Saturday, December 21, 2019

OCODE YATOA ELIMU JUMUISHI KWA WALIMU NA WANAFUNZI NA WAZAZI MANISPAA YA UBUNGO


Meneja wa  Uwezo Tanzania  Zaida Mgalla akizungumza na washiriki hawapo pichani wa  mdahalo wa uwajibikaji wa pamoja katika kuleta elimu bora na jumuishi  katika manispaa ya Ubungo uliowashirikisha wazazi, walimu, wanafunzi, viongozi wa dini pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali za mitaa pamoja na wadau wa maendeleo katika sekta ya elimu.
 ............................................

VICTOR MASANGU, DAR ES SALAAM.

KATIKA kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuboresha sekta ya elimu hapa nchini hususan kwa wanafunzi wa shule za msingi hasa kwa wale wenye mahitaji maalumu  Shirika la Organization for Community Development (OCODE) limeamua kuja na mpango wa kutoa mafunzo kwa walimu, wanafunzi na wazazi kuhusiana na umuhimu wa elimu bora na elimu  jumuishi pamoja na kujadili changamoto zilizopo ili kuzitafutia ufumbuzi.


Hayo yamebainishwa na  Afisa miradi kutoka shirika  hilo la OCODE Tunu Sanga wakati wa mdahalo wa uwajibikaji wa pamoja katika kuleta elimu bora na jumuishi lengo ikiwa ni kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi wanapata haki  yao ya upatikanaji wa elimu iliyo bora kwa ajili ya kuleta mabadilik chanya ya kimaendeleo katika siku zijazo.


Aidha alisema kwamba lengo kubwa la Shirika lao ni kushirkiana na wadau mbali mbali wa sekta ya elimu kukaa pamoja na kujadili mambo mbali mbali ambayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa katika mfumo mzima wa kuwa na elimu jumuishi na elimu iliyobora hasa katika makundi ya watu wenye ulemavu na wale wenye mahitaji maalumu.


“Tupo katika mdahalo huu ambao tumeamua kuuandaa  kwa kushirikiana na watu mbali mbali wakiwemo viongozi wa dini, viongozi wa serikali za mitaa, walimu, wazazi, pamoja na wanafunzi ili tuone ni namna gani tunaweza kufika mbali katika suala zima la kuwa na elimu jumuishi hivyo kwa sasa tupo katika manispaa ya ubungo na kwamba tutaendelea katika maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam,”alisema Sanga.


Kwa upande wake  Afisa elimu vifaa  na Takwimu katika Manispaa ya Ubungo  Brayson Maleko amebainisha kwamba kwa sasa kumekuwepo na matukio mbali mbali ya vitendo vya kikatili na unyanyasaji kwa baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi kulawitiwa  kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo wazazi na walezi kuwa na malezi mabaya kwa watoto wao.


Pia katika kupambana na hali hiyo kwa sasa Manispaa ya ubongo imeanzisha kampeni maalumu kwa ajili ya kupita katika kata zote 14 lengo ikiwani ni kutoa elimu pamoja na kukataa na kupinga kabisa vitendo vya mtoto wa kiume kulawitiwa kwani ni kinyume kabisa na sheria na taratibu za nchi zilizowekwa na kuwaasa wazazi kuhakikisha wanalisimaamia kwa pamoja suala hilo lisiweze kujitokeza tena.


“Ndugu mwandishi kwa sasa wanafunzi  wa kiume wapatao 12 katika shule moja ya  msingi  iliyopo katika  Manispaa ya Ubungo Jijini Dar e es Salaam  wamebainika kufanyiwa vitendo  vya ukatili ikiwemo  kulawitiwa na wazazi wao na wengine kulawitiana wenyewe kwa wenyewe kutokana na sababu  mbali mbali ya ukosefu wa elimu pamoja na malezi mabaya kutoka kwa wazazi wao na walezi,”alisema Maleko.


Kwa upande wake Meneja wa  Uwezo Tanzania  Zaida Mgalla  aliwaasa wazazi na walezi kuhakikisha wanawalinda na kuwatunza watoto wao ili waweze kujitambua na kuepukana na vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuwataka walimu kuwa na nidhamu, huku  mmoja wa walimu walioshiriki katika Mdahalo  huo  Ambrose Mbwala  amesema kuwepo kwa  baadhi ya wanafunzi kufanyiwa  ulawiti vinatokana na tabia ya kushiriki mambo mabaya ya mitani ikiwemo, ngoma, utandawazi, pamoja na vigodoro vya usiku.


