Friday, March 1, 2019

DC KAWAWA AKABIDHI HUNDI YA MILIONI 338.3 KWA VIJANA NA WANAWAKE CHALINZE

Image may contain: 8 people, people smiling, people standing
  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mheshimwa Zainabu Kawawa, akiwa ameshika mfano wa hundi ya milioni 338.3 kwaajili ya vijana na wanawake Halmashauri ya Chalinze.

Image may contain: 7 people, people sitting
 Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mheshimwa Zainabu Kawawa, akizungumza na wana vikundi vilivyopata mikopo hiyo.
.....................................
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mheshimwa Zainabu Kawawa, amekabidhi hundi yenye thamani ya Fedha za kitanzania milioni 338.3 zilizotolewa na Halmashauri ya  Chalinze kwa vikundi 64 vya Vijana na wanawake kwa robo ya pili ya mwaka wa Fedha wa 2018/2019.


Fedha hizo ni asilimia 10 ya Mapato ya ndani yanayo kusanywa na halmashauri hiyo 


Makabidhiano hayo yamefanyika jana katika uwanja wa polisi Chalinze ambapo Mkuu huyo wa Wilaya katika hotuba yake ya kukabidhi hundi aliupongeza uongozi wa halmashauri ya Chalinze kwa kuheshimu na kutii maelekezo ya serikali kwa kutenga asilimia 10 ya Mapato ya ndani na kuwakopesha wanawake, vijana na walemavu.


Hata hivyo Kawawa alihimiza ukusanyaji wa Mapato ya halmashauri kwa kuwataka wananchi na wataalamu kuziba mianya yote inayoweza kusababisha upotevu wa Mapato na kusababisha miradi mbalimbali ya maendeleo kutotekelezeka hivyo kukwamisha utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi. 


"Mikopo hii ya wanawake na Vijana itatekelezeka kwa sababu ya juhudi ya ukusanyaji wa Mapato inayoendelea, ndiyo maana miradi yetu katika maeneo mbalimbali inaendelea kutekelezwa. "Kawawa alisema.


Akitoa ufafanuzi wa taarifa hiyo katika hafla ya ugawaji hundi kwa wanawake na Vijana, Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chalinze Bwana Shabani Millao alieleza kuwa robo ya pili ya mwaka wa Fedha 2018/2019 halmashauri hiyo imetoa kiasi cha shilingi milioni 338.3.


Alisema fedha hizo zimetolewa ili kutekeleza bajeti na maagizo ya serikali ya kuwakwamua vijana na wanawake katika lindi la umasikini wa kipato kwa kuwakopesha asilimia kumi ya makusanyo ya Mapato ya ndani ya halmashauri.


Aidha Millao alieleza kuwa mpaka sasa takribani miaka mitatu tangu ianzishwe halmashauri ya Chalinze imekwisha toa mikopo kwa wanawake na Vijana jumla ya Fedha za kitanzania milioni 967 kwa vikundi 257.


 Aliongeza kuwa, hali hiyo inawawezesha Vijana na wanawake kujiajiri wenyewe kutokana na shughuli za ujasiriamali wanazozifanya kutokana na mikopo hiyo.


"Halmashauri ya Chalinze mpaka sasa haina deni lolote kwa upande wa Asilimia 10 ya Mapato ya ndani yanayo takiwa kupelekwa kwa wanawake na Vijana tunatekeleza kwa kadiri tunavyokusanya na kuisimamia bajeti kwa mujibu wa sheria." Millao alisema.


Kwa upande wake Afisa maendeleo ya Jamii anayeratibu vikundi Bi Wahda Mwishehe aliwataka wanawake na Vijana kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali ili waweze kukopesheka kwa urahisi na kuwataka warejeshe mikopo kwa wakati ili mikopo hiyo waweze kukopeshwa na wengine.


 “ Akinamama wenzangu tuweni waaminifu kwa kurejesha mikopo mliyochukua kwa wakati kwani mambo yamekuwa rahisi kwa sasa kwani serikali imeondoa riba kwa wanawake na Vijana wanapokopeshwa na halmashauri, Mwishehe alifafanua.


Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Mhe Saidi Zikatimu alieleza kwa kina mafanikio ya halmashauri yake katika ukopeshaji fedha kwa vikundi vya wanawake na Vijana kwa kusema kuwa kwa halmashauri ya Chalinze kutoa mikopo siyo tatizo bali wanawake na Vijana kutounda vikundi kwa wakati ili kupatiwa mikopo hiyo.


