Saturday, November 4, 2023

DKT. ABBAS AONGOZA MAPOKEZI YA WAWEKEZAJI ZAIDI YA 150 KUTOKA MAREKANI

 

Na. Edmund Salaho- Kilimanjaro


Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas ameongoza mapokezi ya wawekezaji zaidi ya 150 kutoka Taifa la Marekani ambao wamewasili katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA) majira ya saa moja na nusu kwa ndege ya Shirika la Oman.


Wawekezaji hao wanatarajia kutembelea vivutio mbalimbali nchini ikiwemo Hifadhi bora Afrika kwa mara tano mfulululizo Serengeti pamoja na kivutio bora Afrika kwa mwaka 2023 ‘Ngorongoro’ lengo likiwa ni kujionea fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana katika vivutio hivyo ambapo wanatarajia kutumia zaidi ya siku 10 katika vivutio hivyo.


Aidha Dkt. Abbas, aliongozana na viongozi mbalimbali wa Taasisi za Uhifadhi kutoka TANAPA na Ngorongoro. 








Friday, November 3, 2023

MZEE MBAGALA, MDAU WA MAENDELEO BAGAMOYO ATUA BUNGENI.

 

Mzee, Rajabu Selemani Mbagala (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha nje ya ukumbi wa Bunge, Jijini Dodoma leo tarehe 03 Novemba 2023, katikati ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson na kulia ni Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Mh. Muharami Mkenge, kitoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM kata ya Nianjema ndugu Omar Makamba na katibu mwenezi CCM Kata, Mzee Marijani (Minjori.)


Mzee, Rajabu Selemani Mbagala (kushoto) akiwa katika picha nje ya ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma leo tarehe 03 Novemba 2023, kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Mhe. Eric Shigongo, wa pili kulia ni Katibu mwenezi CCM Kata ya Nianjema Bagamoyo, Mzee Marijani (Minjori.) Waziri wa Maji na Mbunge wa Pangani, Mh. Juma Aweso, Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Mh. Muharami Mkenge,  na wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa CCM kata ya Nianjema ndugu Omar Makamba
..........................................

Na Athumani Shomari- Dodoma

Leo Tarehe 3 November 2023, Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Mheshimiwa Muharami Shaban Mkenge, amemkaribisha Bungeni Mdau wa Maendeleo Jimbo la Bagamoyo Mzee, Rajabu Selemani Mbagala, ikiwa ni nafasi ya kipekee kwa Mzee Mbagala kutokana na umuhimu wake kwa maendeleo ya Bagamoyo.


Mzee Mbagala ni maarufu kwa wakazi wa Bagamoyo kutokana na kujitolea katika maendeleo ya huduma za jamii hasa ukizingatia ni mtu binafsi ambae hana cheo serikalini bali kinachomsukuma ni utu wake dhidi ya binadamu wenzie na kukereketwa kwake na Maendeleo ya mji wa Bagamoyo.


Miongoni mwa mambo aliyoyafanya katika kusaidia huduma za jamii, Mzee, Rajabu Selemani Mbagala ameweza kutoa eneo la kujenga Zahanati katika kitongoji cha Kimarang'ombe kata ya Nianjema, eneo la kuabudia (Msikiti) eneo la kuzikia (Makabuli) kwa waislamu na wakristo, eneo la kujenga ofisi ya Chama Cha Mapinduzi kata ya Nianjema ambapo maeneo yote hayo ameyapima pamoja na kugharamia michoro (survey plan), kwa fedha zake.


Mzee Mbagala aliweza kumiliki maeneo makubwa ya Ardhi ikiwa mji bado haujakua na baadae maeneo hayo kuyapima viwanja na kufanya maeneo kuwa na mitaa mizuri iliyopimwa kitaalamu jambo ambalo linaleta muonekano mzuri wa mji wa Bagamoyo.


Hali hiyo imepelekea Maeneo kadhaa ya Kitongoji cha Kimarang'ombe kuwa na viwanja vyenye muonekano mzuri wa mitaa ukilinginisha na maeneo ambayo hayajapimwa (unplanned areas).


Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Muharami Mkenge, amesema anamshukuru mzee Mbagala kwa kujitolea kwake katika mambo mbalimbali ya maendeleo hali inayoleta chachu ya maendeleo Kata ya Nianjema na Bagamoyo kwa ujumla.


Mbunge huyo Muharami Mkenge amewataka wadau mbalimbali wa maendeleo Bagamoyo kuiga mfano wa Mzee Mbagala ili kuisaidia Serikali katika huduma mbalimbali za kijamii.


Katika safari yake hiyo ya Bungemi Mzee Mbagala amesindikizwa na Mwenyekiti wa CCM kata ya Nianjema ndugu Omar Makamba na katibu mwenezi CCM Kata, Mzee Marijani (Minjori.)



ONDOENI WASI, NCHI IMEHIFADHIWA VIZURI-KIKWETE

 

Maneno hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofis ya Rais Utumishi na Utawala Bora baada ya ziara ya Kamati ya kudumu Bunge inayosimamia Utawala , Katiba na Sheria kutembelea idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa , Dodoma.



Akizungumza mbele ya kamati Mhe. Kikwete pamoja na kuishukuru kamati kwa kufanya ziara ameeleza kuwa ofisi yake itasimamia na kutekeleza maelekezo yote kwa kuwa tayari Serikali imeshatoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika Idara hiyo na mrejesho utatolewa kwa mujibu wa utaratibu mapema iwezekanavyo.