MDAHALO huo umewajumjisha wadau mbali mbali wa sekta ya elimu, viongozi wa dini, viongozi wa serikali za mitaa, wazazi, wanafunzi, pamoja na walimu kwa lengo la kuweza kuhakikisha elimu bora na elimu jumuishi katika ngazi za shule za msingi ili kuweza kuboresha sekta ya elimu  kwa kushirikiana na serikali ya awamu  ya tano.

Afisa elimu vifaa  na Takwimu katika Manispaa ya Ubungo  Brayson Maleko akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusina na mikakati ambayo wamejiwekea katika kusaidia na kuinua sekta ya elimu ikiwemo kuanzisha kampeni ya kuondoa vitendo vya ukatili kwa watoto wa mashuleni. 
Baadhi ya wakufunzi wa mdahalo huo wakiwa wanafuatili mdahalo ulioandaliwa na shirika la OCODE  kuhusiana na suala zima  la elimu jumuishi na elimu bora katika maeneo mbali mbali hususan kwa wanafunzi wa shule za msingi katika manispaa ya Ubungo. 
Mmoja wa walimu kutoka shule ya msingi Goba  iliyopo katika Manispaa ua Ubungo Ambrose Mbwala ambaye alishiriki katika mdahalo huo akitoa ufafanuzi juu ya changamoto ambazo zinapelekea baadhi ya wanafunzi kujiingiza katika mambo ambayo hayana faida kwa jamii.
 
Baadhi ya wanafuniz kutoka katika baadhi ya shule za msingi zilizopo katika manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaa wakiwa wanafuatilia mdahalo huo ambao umeandaliwa na shirika la OCODE kwa lengo la kujadili namna ya kushirikiana katika suala la elimu jumuishi na elimu bora 
Walimu kutoka shule tofauti za msingi wakiwa wanafuatilia mwenendo mzima wa mhadalo huo ukiendelea katika maeneo ya Kiluvya madukani wenye lengo la kujadili mambo yanayohusina na sekta ya elimu jumuishi hasa kwa watoto wa shule za msingi.
(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)

WAZAZI PANGENI JINA LA MTOTO MAPEMA- DC KAWAWA


Na Omary Mngindo, Chalinze

WAZAZI wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wametakiwa kuandaa majina ya watoto watakaozaliwa mapema, hatua itakayowarahisishia kupata matangazo yenye majina.

Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa wilaya hiyo Zaynabu Kawawa, akizungumza na wananchi wa Chalinze kabla ya uzinduzi ulioenda sanjali na ugawaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa Halmashauri hiyo, ambapo watoto 11,816 kati ya 37778 wamepatiwa vyeti vyao vya kuzaliwa.

Alisema kuwa hatua ya wazazi kukubaliana jina la mtoto kabla ya kuzaliwa, itaondoa usumbufu wa upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa unaotokea hivi sasa, kwani mtoto atakapozaliwa tu kwenye cheti chake kitaandikwa jina lake.

"Niwashauri wazazi wenzangu tubadilike, tuandae majina ya watoto watakaozaliwa mapema, ili kuondokana na adha inayopatikana katika upatikanaji wa vyeti vyao, kwani mtoto akiwa na jina mapema katika cheti chake litaandikwa, hivyo kuondoa usumbufu usio wa lazima," alisema Kawawa.

Awali Mganga Mkuu wa halmashauri ya Chalinze Dr. Ernest Kyungu akisoma taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji Amina Kiwanuka, imeeleza kwamba mpango wa usajili wa watoto chini ya miaka mitano unalenga kumwezesha kila mtoto kupata cheti cha kuzaliwa.

"Vilevile mtoto atakayezaliwa kuanzia siku ya utekelezaji wa mpango huu anasajiliwa ndani ya muda mfupi baada ya tukio la kizazi kutokea, serikali kupitia Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini  (RITA) na kutekelezwa kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo," ilieleza taarifa hiyo.

Dr. Kyungu aliongeza kwamba chimbuko la mpango huo ni kutokana na ukweli kwamba, idadi kubwa ya wananchi hawajasajiliwa hivyo hawana vyeti vya kuzaliwa, hatua ambayo serikali imeamua kulipatia ufumbuzi.