Zikatimu alitoa rai kwa maafisa maendeleo wa halmashauri kuwafikia wanawake na Vijana katika vijiji vyao na kuwapa Elimu ya namna ya kujiunga katika vikundi na kuwaelewesha mchakato mzima wa namna ya kupata mikopo,


"Fedha tunazo tunahitaji Vijana na wanawake wajitokeze kuomba mikopo na mikopo hii haina riba kiasi cha Fedha atakachokopeshwa mlengwa ndicho atakachorudisha“. Zikatimu alieleza.
Image may contain: 19 people, people smiling, outdoor

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mheshimwa Zainabu Kawawa akiwakabidhi wawakilishi wa vikundi katika halmashauri ya Chalinze hundi hundi ya milioni 338.3.

MAGAZETI YA LEO MACHI 1, 2019.

Thursday, February 28, 2019

WANAOINGIZA MABINTI WA SHULE GESTI SASA KUKIONA...TGNP YAOMBA MSAADA KWA...

Waziri Kamwelwe asifu utendaji kazi wa Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania




Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi. Isack Kamwele amepongeza utendaji kazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA). Mhe. Kamwele alitoa pongezi hizo wakati alipotembelea Ofisi za TMA, Ubungo Plaza, Dar es Salaam, tarehe 27 Februari 2019 na alipata taarifa ya utendaji kazi wa mamlaka na kutembelea baadhi ya sehemu za kazi kabla ya kuzungumza na wafanyakazi. Mhe. Kamwele alipokelewa na uongozi na menejiment ya TMA, ikiongonzwa na mwenyekiti wa bodi ya ushauri Dkt. Buruhani Nyenzi na kaimu mkurugenzi mkuu Dkt. Ladislaus Chang’a. Kat

“Nawapongeza TMA kwa umakini na utekelezaji wa majukumu yenu, nakiri kusema ni moja ya taasisi makini kati ya taasisi zilizo chini ya wizara yangu nilizo tembelea”. Alizungumza mhe. Kamwele

Aidha, mhe. Kamwele alisisitiza kuboresha mfumo wa ushirikishwaji wa wadau na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa, akitolea mfano mafuriko yaliyo bomoa barabara eneo la Dumila, kuwa baada ya kufuatilia taarifa za hali ya hewa waligundua TMA ilitoa taarifa hizo siku mbili kabla ya tukio na kuonesha rangi nyekundu yenye kumaanisha tahadhari kwa maeneo ya Kilindi lakini taarifa hiyo haikuwafikia walengwa.

Mhe. Kamwele alimalizia kwa kuahidi kutatua changamoto zinazoikabili TMA zikiwemo uhitaji wa ongezeko la vituo vya hali ya hewa, mitambo ya hali ya hewa, kupatikana kwa jengo la kituo kikuu cha utabiri n.k

Akitoa salamu za shukrani kwa upande wa TMA, mkurugenzi wa ofisi ya TMA Zanzibar, Bw. Mohamed Ngwali alimshukuru mhe. Waziri kwa pongezi sambamba na kutembelea na kuona shughuli zinazofanywa na TMA, na kuahidi kufanyia kazi maelekezo yote aliyoyatoa .

Imetolewa:

Ofisi ya Uhusiano

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)

DC BAGAMOYO ATAKA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA WOTE KURIPOTI SHULE IFIKAPO JUMATATU MACH 04.

Image may contain: one or more people, people standing and outdoor
 Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa,  akishiriki ujenzi wa vymba vya madarasa shule ya sekondari Pera Halmashauri ya Chalinze, aliyesimama kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Saidi Zikatimu.
............................

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawaamewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka shule watoto wote waliofaulu kuingia kidato cha kwanza ifikapo jumatatu ya tarehe 04 Mach 2019.


Mkuu huyo wa wilaya ametoa tamko hilo wakati akizungumza na viongozi wa kata na tarafa katika Halmashauri ya Chalinze na kuwataka viongozi hao wasimamie maagizo hayo.


Tamko hilo limekuja baada ya shughuli za ujenzi wa vyumba vya madarasa zikiendelea wilaya yote ya Bagamoyo lengo likiwa ni kuhakikisha hakuna mwanafunzi atakaekosa masomo kwasababu ya upungufu wa vyumba vya madarasa.


Katika ziara yake hiyo ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa, Mkuu huyo wa wilaya ameshiriki shughuli za ujenzi katika shule ya Sekondari Pera kata ya Pera Halmashauri ya Chalinze ambapo ujenzi wake unaendelea.


