Tuesday, January 22, 2019

CCM PANGANI YAMTUNUKU TUZO YA SHUKRANI RAIS DKT MAGUFULI KWA UAMUZI WAKE WA KURIDHIA KUTIA SAINI UJENZI WA BARABARA YA TANGA-,PANGANI HADI BAGAMOYO

Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Pangani Hamis
Mnegero katikati akimkabidhi tuzo  ya shukrani ya  Rais John
Magufuli ,Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo kutokana na
uwamuzi wake wa kuridhia na kutia saini kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani hadi Bagamayo hivi karibuni kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu
Abdallah.

Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Pangani Hamis
Mnegero akizungumza na waandishi wa habari hatua yao ya kumtunuku tunzo ya shukrani Rais John Magufuli kutokana na uamuzi wake wa kuridhia na kutia saini kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani hadi Bagamayo hivi karibuni kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT Taifa Jesca Mbogo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa

......................................

CHAMA Cha Mapinduzi wilaya ya Pangani kimemtunuku tunzo ya shukrani Rais John Magufuli kutokana na uwamuzi wake wa kuridhia na kutia saini kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Tanga Pangani hadi Bagamayo hivi karibuni . 


Akikabidhi tunzo hiyo hapo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya wa Umoja wa wanawake wa chama hicho UWT Taifa Jesca Mbogo wakati akiwa katikaziara ya kukagua shughuli za maendeleo wilayani humo

 
Mwenyekiti CCM wilayani humo Hamis Mnegero alisema kuwa wameamua kutoa tunzo hiyo kama sehemu ya kurudisha shukrani kwa Rais Magufuli kutoka na kufanikiwa kutekeleza ndoto ya siku nyingi ya kuwa na barabara ya kiwango cha lami wilayani humo.


“Tunajua kuna juhudi kubwa ambazo zilikuwa zimechukuliwa na marais
waliotangulia lakini ndoto hizo hazikuweza kutimia lakini kwa juhudi
kubwa za Rais wa awamu ya tani tumeona ujenzi huo sasa unakwenda
kufanyika”alisema Mnegero.


Alisema kuwa barabara hiyo ilikuwa ni kilio cha muda mrefu kwa
wananchi wa wilaya hivyo anaamini kwa kuanza kwa ujenzi huo kutaweza kufufua matumaini mapya kwa wilaya hiyo.


Kwa upande wake Naibu Katibu mbogo alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inajitahidi kuboresha mazingira bora katika sekta mbalimbali ili
kuhakikisha kila mtanzania anapata fursa ya kupata maendeleo na unafuu wa maisha.


“Kama mnavyoona utekelezaji wa sera ya elimu bure pamoja na
uboreshwaji wa huduma za afya hii yote ni kuhakikisha mtoto wa
kitanzania anakuwa na afya bora lakini anapata fursa ya elimu
bora”alisema Naibu Katibu huyo. Naibu Katibu Mkuu Mbogo yupo mkoani Tanga kwa ziara ya siku tatu kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali pamoja na kuzungumza na wanachama wa UWT mkoani hapa


Monday, January 21, 2019

TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE YAWA YA KWANZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KUWA NA WODI YA WATOTO WENYE MAGONJWA YA MOYO

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wadau wa taasisi ya Baps Charity  baada ya kufanya ziara katika taasisi hiyo na kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto jana katika taasisi hiyo Jinini Dar es Salaam. Wodi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza baada ya kufanya ziara fupi ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi mpya ya watoto wenye magonjwa ya moyo jana katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuregenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi na kushoto ni Meneja wa Jengo la taasisi hiyo Bi. Flora Kassembe. Wodi hiyo inatarajiwa kuwa wodi ya kwanza kwa watoto wenye magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na kati.
..................................

Na: Genofeva Matemu – JKCI

Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete (JKCI) imekuwa   taasisi ya kwanza Afrika Mashariki na Kati kuwa na wodi pekee ya kuwahudumia watoto wenye magonjwa ya moyo bila kuwachanganya na watu wazima.

Eneo la wodi hiyo lilitolewa mwaka 2017 wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Magufuli alipokua akizindua Hospitali ya Mloganzila na kuiagiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutoa sehemu ya jengo linalohudumia watoto kwa JKCI ili watoto wenye magonjwa ya moyo waweze kuwa na wodi yao katika kuleta ufanisi wa matibabu ya moyo kwa watoto hapa nchini.


Akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi hiyo Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamaii, Jinsi, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alisema upatikanaji wa wodi hiyo ni juhudi za serikali katika kuhakikisha utolewaji wa matibabu ya moyo kwa watoto ya kibingwa yanaendelea kuboreshwa hapa nchini.