"Kwa mujibu wa sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012, ni asilimia 13.4 tu ya wa-Tanzania Bara waliosajiliwa na kuwa na vyeti vya kuzaliwa, baada ya kubainika kwa changamoto hii, serikali na wadau wa masuala ya usajili walifanya tathmini ya kina juu ya suala hilo," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Friday, December 20, 2019

Wadau wa elimu Songea wataka wazazi wabanwe walipie gharama za chakula kwa watoto wao mashuleni




Joyce Joliga,Songea 
Bado kuna changamoto kubwa ya wanafunzi kupatiwa chakula wakati wa masomo hali ambayo imechangia wanafunzi wengi kukatisha masomo, kufeli mithiani yao  na ongezeko la utoro .

Kufatia hali hiyo  Wadau wa Elimu mkoani Ruvuma wameitaka  Wizara ya elimu  kuwabana  Wazazi na walezi wa watoto wanaosoma  madarasa ya awali  na shule za msingi ili waweze kuchangia gharama za chakula cha watoto wao wakati wakiwa shuleni hivyo kuwasaidia wafanye vizuri kwenye masomo yao na kuondokana na madhara ya kiafya ikiwemo vidonda vya tumbo , utoro,  wizi na unyanyapaa.

kwa mujibu wa ripoti ya Makadirio ya watu (National Population Projections) iliyotolewa na Bodi ya Taifa yaTakwimu NBS feb 2018 Makadirio ya idadi ya watoto wenye umri wa kati ya miaka 5 mpaka 8  mwaka 2018 kulikuwa na  watoto 5, 888,072  na 2019 ilikadiriwa kuwa Tanzania itakuwa na watoto 6,184,084
 Aidan Hyella  ni mdau wa elimu  na Mzazi  anatoa ushauri kwa   Wazazi  kushirikiana na  uongozi wa shule waweke mikakati ya pamoja  ili kuweza  kuhakikisha  watoto wanapata  chakula wakiwa shuleni hivyo kuondokana na  tatizo la kufeli mithiani na kuzimia kutokana na njaa

Anasema, mkoa wa Ruvuma umebarikiwa kuwa na chakula kingi lakini bado shule nyingi hazina huduma ya chakula shuleni hali ambayo inamkosesha mtoto haki ya msingi yakupata milo mitatu na hivyo kudhoofisha akili na mwili”
“Tubadilike wazazi hivi tunajisikia Amani watoto wetu wanashinda na njaa sisi tunakula , nafikiri wakati umefika sasa wa kuwasaidia hawa watoto kupata chakula mashuleni kwani ile Shea yake ambayo angekula akiwa nyumbani ndio atakayokula akiwa shuleni, tuache ubinafsi tuchangie chakula cha watoto wetu,”anasema Aidan

Samimu Ngonyani ni mwanafunzi wa Darasa la pili shule yamsingi Luhila anasema kukosekana chakula shuleni ni mateso kwa wanafunzi kwani wanaondoka nyumbani bila kimywa chai hivyo Wapo wanaotembea umbali mrefu kwenda shule na wakati mwingine uamua kuishia njiani na kuomba omba pesa kwa watu na ukifika muda wa kurudi nyumbani nae anarudi.

“Natamani tupewe chakula shuleni kama darasa la Saba na la nne wao wanakula chakula cha shule Sisi tunashinda na njaa na walimu hawatuonei huruma,”anasema

Naye  Jumanne Msabaha   mwalimu mkuu wa shule ya  msingi Skill path  iliyopo Manispaa ya Songea  amesema, tatizo la watoto kutokula shuleni linachangia kufeli kwa wanafunzi kwani wazazi wengi hawataki kuchangia gharamaya chakula cha Watoto wao hali ambayo inawafanya watoto wengi kukosa haki ya kupata chakula  wakati wa masomo ingawa wapo  baadhi ya wazazi ambao ujitoa na kuchangia gharama hizo.

Ametoa mfano kuwa shule hiyo ina wanafunzi  885 ni wanafunzi 194 tu ndio wanaopata chakula  shuleni   ambapo kati yao  wanafunzi wenye umri wa mika 3-8  ambao wanasoma  chekechea na wali   wapo 240 ambapo wanatakiwa  kupata uji wa lishe , chai na chakula cha mchana lakini hawapati kutokana na wazazi wao kutochangia gharama.

