Saturday, December 7, 2019

WAFANYABIASHARA MBAGALA WAVUTIWA NA HUDUMA ZA TRA KUWAFUATA.

Na Shushu Joel

WANANCHI wa Mbagala jijini Dar es Salaam wamevutiwa na kitendo Cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwapelekea huduma ya utoaji Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) zoezi ambalo linaloendeshwa katika mkoa huo.

Wakizungumza mara baada ya kusajiliwa na kuwa walipakodi wafanyabiashara wa maeneo hayo wamekoshwa na huduma ya kufuatwa mahali walipo.

Monira Said ni mmoja wa wateja waliopatiwa huduma za TIN kwa mara ya kwanza alisema kuwa huduma wanazozitoa watu wa TRA ni zenye kiwango cha kipekee.

"Nimefurahia sana kukabidhiwa TIN yangu kwa mara ya kwanza tena bure huku nilikuwa nikijua labda huduma hii ni ya malipo kumbe hapana" Alisema.

Aliongeza kuwa kwa wale ambao hawajachangamkia nafasi hii ni bora wakajitokeza mapema hili waweze kupata huduma za TRA kwani mafanikio makubwa watayaona mara baada ya kuwa katika mfumo wa TRA.


Aidha, alitoa ushauri kwa maofisa wa TRA kuwa mbagala kwa sasa ni moja ya sehemu zinazokuwa kibiashara na moja ya maeneo yenye biashara kubwa hapa jijini Dar es Salaam kama kariakoo.

Naye Haji Khareed ni mwenyekiti wa wafanyabiashara wa nguo katika soko la mbagala alisema kuwa tangu vijana wengi walikuwa wakiwasubili Kwa hamu kubwa watu wa mamlaka ya mapato (TRA) ili wawaelimishe juu ya umuhimu wa kulipa kodi.

Aliongeza kuwa kufuatwa kwa wateja kwenye maeneo yao ya kazi kumewafanya kujiona ni watu wenye thamani sana katika nchi hii.

"Ukilipa kodi unasaidia nchi kutekeleza miradi mikubwa ya kimaendeleo hivyo kila mmoja wetu awajibike katika kulipa kodi na faida lazima aione "Alisema mwenyekiti Khareed.

Naye Afisa mwandamizi wa elimu kwa mlipa kodi Catherine Mwakilagala amewashukuru wafanyabiashara wa mbagala kwa kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupata huduma toka TRA.

Hivyo amewataka kuendelea kujitokeza pindi wanaposikia watendaji wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) wamekuja waweze kujitokeza kwa wingi ili kupatiwa huduma. Aidha amewapongeza wakazi wa mbagala kwa kumiminika kujitokeza kupata huduma za elimu.
 

Friday, December 6, 2019

MAAFISA HABARI WAPONGEZWA KWA KUISEMEA VIZURI SERIKALI

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Ally Possi  akitoa maelekezo kwa uongozi wa Chama cha Maafisa Habari Tanzania (TAGCO) wa kuendeleza mpango wa kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa maafisa habari wa serikalini leo alipokuwa akifunga mafunzo ya maafisa hao yaliyokuwa yakifanyika jijini Dodoma kwa siku tano.
..........................................


Na Shamimu Nyaki – WHUSM,Dodoma

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo  Dkt.Ally Possi amewapongeza Maafisa Habari,Uhusiano na Mawasiliano Serikalini kwa kutangaza vizuri shuguli za Serikali ikiwemo miradi inayotekeleza ambayo itawaletea wananchi maendeleo.


Dkt.Possi ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akifunga mafunzo ya kimkakati ya Uandishi wa Habari za Serikali ya awamu ya pili kwa  Maafisa Habari,Uhusiano na Mawasiliano Serikalini ambapo amewataka kutumia elimu waliyopata kuendelea kuhabarisha umma kwa weledi na kwa usahihi habari zinazohusu Serikali.


“Maafisa Habari mnafanya vizuri katika kutangaza shughuli za Serikali kwa wananchi,naomba muendelee kufanya hivyo kwa kuwa kada yenu ni muhimu katika kufikisha ujumbe wa Serikali kwa wanachi na mtumie kalamu zenu vizuri ili kulinda na kudumisha amani ya nchi yetu”alisema Dkt. Possi.


Aidha Dkt.Possi amewataka waandaaji wa mafunzo hayo kuendelea kutoa mafunzo hayo mara kwa mara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali pamoja na kutumia mifumo tofauti ya ndani na  nje ya nchi pamoja na kufanya tathmini ili kuona mabadiliko yaliyopatikana kutokana na mafunzo hayo.


Hata hivyo Dkt. Possi aliwashauri Maafisa Habari wote wa Serikali kujiunga na Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) ili kurahisisha mawasiliano miongoni mwao pamoja na kushirikiana katika kazi wanazofanya  ikiwemo kubadilishana uzoefu na kusaidiana kijamii na kitaaluma.


Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi  Idara ya Habari –MAELEZO Bw.Rodney Thadeusi amesema kuwa jukumu la maafisa habari wa Serikali ni kutoa taarifa sahihi na  kwa wakati zinazohuzu Serikali kwa wananchi kutumia njia zote za mawasilano.