“Kwa wodi za watoto wenye magonjwa ya moyo peke yake kwa hapa Afrika Mashariki na kati hii ndio itakua wodi ya kwanza inayowahudumia watoto bila kuwachanganya na watu wazima na hii italeta ufanisi zaidi kwani nafasi ya kufanya makosa haitakuwepo kwasababu kutakuwa na wataalamu wanaohudumia watoto tu” alisema Waziri Ummy


Waziri Ummy, alisema  wodi hiyo ambayo ukarabati wake umekamilika inatarajiwa kuwa  na vitanda 32 na chumba cha uangalizi maalum (ICU) kitakachokuwa na vitanda 15 jambo ambalo litasaidia kuwafanyia upasuaji watoto wengi zaidi waliopo katika foleni ya upasuaji na kuokoa maisha yao.


“Serikali ilitoa milioni 700 kwa ajili ya ukarabati wa wodi hii na sasa kwa mara nyingine tena serikali imetoa milioni 500 kukamilisha miundombinu ya ukarabati wa wodi hii. Nawashukuru sana taasisi ya Baps Charity ambao nao wamewekeza  milioni 800 katika kuhakikisha kuwa wodi hii inakarabatiwa, serikali tutazidi kuunga mkono juhudi hizi ”  alisema Waziri Ummy.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prf. Mohamed, Janabi alisema kwa shifti mbili za kliniki ya watoto zilizopo JKCI inaona wagonjwa wa moyo hadi sitini kwa siku thelathini wakiwa ni watoto, hivyo kulikuwa na umuhimu wa kuongeza wodi hiyo ya watoto.


Akizungumzia upasuaji wa magonjwa ya moyo prof. Janabi amesema kuwa jumla ya wangonjwa 1356 wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua kwa mwaka 2018, hii kwa mwaka jana ukiondoa Afrika kusini JKCI ndio hospitali iliyofanya upasuaji kwa wangonjwa wa moyo wengi zaidi kuliko nchi yoyote ya Afrika.


“Wodi hii mpya ni kwaajili ya watoto chini ya miaka 13 pekee na hii itatufanya kuwa taasisi ya kwanza Afrika Mashariki na kati kuwa na jengo lenye kuhudumia watoto bila kuwanchanganya na watu wazima “alisema prof. Janabi

TAKUKURU LINDI YAWATAKA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO.

Na Hadija Hassan, Lindi

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rusha (TAKUKURU) Mkoa wa Lindi imesema imekuwa ikipata wakati mgumu katika kupata ushahidi wa matukio ya Rushwa hali inayopelekea kushindwa kwenye baadhi ya mashauri ya Rushwa yanayofikishwa Mahakamani

Hayo yamesemwa na kaimu kamanda wa Takukuru Mkoa wa Lindi, Naibu Mkuu wa Takukuru Noel Mseo alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita ofisini kwake kwa lengo la kutoa Taarifa  ya utendaji kazi kwa kipindi cha mwezi Oktoba-Disemba mwaka 2018

Mseo alisema katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita Taasisi hiyo imeweza kupokea malalamiko 52 kati ya hayo 27  yalikuwa yanahusu vitendo vya Rushwa huku taarifa 25 zikihusisha mamlaka zingine
"katika kipindi hiko pia  majarada 3 yalipelekwa makao makuu kwa ajili ya kuombewa  kibali cha Mkurugenzi wa mashitaka(DPP) kuwafikisha watuhumiwa Mahakamani ambapo mpaka sasa jalada moja limesharudi tayari kwa watuhumiwa hao kuwafikisha mahakamani" alisema Mseo

Alisema  kwa kipindi cha mwezi oktoba  hadi Disemba 2018 Taasisi hiyo  imeshinda kesi tatu(3) na kushindwa kesi (2) na kesi 16zikiwa zinaendelea katika Mahakama  mbalimbali za Mkoa na Wilaya

Hata hivyo Mseo alieleza sababu zilizochangia kushindwa kwa baadhi ya kesi ni kutokana na Baadhi ya mashahidi  kutokutoa ushahidi madhubuti kwa watu wanaowafahamu na kuishinao,  pamoja na kuwepo na muingiliano wa Kesi za Rushwa na Kesi zingine kutoka vyombo vingine vya dola, hivyo kufanya kesi kuchukua muda mrefu na kusababisha gharama za kesi kuwa kubwa.

Pamoja na mambo mengine Mseo alitumia fulsa hiyo kuwahasa wananchiwa wa Mkoa huo kuacha maramoja vitendo vinavyojihusisha na Rushwa pamoja na kuwaomba kuendelea kuwaunga mkono kwa kutoa taarifa za vitendo vya Rushwa kwa kutumia namba113 kwa kuwa mapambao dhidi ya Rushwa sio ya Takukuru Peke yake bali ni ya jamii mzima.