“Tumeshakaa vikao  na wazazi si chini ya vitano  vya kuwaelekeza umuhimu wa watoto kupata chakula shulenilakini  bado kuna changamoto wapo wazazi wanakubali kulipa na wapo wanaopinga kwa madai kuwa wanawapa watoto wao pesa za matumizi , hivyo kusababisha watoto kushinda na njaa , watoto wanadondoka kutokana na njaa utakuta mtoto ametoka nyumbani saa 11 alfajiri na hajaandaliwa chochote  hivyo ikifika saa mbili anashindwa kuendelea na masomo kutokana na njaa kali,”alisema Msabaha
Aidha amewataka wazazi kulipa gharama hizo kwani kwa muhula ni sh 40,000 kwa watoto wa awali na chekechea  na kwa wanafunzi wa darasa la kwanza hadi lasaba ni sh 300,000 kwa mwaka ambapo chai mtoto anapewa bure na chakula ambacho anapewa mchana ni wali , nyama , maharage, mboga za majani na tunda . 

kwa upande wake Fatuma Shaban mpishi wa chakula shule yaskill path anasema pamoja na  jitihada mbalimbali zilizofanywa na uongozi wa shulehiyo kuwashawishi  wazazi watoe  pesa za chakula lakini wanagoma ni wazazi wachache ndio wanaona umuhimu na kulipia gharama hizo  nashindwa kuelewa sijui tatizo lipo wapi labda hali ya uchumi ni mbaya au mwamko  mdogo kwani ni 25% ya wanafunzi ndio wanaopata chakula shuleni.
“Roho inaniuma sana kama mzazi kuna wakati naguswa na kuingiwa na huruma kama mzazi na uamua  kuwasaidia watoto ambao wanaanguka kwa njaa au utakuta mtoto mzazi aliwahi kumlipia  gharama za chakula lakini  ghafla anaamuakusitisha mwanae asile chakula , basi  unakaona kanacheza maeneo ya karibu na unapotoa huduma ya   chakula  na kanawaangalia wenzie wanavyokula hivyo  inabidi umuite na kumpatia chakula , wapo wazazi mnazungumza nao na anaomba umpatie mwanae chakula kwa maelewano kuwa atalipa baada ya  muda flani  lakini  baadaye anageuka na kugoma kulipa gharama hivyo hasara inabaki kwako inasikitisha sana ,”anasema Fatuma.

Mwanafunzi wa shule ya msingi Majimaji   Baraka Haule anasema kutotolewa kwa  chakula mashuleni kunawanyima wanafunzi haki ya kusoma na kufanya  vizuri kwenye masomo kwani utakuta wanawaza  chakula badala ya masomo na kujisikia  vibaya pindi wakiwaona wenzao wanavyokula na wengine ujikuta vichwa vikiwauma kutokana na kutokula
Anasema kutokana na kukosekana chakula shuleni baadhi yawanafunzi wamekuwa wakipwwa pesa na wazazi wao ya kula chakula na wengine hawapewi chochote na kusababisha waingie tamaa ya Kuiba, kufanya kazi za kubeba tofali, kuvuna mahindi na kuosha vyombo majumbani kwa watu iliwapate pesa ya kula na hivyo kukosa masomo.
Thomas Makwaya Mzazi anasema , kama wapo wazazi wanaogoma kuchangia chakula wanakosea sana kwani haiwezikani mtoto ashinde bila kula chochote tangu asubuhi hadi anaporudi  nyumbani kwani hata makuzi ya mtoto  uwezo wa mtoto kuwa kiakili inategemeana  mlo kamili na vyakula mbalimbali vilevile ukuaji wa mwili kiafya ni muhimu watoto wapate chakula bora ili kujenga kiakili na kimwili.

