Thursday, October 17, 2019

WATU 51 WASHIKILIWA NA TAKUKURU LINDI.

Na Hadija Hassan, Lindi.


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Lindi inawashikilia viongozi 51 wa vyama 10 vya Msingi vya (AMCOS) vinavyodaiwa na wakulima wa Ufuta wa Mkoa huo kiasi cha Shilingi milioni 486, 869,982 za Msimu wa Mwaka 2019.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Brigedia John Mbungo leo Oktoba 17, kwenye ukumbi wa Taasisi hiyo Mkoani Lindi alisema kuwa ukamatwaji wa viongozi hao wa vyama vya Msingi ni utekelezwaji wa maagizo ya Mh, Rais Dkt, Pombe magufuli.


Alisema Rais Magufuli aliyoyatoa maagizo  Oktoba 15, 2019 katika mkutano wa Hadhara na Wananchi wa wilya ya Ruangwa Kupitia hadhira hiyo Rais Magufuli aliimtaka Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Nchini Brigedia Mbungo pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe , kuhakikisha kuwa vyama kumi vya Msingi (AMCOS) vinavyodaiwa na wakulima wa Ufuta vinalipa fedha hizo kabla ya Msimu wa Korosho kuanza.

Mbungo aliwataja viongozi hao walioshikiliwa na Taasisi hiyo kuwa ni pamoja na Hemedi Yasini kilete – Mwenyekiti , Saidi Hemedi Mkwela – katibu, Twahili Kileta – karani, Hillard Cosmas Chadill – Karani na Hassan Lidemu – Karani wa Chama cha Msingi cha Milindimo AMCOS kwa kudaiwa kiasi cha Shilingi milioni 90,711,354.00 Hasani Lingunja – Karani, Karimu Ngara – Karani wa chama cha Msingi cha Mtonao AMCOS kwa kudaiwa kiasi cha shilingi milioni 73,715,760.00.

Wengine ni Zuber Omary Nolele – Mwenyekiti, Mjamari Haji Kibohu – Katibu wa Chama cha Msingi Kipelele AMCOS Kwa kudaiwa kiasi cha Shilingi milioni 57,257,280.00, Hussein Ally Mnindi – katibu wa Chama cha kinjikikitile AMCOS Saidi Mohamedi Mbunda- Makamu Mwenyekiti, Mathiad Mohamed Likumwili – mjumbe, Chande Mshamu Madudu – mjumbe , Issa Lutumno – mjimbe, Nasra Chingwile karani wa chama cha msingi nachiunga AMCOS kwa kudaiwa shilingi millioni 10,780,100.00.

Ameendelea kuwataja wengine kuwa ni Abdallah Athumani Mtala – Mwenyekiti, Karimu Bakari Maguto – katibu, Hussein Saidi Hussen – Mjumbe, Latifa Abdallah – Karani , Amina Issa Mtauna – Mjumbe wa chama cha Msingi Chikonji AMCOS Kwa kudaiwa kiasi cha Shilingi Milioni 10,325,550.00.

Viongozi wengine ni Zainabu Khalifa - makamu mwenyekiti, Bashiri ally – katibu , Abdallah Abdallah – katibu Msaidizi , Haji juma Namanyanga – Karani, Mohamed Abrahaman Ligoli - Karani, Saidi hashi Nguli – Kalani, Pius Lucas – Karani, Abrahamani Mohamedi Kapanda – Karani wa chama cha Msingi cha Mtama AMCOS kinachodaiwa kiasi cha Shilingi Milioni 8,523,830.00 pamoja na shilingi 160,00.00 za Chama Kikuu cha Ushirika cha Lindi Mwambao.

Aliendelea kuwataja wengine kuwa ni Ally Kinyemela Mtombo – Katibu, Mshamu Mohamedi Ngurangwa – Karani wa Chama cha Msingi Matumbi AMCOS Nurdini Ndope – Mwenyekiti, Shaibu Matumbi – Katibu, Hamza Kumtitima – Katibu Msaidizi Mustafa Chumbo- Mjumbe, Selemani Mtonda – mjumbe, Mponjila Bakari Mponjila karani wa Chama cha Msingi Ruangwa – Mandawa AMCOS kwa kudaiwa kiasi cha shilingi milioni 4,095,200.00,

Mussa Maringa – Mwenyekiti, Jafari Saidi Likwena – Makamu Mwenyekiti, Patrick Martine – Katibu, Abdallah Maringa – Mjumbe Mjumbe wa Bodi, Hassan Mteremko - Karani wa Chama cha Msingi Mchina AMCOS kwa kudaiwa Shilingi milioni 3,604,500. Isumail Mkopi – Mwenyekiti, Hamida Kaulu – Makamu Mwenyekiti, Masoud Hamisi – Katibu, Nadhifu Nauka – Katibu Msaidizi, Isumail Nauka – Mjumbe wa Chama Cha Msingi Mnolela AMCOS kwa kudaiwa na wakulima kiasi cha Shilingi Milioni 3,052,000.00 na Said Mchia – Mwenyekiti, Aziz Mchemba – Katibu, Abubakari Maharagwe – Mjumbe wa chama cha Msingi Mmangawanga AMCOS kwa kudaiwa na wakulima kiasi cha Shilingi milioni 3,314,300,00.


