Friday, May 3, 2019

WANAWAKE BUSEGA WAKILI DR CHEGENI NI JEMBE.

Na Shushu Joel, Busega. 


WANAWAKE wa wilaya ya Busega mkoani Simiyu wamekili kuwa Mbunge wa jimbo hilo Dr Rafael Chegeni ni kiongozi mwenye maono ya mbele ikilinganishwa na watangulizi wake waliopita katika jimbo hilo. 


Ujumbe huo umetolewa jana na kina mama hao wakati walipokuwa wanakabidhiwa cherehani ambazo walimuomba Mbunge huyo ili waondokane na tabia ya kuomba omba fedha kutoka kwa waume zao huku nao wakiwa na fani zao. 


Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa cherehani hizo kina mama hao walisema kuwa Mbunge wao amewatoa katika hatua ya kuwa tegemezi na kujiona kama wamezaliwa upya. 


Akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa kina mama walionufaika na mradi huo Ng'washi Juma alisema kuwa msaada huo umefika wakati mwafaka kutokana na uhitaji wetu kina mama tuliokuwa tumeajiliwa na watu.


Aliongeza kuwa anatoa pongezi kwa Mbunge huyo kutokana na jitihada zake za kuwakomboa kinamama ambao ndio chachu kubwa ya maendeleo hapa nchini.


 "Dr Chegeni amekuwa kiongozi shupavu na mwenye kutambua mahitaji yetu kinamama kwani kipindi kirefu tulikuwa omba omba kutoka kwa waume zetu lakini kutokana na misaada aliyokuwa akitupatia manufaa makubwa "Alisema. 


Naye mkuu wa wilaya hiyo Tano Mwera amempongeza Mbunge huyo kwa kutambua thamani ya wanawake katika wilaya hiyo na hata kuwapatia vitendea kazi ili waweze kujitegemea pasipo kutegemea waume zao.


 Aidha alimtaka Dr chaegeni kuongeza juhudi hizo ili kuwasaidia wanawake wa wilaya hiyo kwa kuwapatia vitendea kazi zaidi na hata kufungua viwanda vya ushonaji. Kwa upande wake Mbunge wa jimbo hilo Dr Rafael Chegeni alisema kuwa msaada huo ni moja ya majukumu yake kwenye jimbo lake la Busega. 


Hivyo amewataka kinamama hao kuzitumia cherehani hizo kwa matumizi yaliyoyaomba ili kuwaletea mafanikio waliyokuwa wakiyasubili kwa muda mrefu. 


Aliongeza kuwa ameandaa mipango kabambe ya kuhakikisha anawakomboa watu wa jimbo hilo na si tu kina mama bali kwa watu wote ili kila mmoja awe na shughuli yake ya kumuingizia kipato. 


Aliongeza kuwa ametoa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya milioni 7 kwa kinamama wasiopungua 30 kwa lengo la kuwatoa kwenye dimbwi la umasikini.

WANAFUNZI 1,103 CHALINZE WARIPOTI SHULENI.

Image may contain: 3 people, people standing and outdoor
Na Omary Mngindo, Lugoba


HALMASHAURI ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, imepokea wanafunzi wote 1,103 waliokosa nafasi ya kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza, kutokana na upungufu wa vyumba 26 vya madarasa.


Idadi hiyo kubwa ya wanafunzi hao imetokana na ufaulu mzuri wa wanafunzi hao uliochangiwa na mkakati wa serikali kuhusu mpango wake wa elimu bure, unaolenga kuhakikisha watoto wote wanapata haki ya msingi ya kupata elimu.


Hayo yamebainishwa katika kikao cha Baraza la Madiwani robo ya kwanza kwa mwaka wa 2019, likiwa chini ya Mwenyekiti wake Said Zikatimu, Makamu Juma Mpwimbwi, Mkurugenzi Mtendaji Amina Kiwanuka na wataalamu mbalimbali ambalo limeelezwa kwamba vyumba 26 vimekamilika kwa sh. Mil. 522.