kwa upande wake Mwalimu Nathan Mtega wa shule yaMsingi  Mitawa anasema swala la chakula  kwa watoto lipewe muhimu wa kipekee yeye anafundisha watoto wa chekechea na wenye utindio wa ubongo   wanatoka kwenye shule ambazo awali milo mitatu hivyo kula shuleni kunasaidia kupunguza utoro, kupenda kusoma kuwa mdadisi na kujenga mwananfunzi "kukosekana chakula kunamuathiri mtotoanakuwa siyo msikivu ana kosa raha , pia inavuja morali ya kufundisha kwa mwalimu kwani huwezi kufundisha watoto wakiwa na njaa , hata ukitoa zoezi watoto hawatafanya  hivyo ni muhimu wazazi na viongozi wa shule wakae na kujadili namna ya kumsaidia mtoto kupata mlo shuleni kwani wapo wanafunzi wanaotoka kwenye familia maskini hivyo kutolewa kwa chakula shuleni kunawasaidia kupata japo milo miwili kwa siku hivyo kufanya vizuri kwenye masomo yao."anasema Nathan
Kwa upande wake Afisa Elimu mkoa wa Ruvuma Ephaim Simbeye anasema mkoa wa Ruvuma unashule 789 za msingi ambapo ni shule 347  pekee ndio zinazotoa huduma yachakula shuleni ambapo watoto upatiwa kande au ugali , ambapo ameitaka jamii  kuchangia chakula kwa hiari.
"Wazazi waelewe kuwa kuchangia chakula ni muhimu na jukumu lao kwani  ile shea ya mtoto ambayo angekula nyumbani  anakula shuleni  hivyo kumuondolea maradhi  mbali mbali ikiwemo  vidonda vya tumbo  kumshindiha mtoto bila kula chochote ni ukatili mkubwa ",anasema Simbeye
Anasema kamati za  kukusanya chakula zishirikiane na kamati za wazazi kuhakikisha watoto wanapata chakulashuleni kwani mkoa wa Ruvuma una chakula kingi  ni aibu watoto kushinda bila kula.


watoto 4612 wanaudumavu Ruvuma

Mganga Mkuu Ruvuma Dr.Jairy Khanga


Joyce Joliga,Songea
Watoto 1101 kati ya 4612  walipata matibabu ya utapiamlo mkali katika vituo vya kutolea huduma za afya ambapo lengo ni kuwafikia  watoto wanaosadikika kua na utapiamlo Mkali kutokana na takwimu za Survey.
Akizungumza na Mwananchi Mganga Mkuu mkoa wa Ruvuma Dkt.Jairy Khanga alisema  watoto hao walipatiwa  matibabu  katika kipindi  cha  mwezi July 2018 hadi June 2019, ambapo takwimu za National nutrition survey 2018 zinaonesha mkoa wa Ruvuma bado ni miongoni mwa mikoa yenye hali duni ya lishe kwa watoto chini ya miaka mitano ikiwa udumavu ni 41% kitaifa ikiwa ni 31.8%, Ukondefu kwa watoto ni 3% kitaifa ikiwa ni 4% na uzito pungufu ikiwa ni 16.5% kitaifa ikiwa ni 14.6%.

AlisemaUtapiamlo huathiri afya, uzalishaji mali na maendeleo katika jamii. Athari hizo hujitokeza kwa njia mbali mbali kama Kupungua kwa uwezo wa akili hivyo watoto kupata ugumu wa kufundishika na kuelewa  Kuchelewa katika hatua za ukuaji wa mtoto kimwili na kiakili.
Anazitaja athari nyingine ni  Kuongezeka kwa magonjwa na vifo vya watoto
Ikiwa ni pamoja na  Kuongezeka kwa magonjwa na vifo kwa wanawake wajawazito
na Kupungua kwa kinga ya mwili na  Kuongezeka kwa walemavu, mfano mgono wazi na vichwa vikubwa na Kupungua kwa uwezo wa kufanya kazi na uzalishaji mali.

 Kwa upande wake Ofisa Lishe Mkoa Eugenia Kombeo alisema,  , tayari mikakati mbalimbali imewekwa ili kuboresha hali za lishe za watoto wadogo ikiwa ni pamoja na Elimu ya lishe kutolewa ipasavyo katika vituo vya kutolea huduma za afya na katika Jamii kupitia wahudum wa afya ngazi ya vijiji kwa wajawazito na wamama wanaonyonyesha ,kuanzia July 2018 hadi june 2019 wamama na walezi 60865wenye watoto wenye miez 0-23 walipatiwa elimu ya usahihi wa ulishaji wa watoto wachanga na wadogo.

Naye Aureria Mhagama mkazi wa Mshangano alisema tatizo la Lishe duni limechangiwa na baadhi ya wakinamama kutohudhuria kliniki hivyo kukosa elimu sahihi hali ambayo imesababisha watoto wengi kudumaa na wengine kupoteza maisha.