MBUNGE wa
viti maalum Mkoa wa pwani, Subira Hamisi Mgalu (kulia) akimkabidhi Diwani wa kata ya Nianjema, Abdul Mzee Pyalla matofali kwaajili ya ujenzi wa choo katika shule ya mpya ya sekondari inayojengwa katika kata ya Nianjema Halamshauri ya Bagamoyo.
.........................................................
MBUNGE wa
viti maalum Mkoa wa pwani, Subira Hamisi Mgalu, ametoa Tofali 350 kusaidia
ujenzi wa vyoo katika shule mpya za kata zinazojengwa Kata ya Nianjema na
Mapinga zilizopo Halmashauri ya Bagamoyo
Mkoani humo.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi Tofali hizo akiwa kata ya Nianjema Halmashauri ya
Bagamoyo, Mgalu alisema anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Samia Suluhu Hassani kwa kutenga fedha kwa kila Halimashauri ili zitumike
kujenga vyumba vya madarasa ambapo kwa kata za Nianjema na Napinga zimetumika
kujenga shule mpya za kata ambazo hapo awali hazikuwepo.
Aliongeza kwa
kusema kuwa licha ya fedha hizo zilizotolewa kwaajili ya ujenzi wa shule hiyo
ya sekondari, bado baadhi ya kazi zinahitaaji kutekelezwa na Halmashauri, wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo ili
kufanikisha malengo hayo ambapo yeye Mbunge wa viti maalum, mkoa wa Pwani ambae
pia ni mdau wa maendeleo alitoa ahadi ya kuchangia tofali na sasa ametekeleza.
Akielezea
baadhi ya kazi ambazo zinahitaji kutekelezwa na Halmashauri, wananchi na wadau mbalimbali ni pamoja ujenzi
wa vyoo,
‘’ Nilipokuja
Tarehe 21 mwezi wa 11 nilitoa ahadi ya kuchangia tofali 250 katika shule hii
mpya ya Nianjema na Mwenyezimungu amenijaalia leo kutekeleza ahadi yangu’’
Alisema Mgalu.
Alisema mpaka
sasa ameshatembelea shule 25 katika Halmashauri za Bagamoyo, Chalinze, Kibaha
Mji, Kibaha Vijijini, Kisarawe, na Mkuranga ili kukagua miradi ya maendeleo na
kuchangia kwa nafasi yake kama Mbunge anewakilisha Mkoa wa Pwani.
Kwa upande
wake Diwani wa kata ya Nianjema Abdul Pyalla, amemshukuru Mbunge huyo kwa namna
anavyoonyesha ushirikiano wa karibu katika mambo mbalimbali ya maendeleo.
Alisema Mh.
Subira Mgalu ni mfano wa kuigwa kwani kwa hatua hii ya ujenzi ilipofikia tayari
ameshatembelea mara tatu na hasa ikizingatiwa kuwa ana majukumu ya kutembea
mkoa wote wa Pwani na hilo analifanya bila ya kuchoka.
Aidha,
amewapongeza wananchi wa kata ya Nianjema kwa kujitolea mambo mbalimbali
yanayohusu ujenzi huo wa shule mpya ya sekondari katika kata hiyo.
Alisema
wananchi wa kata ya Nianjema ni waelewa na wpo tayari kwa kila
wanachoshirikishwa kuhusu maendeleo ya kata yao.
Wakati huohuo
amewashukuru wadau mbalimbali ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa ni
wenye kujitolea hali na mali katika kufanikisha ujenzi huo
Ujenzi huo wa
shule Kata za Nianjema na Mapinga unatekelezwa kupitia fedha zilizotolewa na
Shirika la fedha la Kimataifa (IMF) kwaajili ya mpango wa maendeleo kwa ustawi
wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19, ambapo Halmashauri ya Bagamoyo imepokea
shilingi Bilioni 1.4
MBUNGE wa
viti maalum Mkoa wa pwani, Subira Hamisi Mgalu akizungumza mara baada ya kukabidhi matofali kwaajili ya ujenzi wa choo katika shule ya mpya ya sekondari inayojengwa katika kata ya Nianjema Halamshauri ya Bagamoyo.
MBUNGE wa
viti maalum Mkoa wa pwani, Subira Hamisi Mgalu, (kushoto) akipita eneo la ujenzi wa shule ya sekondari Nianjema kukagua kazi inavyoendelea, kulia ni Diwani wa kata ya Nianjema, Abdul Pyalla pamoja na Diwani wa kata ya Kisutu, Awesu Ramadhani.
MBUNGE
wa
viti maalum Mkoa wa pwani, Subira Hamisi Mgalu, (kushoto) akipita eneo
la ujenzi wa shule ya sekondari Nianjema kukagua kazi inavyoendelea, nyuma yake ni Diwani wa kata ya Nianjema, Abdul Pyalla pamoja na Diwani wa
kata ya Kisutu, Awesu Ramadhani.


MBUNGE
wa
viti maalum Mkoa wa pwani, Subira Hamisi Mgalu, akiwa anachapia udongo kwenye moja ya chumba cha darasa katika ujenzi wa shule ya sekondari unaojengwa kata ya Nianjema Halmashauri ya Bagamoyo, Mgalu alifika eneo hilo la ujenzi kukaabidhi matofali yatakayotumika kujenga choo.