Wakati hyuo huo Mkuu huyo wa wilaya Zainabu Kawawa amesema kila mzazi anapaswa kusaini mkataba maalum wa kuthibitisha kuwa mtoto wake atasoma kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne bila ya kukosa.


Katika zoezi hilo la kusaini mikataba amewaagiza maafisa tarafa kusimamia na mzazi au mlezi atakaekwenda kinyume atachukuliwa hatua za kisheria.
Image may contain: 15 people, people smiling, people standing 
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa kata na tarafa na wanachi wanaoshiriki ujenzi wa shule ya sekondari Pera Halmashauri ya Chalinze, kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Saidi Zikatimu.
  

NAPE APONGEZA KUWASHWA UMEME KIJIJI CHA TULIENI, LINDI.

NA HADIJA HASSAN, LINDI.

Kuzinduliwa kwa Umeme , kupitia mradi wa Umeme Vijijini (REA) katika Kijiji cha Tulieni kata ya Mtua Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Mkoani humo kunaweza kuwa Mwarobaini wa kumaliza changamoto ya upatikanaji wa Maji  inayowakabili wananchi kijijini hapo

Hayo yameelezwa na Mbunge Jimbo la Mtama Nape Nnauye wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa uwashaji wa umeme katika kata hiyo uliofanyika jana katika ofisi za  kijiji cha  Tulieni  na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu

Akizungumza kwa niaba ya Wananchi wa Kijiji hicho Nape alisema kuwa kutokana na Kijiji  kuwa mlimani wakazi wa maeneo hayo hulazimika kushuka chini (mabondeni) kufuata huduma ya Maji katika mifereji na mito ambayo hata hivyo sio salama kwa afya zao

" Wakati wa Kampeni za uchaguzi mwaka 2015 kijiji hiki kilikuwa na Matatizo Makubwa mawili , moja bara bara ambalo limeshaanza kufanyiwa kazi na wakala wa bara bara mijini na vijijini (TARURA ) kwa kujenga barabra hiyo kwa kiwango cha lami lakini la pili uliposikia akina mama hawa wanapiga Vigere gere hapa tunatatizo kubwa la maji "Alisema Nape

"kutokana na Kijiji hiko kuwa  Mlimani  dawa pekee ya kuyaleta maji huku juu ilikuwa ni Umeme ndio maana tukasema tuanze na Umeme  alafu tuyavute maji kutoka  chini kuyaleta huku juu na awa akina mama waone wako Tanzania mzuri kwa kufungua maji kwenye mabomba" aliongeza Nape

Nape alifafanua kuwa uwekwaji wa umeme katika kijijini hapo kwa kiasi kikubwa utaleta chachu ya kuanzisha mchakato wa kutatua kero ya Upatikanaji wa maji

Akizungumza na Wananchi hao  Naibu Waziri Subira Mgalu  aliwaondoa wasiwasi wanakijiji hao juu ya Upatikanaji wa Maji kwani Serikali ilishaagiza kuzipa kipaumbele Taasisi muhimu kuunganisha umeme  katika maeneo yaliyopitiwa na Miradi ya Umeme Vijijini (REA) kama vile shule, Zahanati , miradi ya maji na Taasisi zingine kama hizo

Hata hivyo Mgalu alimuagiza Meneja wa Shirika la Umeme (TANESCO) Mkoa wa Lindi Mhandisi Felisian Makota Kufikisha Umeme huo mara moja katika chanzo cha Maji Kijijini hapo pindibMchakato huo utakapoanza

Akisoma Taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa usambazaji Umeme Vijijini REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza Meneja wa TANESCO Mkoa wa Lindi Mhandisi Felisian Makota alisema kuwa katika kutekeleza mradihuo kijiji cha Tulieni kimepangiwa kuwa na Wigo wa Msongo wa Umeme K .W  33 ambapo kazi hiyo imekamilika, ujenzi wa Line ndogo kilo mita 2 ambayo mpaka sasa tayari  mkandarasi amejenga kilomita 0.6  pamoja na mashine umba moja ambapo wateja wa awali wanataraji kuwa 14
 Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu (kati kati) na Mbunge Jimbo la Mtama Nape Nnauye (kushoto)
 
Wananchi wa Kijiji cha Tulieni kata ya Mtua Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Mkoani Lindi wakimsikiliza Naibu waziri wa Nishati wakati wa uzinduzi wa kuwasha umeme katika kijiji hicho.