Saidi Nyalubi Mpili – Mwenyekiti, Saidi Likotea – Katibu, Bakari Mpili – Mjumbe wa Chama cha Msingi Mageuzi AMCOS kwa kudaiwa kiasi cha Shilingi milioni 2,630,000,00 Hata hivyo mbunga alisema kuwa kati ya fedha shilingi milioni 436,869,982 zinazodaiwa na wakulima hao wa Ufuta tayari watuhumiwa hao wamesharejesha kiasi cha Shilingi milioni 46, 416,830,00.


Mbunga pia alisema kuwa zoezi la ufuatiliaji wa madeni ya wakulima litaendelea kwa AMCOS za Nyangamara, Namangle, Nahuka huku, Mtua, Kigoli, Malungo, Madwanga, Nanjilinji, “A”, Zinga, Rutamba, Nyangamara, Naambu, mbwemkuru, Mlindimo Mtunaho AMCOS Mbunga pia alitoa rai kwa viongozi wote wa vyama vya ushirika Nchini vinavyodaiwa na wakulima viwalipe wakulima hao haraka iwezekanavyo kabla ya TAKUKURU haijawafikia huku akisisitiza kuwa katika zoezi hilo hakutakuwa na chama ambacho kinadaiwa kitakachobaki salama

SHULE YA EMI YAHITAJI MIL. 80 KUJENGA KITUO.

 
Mkurugenzi wa shule ya Thobias Joachim, akisoma taarifa ya shule hiyo mbele ya mgeni rasmi.
 
Mkurugenzi wa shule ya Thobias Joachim, akimkabidhi taarifa ya shule hiyo mgeni rasmi Meneja wa benki ya CRDB Mkoa wa Pwani Rose Kazimoto.
...................................

Na Omary Mngindo, Kibamba.

SHULE ya EMI School iliyopo Kibamba Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, inahitaji zaidi ya shilingi milioni 80 kujenga Kituo Mtaa wa Kongowe, wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.

Aidha taarifa ya Mkurugenzi wa shule hiyo Thobias Joachim imetanabaisha kwamba, mbali ya wanafunzi wanaoishi na wazazi, pia inawasomesha watoto wanaoshi kwenye mazingira hatarishi, wanaotokea maeneo mbalimbali.


Taarifa ya Mkurugenzi mbele ya Rose Kazimoto Meneja wa benki ya CRDB Mkoa wa Pwani katika mahafari ya tano tangu kuanzishwa kwake, imeeleza kuwa awali walihitaji milioni 200 kwa ajili ya kununua eneo Mtaa wa Kongowe Kibaha ili wajenge kituo kwa ajili ya kuendeleza watoto kielimu.

"Nitumie fursa hii kuwashukuru wazazi na walezi wa wanafunzi, pia wadau waliojitolea katika kufanikisha upatikanaji wa kiasi cha shilingi milioni 120 kati ya shilingi milioni 200, tayari tumeshanunua eneo Kongowe, sasa tunatafuta fedha kwa ajili ta kuanza ujenzi," ilieleza taarifa ya Mkurugenzi huyo.


Akizungumza na wazazi na walezi wa wanafunzi hao, mgeni rasmi Rose alianza kumpongeza Mkurugenzi Joachim na watumishi wake, kwa kuona umuhimu wa kuwasomesha bure watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi, huku akiwaomba wadau kujitokeza kusaidia juhudi hizo.

"Katika taarifa iliyosomwa na Mwalimu Mkuu imegusia changamoto ya sisi wazazi kutolipa ada, niwaase tuwe tunalipa kwa wakati ili tusikwamishe juhudi zinazofanywa na uongozi wa shule, pia tuache kuwahamisha watoto wetu katika shule kwa kukwepa ada," alisema Rose.

Mwenyekiti wa Kamati ya shule Ramadhani Sinale naye amewaasa wazazi kujitokeza katika kusaidia maendeleo ya shule, huku akieleza kwamba imekuwa mkombozi mkubwa katika eneo hilo kwa kuwapatia elimu safi vijana.

"Pamoja na hayo Changamoto za uendeshaji, miundombinu, kitaaluma tunaendelea kuzitatua, pia ada inatugusa wazazi, anajitahidi kuzitatua, hatuna vifaa vya kufundishia kama kompyuta ambavyo ni muhimu hapa shuleni," alisema Sinale.

Wednesday, October 16, 2019

UANDIKISHAJI WAPIGA KURA CHALINZE WAENDA VIZURI

 
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Bi Kasilda Mgeni, akipata maelezo kuhusu hali ya uandikishaji wapiga kura katika jimbo la Chalinze.
.......................................

Na Shushu Joel

Katibu tawala wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Bi Kasilda Mgeni, amefurahishwa na wananchi wa halmashauri ya chalinze kwa kuweza kuitikia wito wa kujiandikisha kwenye daftali la kupiga kura.

Wananchi wamekuwa mstari wa mbele katika zoezi la kujiandikisha kutokana na uelewa wa kutumia fursa ya kuwachagua viongozi wao.

Akizungumza na baadhi ya wananchi katika moja ya vituo vya kujiandikishia alivyotembelea kwenye kata ya ubena, halmashauri ya chalinze katibu tawala huyo aliwapongeza wananchi waliojiandikisha na kuwataka wawahamasishe na wenzao ambao bado ili nao wajiandikishe kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi na moja.

"Kwa kweli chalinze wananchi hongereni sana kwa kujiandikisha kwa wingi nadhani kufikia mwisho wa zoezi hili mtakuwa mmevuka lengo lenu" Alisèma.

Aidha Mgeni amempongeza mbunge wa jimbo la chalinze mh. Ridhiwani Kikwete kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuhamasisha wananchi wake ili wakajiandikishe.


Aliongeza kuwa Kikwete ni kiongozi wa pekee aliyefanikisha kazi ya hamasa kwa wananchi kwani watu wamejitokeza na wanazidi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kujiandikisha na kwa baadhi ya vituo kuonekana wamemaliza kuandikisha huku wakiwa wamevuka malengo yaliyokuwa yamekusudiwa.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani Kikwete alisema kuwa ujio wa kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na katibu tawala imemuongezea nguvu na mzuka zaidi.

Alisema kuwa wananchi wa chalinze wamehamasika wenyewe mara baada ya kutangaziwa na gari maalum lililotolewa na halmashauri kwa ajili ya kuwahamasisha wakazi wa chalinze kuweza kujitokeza.

Aidha Aliongeza kuwa kila kazi inachangamoto zake lakini kwa chalinze changamoto kubwa ni mfululizo wa mvua zilizokuwa zikinyesha hivyo kupelekea wananchi kutojitokeza huku wengine wakiwa mashambani.

"Kwa jinsi hali inavyoelekea wanachalinze tutavuka malengo tuliyokuwa tumejiwekea kwani kwa sasa tuna zaidi 80% huku siku chache zikiwa zimebaki.

Naye msimamizi mkuu wa uchaguzi katika halmashauri hiyo Shabani Milao amempongeza mbunge kwa jinsi alivyojitolea kutoa hamasa kwa wananchi katika zoezi zima la kujiandikisha.

Aliongeza kuwa zoezi linaenda vizuri na wanataraji kufikia lengo lililokusudiwa. kilichokuwa kimekusudiwa na serikali.
 
Katibu tawala wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Kasilda Mgeni, akipata maelezo kuhusu hali ya uandikishaji wapiga kura katika jimbo la Chalinze, pembeni yake ni Mbunge wa hilo, Ridhiwani Kikwete na kulia msimamizi wa uchaguzi katika halmashauri hiyo Shabani Milao.
 
Katibu tawala wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Kasilda Mgeni, akiwa amefuatana na msimamizi wa uchaguzi katika halmashauri ya Chalinze Shabani Milao, wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama (KUU) wilaya, ilipotembelea halmashauri hiyo kukagua vituo vya uandikishaji wapiga kura.


Picha chini na juu zikimuonyesha Katibu Tawala wilaya ya Bagamoyo, Bi Kasilda Mgeni akifuatana na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwet na Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Chalinze, Shabani Milao, wakati Kamati Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ilipofanya ziara katika halmashauri hiyo kukagua vituo vya uandikishaji wapiga kura.

   
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwet, akizungumza katika moja ya vituo vya kuandikisha wapiga kura wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Bagamoyo, ilipotembelea katika jimbo hilo ikiongozwa na Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Bi Kasilda Mgeni.