Wednesday, February 6, 2019

RAIS MAGUFULI AZINDUA MAHAKAMA INAYOTEMBEA.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuzindua rasmi gari maalumu litakalotumika kama Mahakama inayotembea  akiwa na  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, , Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Sophia Mjema wakati wa   maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya gari maalumu litakalotumika kama Mahakama inayotembea  baada ya kuizindua rasmi akiwa na  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi, Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Mbarouk Salum Mbarouk, Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird, wakati wa   maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019. Anayetoa maelekezo ni Mkuu wa Kitengo cha TEHEMA wa Mahakama ya Tanzania Bw. Enock Kalege na Kulia kabisa ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri Mahakama ya Tanzania Mhe. Eva Nkya.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitelemka kutoka kwenye gari maalumu litakalotumika kama Mahakama inayotembea baada ya kulizindua rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma wakati alipowasili kuhudhuria  maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia  kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza  Mkuu wa Kitengo cha TEHEMA wa Mahakama ya Tanzania Bw. Enock Kalegebaada ya kuzindua rasmi Mfumo wa Kielektroniki wa Kuratibu Mashauri (DSDS ll)  wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Majaji Wakuu Wastaafu Mhe. Augustino ramadhani na Mhe. Mohamed Chande Othmana kabla ya kupiga nao picha ya kumbukumbu kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Spika Job Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi na Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Mbarouk Salum Mbarouk  baada ya kuhudhuria   kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019.

PICHA NA IKULU


TAASISI YA IFAKARA YAPONGEZWA KWA UTAFITI.


Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa afya ifakara (ihi) Dkt. Honorati Masanja akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo.
 

Mkurugenzi wa huduma za afya ustawi wa jamii na lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Ntuli Kapologwe 
...................................................
 
Wataalamu wanaofanya tafiti za magonjwa mbalimbali hapa nchini wametakiwa kulenga mahitaji ya watekelezaji ili tafiti hizo zifanye kazi na kuleta mabadiliko yanayokusudiwa.


Akizungumza katika Mkutano  uliowajumuisha watafiti wa magonjwa mbalimbali uliofanyika mjini Bagamoyo leo February 06, 2019, Mkurugenzi wa huduma za afya ustawi wa jamii na lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Ntuli Kapologwe amesema changamoto iliyopo katika maswala ya utafiti ni kufanyika kwa tafiti bila ya kufanyiwa kazi.


Alisema, watafiti sasa wanapaswa kwenda sambamba na mahitaji ya watekelezaji ambao ni serikali.


Alisema changamoto iliyojitokeza kwa miaka kadhaa huko nyuma ni watafiti kufanya utafiti kisha tafiti hizo kutofanyiwa kazi kutokana na sababu mbalimbali.


Aidha, Dkt. Kapologwe ameipongeza Taasisi ya utafiti wa Afya ya Ifakara (ihi) kwani imekuwa ikihakikisha, tafiti inazofanya ni zile ambazo zenye uhitaji kwa mujibu wa mpango mkakati wa Ofisi ya Rais TAMISEMI ambayo ndiyo wizara inayohusika na utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya serikali.


Alisema uwepo wa Taasisi ya ifakara hapa ncini ni kiungo muhimu kati ya serikali na watafiti kutoka sehemu mbalimbali kwani maamuzi yanayofanywa na serikali hutegemea tafiti za kitaalamu kama zinazofanywa na Taasisi ya ifakara.


Aliongeza kuwa, kwa mwaka huu wa 2019 Ofisi Rais TAMISEMI itawasilisha maeneo ambayo yamekuwa na changamoto katika kutolea maamuzi mbalimbali kutokana na kukosekana na takwimu za kitafiti.


Alisema kwa sasa duniani huwezi kufanya maamuzi yoyote bila ya kuwa na matokeo ya kitafiti, hivyo jopo la watafiti ni sehemu muhimu sana katika kutekeleza mikakati mbalimbali ya serikali kwa kutokomeza magonjwa ndani ya jamii.


Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa afya ifakara (ihi) Dkt. Honorati Masanja amesema kituo cha utafiti cha ifakara (ihi) kimeweza kufanikiwa katika tafiti zake ambapo hivi karibuni imefanya utafiti wa chanjo ya Malaria na huenda ikawa ni chanjo ya kwanza kutolewa katika mfumo wa huduma za afya.


Alisema utafiti huo wa chanjo ya Malaria umefanyika kwenye kituo kilichopo Kingani Bagamoyo ambapo Taasisi ya ifakara ilikuwa ni miongoni mwa Taasisi 11 zilizofanya utafiti huo ambao umeonyesha mafanikio makubwa.


Aliongeza kwa kusema kuwa, kufuatia utafiti huo ulifanyika Bagamoyo, Shirika la Afya Duniani (WHO) limapanua wigo na kufanya utafiti huo kwenye  watu wengi zaidi ambapo nchi tatu zinashiriki kufanya utafit huo ambazo ni Ghana, Malawi na kenya.


Dkt. Masanja alisema utafiti huo umezaa matunda na baada ya kukamilika kwa utafiti unaosimamiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) huenda ikawa ni chanjo ya kwanza itakayotumika kwenye mfumo wa kawaida wa utoaji wa huduma za Afya.


