomari
Bagamoyo
Wajasiriamali wanawake Mkoani Pwani walio chini ya Chama cha Wanawake wafanyabiashara (TWCC) wametakiwa kuzingatia ubora wa bidhaa zao ili kuingia katika ushindani wa soko huru la Afrika (AFCFTA)
Akifunga mafunzo ya siku mbili ya Chama cha Wanawake wafanyabiashara (TWCC) yaliyofanyika wilayani Bagamoyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo, Shauri Selenda amesema bidhaa zenye ubora huongeza thamani na kuweza kukabiliana na ushindani uliopo sokoni.
Katika hutuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mwanasheria wa Halmashauri ya Bagamoyo, Hemedi Malogo, Selenda amesema wajasiriamali wa Mkoa wa Pwani wanaweza kutumia mazao yanayopatikana mkoani humo ili kujiongezea kipato.
Alisema mkoa wa Pwani una bidhaa za Kilimo, Mifugo, Uvuvi, pamoja na ufugaji ambapo vyote hivyo vikitumiwa vizuri vinaweza kukuza pato la mtu mmoja mmoja, familia na hatimae Taifa kwa ujumla.
Aliendelea kueleza kwa kusema kuwa, swala la uwezeshaji wanawake na vijana kiuchumi, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na mama Dkt. Samia Suluhu Hassan imekuwa ni sehemu ya kipaumbele chake.
Alisema kutokana na umuhimu huo, Tanzania imekuwa Mwanachama wa Jumuiya mbalimbali za maendeleo ya kikanada na kimataifa ikiwemo jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) na imeridhia utekelezaji Mktaba wa eneo la soko huru la Afrika (AFCFTA) ili kutoa fursa za masoko kwa watanzania.
Selenda alisema, ni matumaini ya Serikali kuona wajasiriamali wanazitumia vizuri fursa hizo ili waweze kunufaika nazo kwakuwa Tanzania inazalisha bidhaa nyingi zenye ubora hivyo wanawake wanatakiwa wawe mstari wa mbele katika kuchangamkia fursa.
Alimalizia kwa kuzitaka Taasisi mbalimbali za Serikali ambazo zimeshiriki kwenye mafunzo hayo, kushirikiana na wafanyabiashara hao kuhakikisha bidhaa zao zinafuata taratibu na kanuni zote ili ziweze kukua, na kuwa endelevu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Wanawake wafanyabiashara Taifa (TWCC) Bi Mercy Emanuel Sila amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wafanyabiashara wanawake kuhusu taratibu, Sheria na kanuni za kufanya Biashara maeneo waliyopo na kwenye soko la Afrika (AFCFTA).
Alisema kupitia TWCC wanawake wanaweza kupiga hatua ya kimaendeleo kwenye biashara zao na kujua njia mbalimbali za kukuza mitaji, kuboresha biashara na kutafuta masoko.
Alitumia nafasi hiyo kuishukuru Serikali kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Sukuhu Hassan kwa kutoa umuhimu juu ya wanawake na kutengea asilimia 10 ili kujiemdeleza kupitia vikundi vyao.
Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wamesema wanaishukuru TWCC kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo yamewajengea uelewa mkubwa katika maswala mbalimbali yahusuyo biashara.
Wamesema kupitia mafunzo hayo wamepata uelewa juu ya ulipaji kodi, uelewa juu ya kupata kusajili majina ya Kampuni, kupitia Taasisi na mashirika yaliyokuwepo kwenye mafunzo hayo.
Mashirika yaliyokuwepo kwenye mafunzo hayo kwa lengo ka kutoa elimu ni Mamlaka ya mapato nchini (TRA) Shirika la viwango nchini (TBS) Shirika la kuhudumia Viwanda vidogo (SIDO) Wakala wa usajili wa biashara na leseni (BRELA)
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania (TWCC) yamewashirikisha wafanyabiashara wanawake wa mkoa wa Pwani kutoka Halmashauri za Bagamoyo, Chalinze, Kibaha, Mkuranga, Kibiti, na Mafia.






























