“Maafisa habari kazi yetu kubwa ni kuisemea Serikali tusiposema sisi wengine watasema na wengine wanaweza kusema ambayo sio sahihi na wakati mwingine kukosoa hata yale mazuri ambayo Serikali inatekeleza kwa wananchi wake hivyo tuendelee kutumia taaluma yetu kuitangaza vizuri  Serikali”alisema Bw.Rodney.


Naye  Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bibi.Sara Msika amesema lengo la  mafunzo hayo ni kuendelea kuboresha taaluma ya maafisa hao katika kipindi hiki ambacho dunia imekuwa na mabadiliko makubwa katika kada hii ya uandishi wa habari.


Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo  Afisa Habari kutoka TBC Bibi.Catherine Nyoni ameshukuru waandaaji wa mafunzo hayo kwa kuona umuhimu wa kutoa mafunzo kwa Maafisa Habari Serikalini ambayo yamesaidia  kuboresha taaluma yao pamoja na kubadilishana uzoefu.


Mafunzo hayo ya siku tano yalioandaliwa na Idara ya Habari –MAELEZO pamoja na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) yamekuwa na mada mbalimbali ikwemo namna ya kutumia mitandao ya kijamii kuhabarisha umma pamoja na uandishi mzuri wa habari za Serikali.


 

MAJAMBAZI YAIBA MILIONI 3 KIBAHA.

VICTOR MASANGU, PWANI.

JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani linawasaka watu sita wanaodhaniwa  kuwa ni  majambazi baada ya kuvamia katika kiwanda cha kutengenezea vifungashio kilichopo maeneo ya Picha ya ndege Wilayani Kibaha nakufanikiwa kuiba kiasi cha shilingi milino 3, simu nne za  mkononi, pamoja na kompyuta mpakato mbili.  


Akizungumza na waandishi wa habari Ofisni kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamisshna Msaidizi wa Polisi (ACP) Wankyo Nyigesa, amesema kwamba tukio hilo limetokea usiku wa kumakia leo  majira ya tisa usiku ambapo pia waliwashambulia wamiliki wa kiwanda hicho  wakiwa na silaha mbali mbali za jadi ikiwemo marunga, mapanga, na nondo na kukimbilia pasipojulikana na kwamba walinzi wa kiwanda hicho wanashikiliwa.


Katika hatua nyingine Kamanda Wankyo  amebainisha kuwa Polisi mkoani humo imewakamata  watu nane  akiwemo daktari wa idara ya mifugo kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa mifugo aina ya mbuzi na kondoo  pamoja na kuuza nyama ya ng’ombe kilo 405 isiyokaguliwa katika eneo la halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani ambapo watuhumiwa wote wamefikishwa mahakamani.

Thursday, December 5, 2019

WANANCHI BUZA WAMIMINIKA KUPATA HUDUMA TRA.

Na Shushu Joel. 

WANANCHI wa Buza jijini Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi kwenye banda la utoaji wa huduma na Elimu kwa mlipa kodi.

Wakizungumza kwa wakati tofauti mara baada ya kuhudumiwa na kukabidhiwa kwa vyeti vyenye Namba ya Utambulisho wa Mlipakodiza, wameipongeza mamlaka hiyo kwa kuwapelekea huduma milangoni mwao.

Gift Bosco (47)ni mkazi wa buza ninaipongeza mamlaka ya mapato Tanzania kwa utoaji wake wa elimu kwa kutufuata wakazi wa buza.

"Nimefanikiwa kupata TIN ninaamini huu ni mwanzo wa kuwa miongoni mwa walipa kodi wazuri"

Aliongeza kuwa wananchi wengi hawana uelewa juu ya umuhimu wa kulipa kodi hivyo wawe wanaangalia vipindi vya TRA kwenye TV kwani vinaelimisha sana kuhusu umuhimu wa kulipa kodi.

Aidha amewataka mamlaka ya mapato kuendelea kuwatembelea na kuwaelimisha kwani uelewa unaongezeka siku hadi siku.

Naye Muhammad Ally ni mmoja wa wakazi wa Buza na ni mfanyabiashara wa duka amesema kuwa miaka ya nyuma ukiwaona watu wa mamlaka ya mapato Tanzania wanakuja basi unaenda kufunga duka na wewe kwenda kujificha lakini kutokana na elimu pana inayotolewa na mamlaka hiyo wengi wamekuwa waelewa juu ya ulipaji wa kodi.

Aidha, Ally amesifu utendaji wa kazi wa TRA kwa kuwafikia wateja wake tena majumbani kabisa.

Kwa upande wake Meneja wa Elimu kwa mlipa kodi Diana Masalla kutoka TRA alisema kuwa zoezi la utoaji wa elimu linaendelea kila mahali kwa lengo la kuwaelimisha wananchi zaidi.

Hivyo amewapongeza wananchi wa buza kwa namna walivyojitokeza kusikiliza na kuelimishwa umuhumi wa kuwa na TIN na kulipia kodi ya majengo.

Aidha Masalla aliongeza kuwa TRA itaendelea kutoa elimu kwa kila mwananchi ili aweze kunufaika na biashara yake anayoifanya kwani wafanyabiashara wengi wamekuwa wakifeli kutokana na ukosaji wa elimu.

"TRA imetambua thamani yenu na ndio maana tumeamua kuwafuata karibu na biashara zenu ili msifunge na kutufuata mbali sasa tunakufuata mlangoni kwako ili tukuhudumie"