Zikatimu alianza kwa kuwapongeza madiwani kwa kukubali kuidhinisha kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya zoezi hilo, huku akishukuru ushirikiano mkubwa kutoka kwa wataalamu mbalimbali, sanjali na wananchi ambao wameungana katika kufanikisha ujenzi huo.


"Nianze kwa kuelezea furaha yetu ya kufanikisha ukamilishaji wa vyumba vyote 26 vya madarasa, zoezi ambalo tumelifanikisha kupitia vyanzo vyetu vya mapato ya ndani, wanafunzi wote 1,103 wameingia darasani wanaendelea na masomo yao," alisema Zikatimu. Wakichangia mada katika kikao hicho, diwani Hussein Hading'oka amelalamikia ubovu wa barabara katani kwake, hiku aksema wakati miundombinu hiyo ikisimamiwa naa halmashauri hali haikuwa hivyo.


"Katika vijiji vyangu kuna ubovu mkubwa wa barabara, tangu kuingia kwa utaratibu mpya wa barabara zetu kuwa chini ya TARURA kumekuwepo na matatizo makubwa, katika kipindi hiki hazipitiki kabisa," alisema Hading'oka.


Aidha halmashauri hiyo inenunua vifaa maalumu vya kupimia ardhi (GPS) vinavyolenga lupungiza kama so kumaliza kabisa malalamiko ya upimaji wa ardhi ambapo katika baraza lililopita diwani wa Kata ya Lugoba Rehema Mwene alilalamikia gharamaa ya upimaji wa shamba eka moja kwa sh. Milioni moja.


Katika baraza hilo Makamu Mwenyekiti Juma Mpwimbwi diwani wa Kata ya Miono, ameliomba baraza hilo kuandaa mafunzo kwa vijana juu ya matumizi ya vifaa hivyo, ili kuwarahisishia kazi hiyo wananchi na naofisa wanaohusika na idara hiyo.

BAGAMOYO WAZINDUA CHANJO YA KICHOCHO NA MINYOO.

Image may contain: 5 people, including Salvio Wikesi, people smiling, table
Idara ya Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, imeendesha zoezi maalum la utoaji dawa kinga kwa ajili ya kinga tiba ya kichocho na minyoo tumbo, kwa watoto wenye umri kati ya miaka 5 – 14.


Zoezi hilo limezinduliwa jana katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kizuiani iliyopo kata ya Kisutu, ambapo Mgeni rasmi Dkt. Salvio Wikesi aliyemwakilisha Mkuu ya Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainab Kawawa, amewatoa hofu Wananchi, hususani Wazazi juu ya utoaji wa dawa hizo, akisisitiza kwamba, dawa hizo ni kinga tiba na si chanjo kama inavyofahamika na wengi, na akaongeza kuwa dawa hizo ni salama na zimethibitishwa ubora wake na mamlaka zinazohuzika.


“Kumekuwa na dhana potofu kwenye jamii, kuwa dawa hizi si salama, hivyo wazazi kukataa watoto wao wasipewe dawa hizi na wakati mwingine kuwakataza watoto wasifike Shuleni siku ambazo dawa zinatolewa. 


Nachukua fursa hii kuwaondoa hofu wazazi na Wananchi wote kuwa dawa hizi ni salama na muhimu kwa watoto wetu na wawaruhusu watoto kupatiwa dawa kinga hizi, kwani magonjwa haya yasiyopewa kipaumbele ni hatari na yaweza hata kuhatarisha uhai wa mtoto anapochelewa kupatiwa matibabu yake” Amesema Dkt. Wikesi.


Nae Mratibu wa Kitengo cha Magonjwa yasiyopewa kipaumbele kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Ndg. Mohamed Farah amesema lengo la utoaji wa dawa kinga hizo Mashuleni ni kutoa kinga na tiba kwa magonjwa ya kichocho na minyoo tumbo kwa Watoto wote wenye umri wa miaka 05-14 waliopo Shuleni na nje ya Shule (nyumbani).