“Ujio wenu hapa umeambatana na maelekezo muhimu sana kwetu ili kuimarisha shughuli zinazofanywa na Idara hii kwa ustawi wa Serikali na Taifa kwa jumla, nasi tuko tayari kutekeleza maelekezo hayo kwa haraka na ufanisi” alisema Mhe. Kikwete.


Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Dkt. Mhagama amemsisitiza Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kuhakikisha ofisi yake inaisimamia vyema Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa katika zoezi la kuhifadhi nyaraka ambazo zimekusanywa hivi karibuni ili ziwe kwenye utaratibu mzuri kama zilivyo nyingine kwa lengo la kuepuka upotevu wowote wa nyaraka hizo. 


Thursday, November 2, 2023

MAGAZETI YA TANZANIA LEO TAREHE 03 NOVEMBA 2023

 





















CCM HAINA MASHAKA NA UTENDAJI KAZI WA WAZIRI MKUU-MAKONDA

 

Asema ni kiongozi mchapakazi na mtiifu, Chama kina matumaini makubwa


 


KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi Paul Makonda amesema CCM haina shaka na utendaji kazi wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwani ni kiongozi mchapakazi na mtiifu.


 


“…Katika utendaji wa kazi sisi upande wa Chama tuna matumaini makubwa na uwajibikaji na uaminifu wa Waziri wetu Mkuu Kassim Majaliwa, tumemuona katika maeneo mengi akisimamia shughuli mbalimbali za Serikali na nilipotoa agizo la Chama kwa Waziri Mkuu nilitaka agizo hilo lifike kwa mtu anayeweza kuleta matokeo chanya kwa Chama.”


 


Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi amesema lengo la CCM chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha Serikali inatimiza kile ambacho imepewa kukifanya kwa mujibu wa ilani ya uchaguzi, hivyo wana matumaini makubwa na utendaji kazi wa Mheshimiwa Majaliwa.


 


Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Novemba 2, 2023) alipokwenda ofisini kwa Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma. Amesema lengo la Chama ni kuhakikisha ndoto ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na kuwatumikia na kuwaletea maendeleo wananchi wote hususani wanyonge inafikiwa.


 


Amesema Waziri Mkuu ni mtendaji mtiifu, mwaminifu na kwamba maelezo yaliyotolewa kwake na CCM kuhusu kushughulikia migogoro ya ardhi tayari ameyapokea na ameanza kuyatekeleza. “Nina imani hata miezi sita tuliyompa inawezekana akatumia hata miezi mitatu tukapata ripoti.”


 


Kadhalika, Makonda amesema Chama kimemwagiza Waziri Mkuu kuwachukulia hatua wote ambao wataonekana kukwamisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ndani ya Serikali. “Yeyote ambaye anabainika kufanya ubadhirifu wa mali za umma na Waziri Mkuu akabaini achukue hatua mara moja na Chama tumempa baraka zote.”


 


Kwa upande wake, Waziri Mkuu amesema Serikali imepokea maelekezo ya Chama na kwamba itaendelea kuyafanyia kazi na kuhakikisha migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini inaendelea kushughulikiwa.


 


Akizungumzia kuhusu suala la udhibiti wa fedha za umma, Mheshimiwa Majaliwa amesema serikali itaendelea kulisimamia jukumu hilo ili fedha zinazotolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo zitumike ipasavyo na katika viwango vya ubora vinavyotarajiwa.


 (mwisho)


IMETOLEWA NA:


OFISI YA WAZIRI MKUU,


ALHAMISI, NOVEMBA 2, 2023. 

KAMATI YA MAPATO YA HALMASHAURI YAWATAKA WADAU WA BIASHARA KULIPA USHURU KWA WAKATI.

 

Kamati ya mapato ya Halmashauri ya Chalinze ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo kwa mujibu wa mwongozo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri imefanya kikao chake leo katika ukumbi wa Ofisi ya Mkurugenzi.


Katika kikao hicho Mwenyekiti ameongoza kikao hicho kwa misingi ya kufanya tathmini ya ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri kwa robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2023/2024. Kamati imefanya tathmini kwa kupokea taarifa ya ukusanyaji mapato kwa vyanzo mbalimbali vya mapato.


Baada ya kikao hicho kamati ya mapato imewaagiza wananchi wote katika Halmashauri ya Chalinze kulipia ushuru na kodi mbalimbali kwa wakati na kuzingatia Sheria taratibu na miongozo ya ulipaji kodi na ushuru huo.


Aidha Kamati hiyo imetoa maelekezo kwa wafanyabiashara kuzingatia taratibu za kufanya biashara kwa kuhakikisha wanakuwa na leseni za biashara na wananchi kuacha ujenzi holela, kujenga pasipo kibali cha Ujenzi ni kosa kwa mujibu wa sheria za mipango miji.


Hata hivyo wajumbe wa Kamati kwa pamoja wamekubaliana kuwa juhudi za ukusanyaji mapato ziongezeke hususan kwa vyanzo ambavyo kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha havikufikia asilimia 25 ya makusanyo na kutolewa taarifa ya makusanyo kila wiki.





 

MAKONDA USO KWA USO NA MAJALIWA DODOMA

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa leo Tarehe 02 Novemba 2023. Amekutana na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM itikadi na uenezi Paul Makonda, Ofisini kwa Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa leo Tarehe 02 Novemba 2023. Amekutana na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM itikadi na uenezi Paul Makonda, Ofisini kwa Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa leo Tarehe 02 Novemba 2023. Amekutana na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM itikadi na uenezi Paul Makonda, Ofisini kwa Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma.