Monday, August 5, 2019

VULU AKABIDHI KITANDA ZAHANATI YOMBO

Na Omary Mngindo.
Mbunge wa viti Maalumu Mkoa wa Pwani Zaynabu Vulu, mwishoni mwa wiki amekabidhi kitanda katika zahanati ya Kijiji cha Yombo Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Akiambatana na mwenyeji wake Dkt. Shukuru Kawambwa, Vulu alisema kuwa hatua hiyo inalenga kusaidia wakazi hao, ambapo mbali ya kitanda pia amekabidhi vifaa vya kutumika wakati wa kujifungua (delivery kit) na pampas za watu wazima.

Alisema kuwa akiwa mbunge wa Viti Maalum ngazi ya mkoa akishirikoana na wenzake wa majimbo wamekuwa na ushirikiano katika kusaidia kupambana na changamoto zinazowakabili wananchi.

"Wananchi wenzangu leo nimekuja hapa katika zahanati yetu ya Yombo kwa ajili ya kukabidhi kitanda hiki kitakachotumika kwa wagonjwa tunaopaya huduma hii hapa," alisema Vulu.

Nae Dkt. Kawambwa alianza kwa kumshukuru Vulu kwa mapenzi aliyoyaonesha kwa wana-Yombo, kufuatia kukabidhi kitanda godoro pamoja na mifuko yenye vifaa maalumu vya kuwasitiri wagonjwa wa kike na kiume wakati wanapatiwa huduma.

"Wabunge wote kuanzia viti maalumu pamoja na wa majimbo tumekuwa tukifanyakazi pamoja katika kuwatumia wananchi wetu, kipekee nimshukuru Dada yangu Vulu kwa zawadi hii kwa wana-Yombo," alisema Dkt. Kawambwa.

Kwa upande wake muuguzi wa zamu Anna Mzeru mbali ya kumshukuru Vulu, pia amesema kwamba vifaa vilivyotolewa na mbunge huyo vina uwezo wa kuwahudumia wagonjwa watano, huku akiwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia.

Mmoja wa wakazi wa Yombo Semeni Mgeni alielezea changamoto iliyopo katika zahanati yao ikiwemo upungufu wa watumishi ambapo, wapo wawili tu, hivyo kuchangia kutopatilana kwa huduma sahihi kwa muda wote.

"Utakuta mtu anakuja na mgonjwa aidha wa kuchoma sindano lakini kutokana na kuwepo kwa mtumishi mmoja pengine ndio anatoa huduma mfano ya mgonjwa aliyezidiwa anawaacha wengine anamkimbilia huyo wemgine inabidi wasubili," alisema mkazi hiyo.

Saturday, August 3, 2019

MWENYEKITI WA CCM LIWALE AFIKISHWA MAHAKANI KWA TUHUMA ZA KUPOKEA RUSHWA.

Na Hadija Hassan, Lindi.


Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Lindi imemkamata na kumfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Likongowele Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi Mohamedi Nandope kwa Tuhuma za Kuomba na kupokea Rushwa.


Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Mkutano wa Taasisi hiyo Mjini Lindi jana, Kaimu Mkuu wa TAKUKURU wa Mkoa huo, Noel Mseo alisema Nandope alikamatwa tarehe 28/07/2019 majira ya saa moja jioni mtaa wa Nangando Wilayani Liwale kwa tuhuma za kupokea Rushwa kutoka kwa Mtumishi wa Idara ya Afya wa Wilaya hiyo.


Mseo aliwaeleza wanahabari kuwa Taasisi hiyo ilipata taarifa kutoka kwa Raia mwema ya kuwepo kwa mazingira ya kiongozi huyo wa chama cha Mapindizi CCM kuomba Rushwa ambapo ilianza kufuatilia kwa ukaribu na kubaini kuwa Kiongozi huyo alikuwa anashawishi kupewa Rushwa.


Alisema baada ya hapo Taasisi hiyo iliamua kumuwekea Mtego ambapo Mshitakiwa aliweza kufika Eneo la Tukio ambalo walikubaliana na Muhudumu huyo wa Afya na hatimae wakaweza kumnasa akiwa na fedha Taslimu ambazo Tsh. 300,000. ambazo alikuwa ameziomba kwa Mtumishi huyo.


Mseo Alidai kuwa mwenyekiti huyo alikuwa anaomba fedha kutoka kwa mtumishi huyo wa idara ya afya kwa madai kwamba angeweza kumsaidia ili asichukuliwe hatua kutokana na tuhuma za malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya utoaji huduma Dhidi yake.


Hata hivyo Mseo alidai kwamba Taasisi hiyo tayari imeshamfikisha Mahakama ya Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi Mtuhumiwa huyo ambapo kesi yake itatajwa Tarehe 12/08/2019

MTAFITI KUTOKA CHUO KIKUU DSM AELEZA NJIA RAHISI ZA UFUGAJI WA SAMAKI.

Hadija Hassan, Lindi.

Ili kuendelea kupata protini inayotokana na Dagaa wanaotoka kwenye mito, maziwa na bahari Chuo kikuu cha Dar es saalam kupitia kitengo cha Utafiti wa Vyakula vya Samaki Kimeanzisha Njia raisi ya kufuga samaki kwa kutumia vyakula vilivyopo katika maeneo husika.


Hayo yameelezwa jana na Mtafiti wa Vyakula vya Samaki Kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es saalam Dkt. ,Shadrack Ulomi, alipokuwa anazungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG katika viwanja vya Maonyesho ya Wakulima, wafugaji na wavuvi kanda ya Kusini (nane nane) Ngongo manispaa ya Lindi.


Alisema kwa kuzingatia umuhimu wa Protini kwa kiumbe kilicho hai katika ukuwaji samaki kama viumbe wengine na wao wanaitaji protini ya kutosha ili waweze kukuwa vizuri.


Ulomi alisema kwa kutumia wadudu na mimea iliyopo katika maeneo husika wafugaji wa Samaki wataweza kupata vyakula vizuri na vyenye ubora vya kuongeza Protini kwenye samaki wanaowazalisha


“bidhaa ambazo tumewaletea wafugaji hapa ni poamoja na njia raisi ya kufuga samaki kwa kutumia vyakula ambavyo tunaweza tukavitengeneza tukiwa nyumbani ambapo tumeamua kufanya hivyo Endapo Dagaa watakapokwisha kwenye Maziwa na Mito angalau watu waendelee kupata protini za kwenye Dagaa kwa kutumia njia Mbadala kupitia samaki wanaowafuga”


Ulomi aliongeza kuwa kwa kutumia mimea jamii ya Zola ambayo inakiwango cha protini kwa 20%-25%, mimea ya lusina ambayo ina protini zaidi ya 25% -30%, wadudu aina ya Mende wenye Protini 67%-70% wafugaji wa Samaki wanaweza kutengeneza chakula cha Samaki ambacho ni cha bei nafuu.

Thursday, August 1, 2019

MWENGE WA UHURU 2019 WAZINDUA HOSPITALI MSOGA.

 Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali, akiwa pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya kikwete, Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa, pamoja na viongozi wengine waandamizi wa halmashauri ya wilaya Chalinze kwaajili ya kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi ya hospitali ya Msoga kuwa na hadhi ya wilaya.
Image may contain: 12 people, people standing 
RAIS Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete, kushoto kwake ni Naibu waziri wa Nishati ambae pia ni Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani, Subira Hamisi Mgalu, kutoka kushoto ni Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Bagamoyo, John Francis (Bolizozo) Katibu wa CCM wilaya, Salum Mtelela, na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo, Abdul Rashidi Sharifu, wakisubiri kupokea Mwenge katika hospitali ya Msoga.
 
 Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali, akisalimiana na mbunge wa kuteuliwa mama Salma Kikwete.
.........................................  

NA MWAMVUA MWINYI,MSOGA

RAIS Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete ameimwagia sifa wizara ya afya kutokana na kuboresha sekta ya hiyo pamoja na kupandisha hadhi kituo cha afya Msoga kuwa hospital ya wilaya.


Akizungumza baada ya mwenge wa uhuru kuzindua huduma za upasuaji katika hospital ya wilaya iliyopo kata ya Msoga halmashauri ya Chalinze, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, alisema hospital hiyo ilianza kama zahanati hivyo anashukuru kuongezwa hadhi.


Kikwete alieleza, jitihada za kuimarisha sekta ya afya zinazofanywa na serikali chini ya wizara hiyo zinahitaji kupewa pongezi.


"Mimi ni mzaliwa wa Msoga, kitovu changu kilidondokea hapa, nimefarijika kituo hiki kupandishwa hadhi nina imani itakuwa mkombozi kwa wananchi wa Msoga na maeneo jirani kupata huduma ya matibabu ya karibu na kuondokana na kero ya kufuata huduma umbali mrefu, "alisema Kikwete.


Awali mganga mfawidhi hospital ya Msoga ,Daktari Nelson Luoga alisema, hospital hiyo ilianza kutoa huduma za tiba kama zahanati tangu mwaka 1943 .


"Ilipandishwa hadhi kuwa kituo cha afya mwaka 2016 baada ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete kujenga majengo mapya ndani ya eneo la zahanati ya Msoga."alifafanua Luoga.


Nae kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2019, Mzee Mkongea Ali, alizindua mradi huo na kusema, serikali inaendelea kuboresha sekta ya afya ili kutoa huduma bora kwa jamii.


Wakati huo huo mwenge huo ulizindua mradi wa josho la mifugo na mradi wa uhifadhi wa chanzo cha maji (lambo), ambapo mke wa Rais mstaafu ambae pia ni mbunge wa kuteuliwa mama Salma Kikwete aliwataka wakulima na wafugaji kuwa kitu kimoja na kuepukana na migogoro baina yao.


Alisema ,washirikiane na kuheshimiana badala ya kuingiliana katika shughuli zao.Awali akipokea mwenge wa uhuru kutoka halmashauri ya Kibaha,mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Zainab Kawawa alisema ,mwenge huo umepitia miradi 15 yenye thamani ya zaidi ya sh.milioni 945.1.


Mwenge wa uhuru ulipokelewa mkoani Pwani Julai 24 na kukimbizwa kwenye wilaya saba ,halmashauri Tisa ambapo miradi 95 imepitiwa yenye thamani ya zaidi ya sh.bilioni 40.436.6:', kati ya miradi hiyo miradi 61 imekaguliwa,17 ilipaswa kuwekwa jiwe la msingi,9 kuzinduliwa na 8 kufunguliwa huku agost 2 ukitarajiwa kupokelewa mkoa wa Morogoro.