Dkt. Masanja ameongeza kwa kusema kuwa, baadhi ya magonjwa yanajitokeza kutokana na mabadiliko ya tabia nchi hivyo kazi ya watafiti ni kutoa taarifa mapema ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi katika magonjwa.


Alisema katika kufanya utafiti pia wataalamu hao wanafanya utafiti wa magonjwa yenye uhusiano wa binadamu na wanyama kutokana na baadhi ya watu kuishi karibu na mbuga za wanyama hivyo ipo hatari ya magonjwa ya wanyama kuingia kwa binadamu.


Mkutano wa kwanza wa mwaka ambao ambao umewakutanisha wanasayansi wa Taasisi ya utafiti wa Afya ya ifakara (ihi) umefanyika mjini Bagamoyo lengo likiwa ni kupitia mambo mbalimbali ya kiutafiti yaliyofanyika katika kipindi cha mwaka 2018.


Mkutano huo umehudhuriwa na wadau mbalimbali katika sekta ya Afya wakiwemo wataalamu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Tume ya Sayansi na Teknolojia, Taasisi ya TPRA Arusha, Taasisi ya utafiti ya NIMRI, na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Muhimbili.

 Washiriki wa Mkutano huo wakiendelea na majadiliano. 

Washiriki wa Mkutano huo wakiendelea na majadiliano.

WANANCHI CHANGIENI SHUGHULI ZA MAENDELEO - RC NDIKILO

Image may contain: 5 people, people standing and outdoor
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Eng. Evarist Ndikilo amefanya ziara maalum ya kutembelea, kukagua na kuhimiza Wananchi kushiriki shughuli za maendeleo hususani kuchangia ujenzi wa madarasa ya Shule za Sekondari.



Ziara hiyo ya siku moja iliyoanzia katika Kata ya Mapinga ambapo Mkuu wa Mkoa alipokelewa na Mwenyeji wake, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainab Kawawa, ilikua na lengo la kuhamasisha Wananchi kushiriki kikamilifu kuchangia ujenzi wa madarasa katika Shule za Sekondari za Kata, Wilayani Bagamoyo, ili wanafunzi waliochaguliwa awamu ya pili kujiunga na elimu ya Sekondari kuhakikishiwa nafasi ya kujiunga na elimu hiyo.
 
Akizungumza na Wananchi katika Mkutano maalum wa majumuisho ya Ziara hiyo uliofanyika katika Kijiji cha Kongo, kilichopo Kata ya Yombo Wilayani hapa, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Eng. Evarist Ndikilo amewaasa Wananchi kuacha kuisusia Serikali kujenga miundombinu ya elimu kwa kisingizio cha elimu bure.
 
Akifafanua Mhe. Eng. Ndikilo amesema kuwa dhana ya elimu bila malipo haimaanishi Wazazi kutochangia kabisa gharama za elimu, bali Serikali inampunguzia mzazi gharama hizo kwa kumlipia mwanafunzi ada, chakula kwa wanafunzi wa bweni pamoja na gharama zingine za uendeshaji wa Shule lakini ujenzi wa miundombinu kama madarasa na madawati ni wajibu wa kila Mwananchi kuchangia ili wanafunzi wapate mahala pa kujifunzia na pale Wananchi wanapofanya vizuri katika ujenzi wa miundombinu, basi Serikali huunga mkono juhudi hizo za Wananchi.
 
“Nawaagiza Wakuu wote wa Wilaya za Mkoa wa Pwani na Wakurugenzi wote wa Halmashauri wahakikishe Wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na elimu ya Sekondari wanapata nafasi hiyo, hususani wale waliochaguliwa awamu ya pili, fanyeni jitihada za makusudi kukamilisha vyumba vya madarasa vinavyoendelea kujengwa sasa ili Wanafunzi hao wapate nafasi ya kuendelea na elimu ya Sekondari” Amesema Ndikilo.
 
Nae Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainab Kawawa akitoa takwimu za ufaulu wa kidato cha kwanza kiwilaya, amesema jumla ya Wanafunzi 1869 walichaguliwa kujiunga na elimu ya Sekondari kwa Mwaka 2019 katika awamu ya kwanza, na awamu ya pili jumla ya Wanafunzi 482 wamechaguliwa huku Wilaya ya Bagamoyo ikiwa na upungufu wa vyumba 32 vya madarasa hadi sasa.
 
Pamoja na uhamasishaji huo wa Wananchi kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa, Mkuu wa Mkoa pia ametumia Ziara hiyo kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo ya Sekta ya miundo mbinu ya barabara, Afya na shughuli za wanufaika wa TASAF, ambapo amekagua ujenzi wa mfereji wenye ukubwa wa mita 500, mradi uliotekelezwa na wakala wa barabara vijijini (TARURA) katika Kata ya Dunda, Ujenzi wa Kituo cha Afya Matimbwa, Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Mapinga katika Kata ya Mapinga na Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na Ofisi moja ya Walimu katika Shule ya Sekondari Hassanal Damji, iliyopo Kata ya Magomeni.