Akaongeza, kwa Mwaka 2018, zoezi hili la utoaji dawa kinga kwa watoto wenye umri wa miaka 05-14 lilifanikiwa kwa 90.2/% na kwa Mwaka huu wanatarajia kupata mafanikio zaidi kwani wamefanya uhamasishaji wa kutosha kwa jamii na kusisitiza kuwa kwa watoto ambao hawako Shuleni, wazazi wawapeleke watoto hao katika vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali ili kupatiwa dawa hizo.


Zoezi hili la utoaji dawa za Minyoo tumbo na Kichocho pia linaendelea katika Vituo vyote vya Afya, Zahanati na Hospitali ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.

imeandaliwa na Afisa habari Halmashauri ya Bagamoyo
Image may contain: 2 people, child

BILIONI 160 KUFIKISHA UMEME VIJIJINI.


Pichani Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akizingumza na walazi wa Kijiji cha Msigi (hawapo pichani) wakati Mgalu akiwa katika ziara kwenye Kata za Ubena, Talawanda na Kiwangwa kukagua vilundi vya Wajadiriamali waliopatiwa gedha kupitia halmashauri hiyo. Wanaoshuhudia ni Said Mwakapugi ofisa Maendeleo halmashauri hiyo, Jumanne Rajabu Mwenyekiti wa Kijiji na Said Zikatimu. 

Picha na Omary Mngindo.
  ...........................................................

Na Omary Mngindo, Chalinze

WIZARA ya Nishati imepatiwa kiasi cha shilingi bilioni 160 kwa ajili ya kufikisha umeme katika maeneo ambayo hayajafikiwa, kutokana na makosa ya upimaji wa umbali.


Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu ameyasema hayo jana akiwa katika ziara ya kukagua vikundi vilivyokopeshwa pesa za mapato ya ndani ya halmashauri ya Chalinze mkoani hapa, ambapo aliitumia siku ya wafanyakazi duniani Mei Mosi kutembelea Kata za Ubena, Talawanda na Kiwangwa. 


Akiwa katika vijiji vya Msigi, Talawanda, Magulumatali na Bago, Mgalu alipokea kilio hicho kutokana kwa wananchi kuhusu kutofikiwa na umeme, hali waliyoielezea inachangia kudumaza maendeleo ikiwemo shughuli za kiuchumi, ukizingatia umuhimu wa huduma hiyo.


Akizungumza na wananchi katika maeneo hayo akiambatana na Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Said Zikatimu, Mgalu alisema kwamba serikali baada ya kubaini mapungufu hayo ya kibinadamu, Rais Dkt. John Magufuli alisema hataki agombanishwe na wananchi, akawapa ridhaa ya kuomba fedha hazina kwa ajili ya kazi hiyo.


"Mapungufu yaliyojitokeza, nitolee mfano hapa Magulumatali, waliosimamia zoezia la upimaji kutokaea Chalinze wamesema kuna umbali wa kilometa 6 wakati uhalisia ni kilometa 10, pia katika maeneo mengine hivyohivyo, tukaandika ombi hazina tukapatiwa kiasi hicho," alisema Mgalu. 


Aliongeza kwamba zoezi la usambazaji umeme kwa mradi uliopo wa REA unaendea hivyo wananchi kwa sasa waendelee na uwekaji wa waya katika nyumba na kwamba umeme utawafikia kama ilivyodhamiliwa na serikali ya kuwafikishia huduma hiyo wananchi wote. 


Nao wakazi wa Kijiji cha Bago Kata ya Talawanda wamelalamikia kutounganishiwa umeme kwa muda mrefu, huku huduma hiyo ikiishia kwa majirani zao hali inayosababisha malalamiko mengi kutokana kwa wakazi hao. 


Kwa upande wake Diwani wa kata ya Talawanda ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Saidi Zikatimu alisema kwamba anaimani na kazi kubwa inayofamywa na Serikali kupitia Waziri Dkt. Medard Kalemani na Naibu wake Mgalu, kwa namna wanavyochapakazi, huku akiwaomba wakazi ndani ya halmashauri na jimbo zima la Chalinze waendelee na uwekaji wa miundombinu hiyo tayari kwa kupokea huduma hiyo.