Thursday, October 21, 2021

RAIS DK.MWINYI AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUWA IKULU ZANZIBAR

No description available.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe.Jaji Khamis Ramadhan Abdalla  kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Mahkama Kuu Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar

No description available.

Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Balozi Masoud Abdalla Balozi  kuwa Katibu wa Rais wa zanzibar -Ofisi ya Rais – Ikulu   hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

No description available.

Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Capt.Khatib Khamis Mwadini   kuwa  Naibu Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) wakati wa  hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

No description available.

Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Bw.Suleiman Abdulla Salum  kuwa Katibu wa Tume ya Utangazaji hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

No description available.

Viongozi walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza a Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi wakiangalia hati za Viapo vyao kabla kuapishwa rasmi katika hafla  iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

No description available. 

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman (kulia) Abdulla,Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid pamoja na Viongozi wengine ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi   walioteuliwa na Rais  wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza wa Mapinduzi   Dk.Hussein Ali Mwinyi hivi karibuni  katika hafla  iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

No description available.

Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akiwa amesimama na Viongozi wengine wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa na Kikundi cha Brass Band  cha  Jeshi la Polisi katika hafla ya kuapishwa Viongozi   aliowateuwa hivi karibu kushika nafasi mbali mbali za Uongozi hafla  iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

 No description available.

Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakiwa katika Hafla ya kuapishwa Viongozi walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi hivi karibuni,hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar

 No description available.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi aliowateuliwa hivi karibuni (nyuma waliosimama) na Kaimu Jaji Mkuu wa Mahkama Kuu Zanzibar Mhe.Jaji Khamis Ramadhan Abdalla (wa nne kulia) wakiwepo na viongoze wengine wakuu,baada ua hafla ya kiapo leo Ikulu Jijini Zanzibar.

Picha na Ikulu

 

TANZANIA KUTUMIA MKUTANO WA TATU WA WANAWAKE URUSI KUZIDI KUWEZESHA WANAWAKE

 No description available.

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Mwajuma Magwiza akishiriki katika moja ya mkutano katika Mkutano wa tatu wa Wanawake nchini Urusi uliofanyika Oktoba 13-15 jijini Saint Petersburg.

..........................................

Na WAMJW Saint Petersburg Urusi

Tanzania imeazima kuendelea kuwawezesha wanawake katika nyanja mbalimbali ikiwemo Uongozi na uwezeshaji Wanawake kiuchumi kupitia Majukwaa ya uwezeshaji wanawake Kiuchumi.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Mwajuma Magwiza wakati akizungumzia namna Tanzania ilivyojifunza kutokana na Mkutano huo wa wanawake nchini Urusi.

Bi. Mwajuma amesema kuwa Tanzania imejifunza kuwa Wanawake wanaweza kushiriki katika Sekta mbalimbali na kutoa mchango wao kwenye Sekta husika na kutumia fursa hizo kupata ajira na kuajiri wengine.

Ameongeza kuwa Tanzania inahimiza Wanawake kushiriki katika uchumi wa viwanda ila kutokana na Mkutano huo imeleta changamoto mpya za kuangalia maeneo ambayo wanawake wanaweza kushiriki ili kupata fursa za kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo.

Ameyataja maeneo hayo kuwa ni sanaa ya uigizaji, ulimbwende na michezo ambapo wanawake wanaweza kushiriki vizuri iwapo kutakuwa na mazingira mazuri yanayoweza kuwa na tija kwenye maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

“Katika Sekta hizi inabidi tuangalie ni maeneo yapi na yana changamoto gani kwa wanawake ili tuwasaidie waweze kufika Kimataifa katika Sekta hizo” alisisitiza Bi Mwajuma

Aidha, ameongeza kuwa Tanzania imeshaanza na inaendelea kuwawezesha wanawake katika Uongozi na majukwaa ya Uwezeshaji Kiuchumi kwenye ngazi za Wilaya na Mkoa ili kuweza kuwapa fursa katika Sekta mbalimbali.

“Nimejifunza kuwa katika kila eneo ambalo mwanamke anafanya kazi inatakiwa kupaangalia na kuona ana changamoto zipi na kumuwezesha ili aweze kuinuka Kitaifa na Kimataifa” alisema Bi. Mwajuma

Tanzania imeshiriki katika Mkutano wa Tatu wa Wanawake nchini Urusi uliofanyika nchini humo kuanzia tarehe 13-15 Oktoba 2021 ambapo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Dorothy Gwajima alimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan.