Monday, November 5, 2018

PWANI YATILIANA SAINI MKATABA WA USAMBAZAJI DAWA ,VIFAA TIBA KUPITIA MSHITIRI MMOJA

Katibu tawala wa mkoa wa Pwani Theresia Mbando (wa pili kulia ) na mkurugenzi wa Astra Pharmacy Ranjiy Jha(wa kwanza kushoto ) wakitia saini mkataba wa usambazaji wa dawa ,vifaa tiba na vitendanishi kwa kupitia mfumo wa mshitiri mmoja (prime vendor system),wa kwanza kulia ni mfamasia wa mkoa Elias Mabonesho
.....................................

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

MKOA wa Pwani,umefikia asilimia 90 ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ,hadi kufikia octoba 2018, hatua ambayo inaelekea kwenda kupunguza kero ya upungufu wa dawa na vifaa hivyo kwenye vituo vya afya.

Hayo yalibainika ,wakati wa kikao cha mkoa cha zoezi la kusaini mkataba wa usambazaji wa dawa ,vifaa tiba na vitendanishi kupitia mfumo wa mshitiri mmoja (prime vendor system),zoezi ambalo limefanywa baina ya katibu tawala wa mkoa Theresia Mbando na mkurugenzi wa Astra Pharmacy Ranjiy Jha.

“Kwa mujibu wa taarifa zinavyotolewa katika mfumo wa kukusanya na kuchambua data za afya (DHIS 2 ),hadi kufikia kipindi hicho wamefikia asilimia hiyo jambo ambalo limenifurahisha” alisema Theresia .

Theresia alisema ,kwa hatua waliyofikia mzabuni huyo anatarajiwa atafikisha lengo la upatikanaji wa dawa kwenye vituo na halmashauri za mkoa kwa asilimia 100.

“Wananchi wamekuwa wakilalamikia juu ya upungufu wa dawa na vifaa tiba katika vituo vyetu hivyo ni imani yangu kwa hatua hii ,itakuwa muarobaini wa malalamiko hayo “

Aidha alisema,  kumekuwa na wastani wa utimilizaji wa oda kwa kiwango ambacho ni cha kubadilika badilika kutoka bohari ya madawa (MSD).

“Kufuatia uwepo wa mshitiri huyu naamini kwa bidhaa ambazo hazijatimia utimilifu kama ziliombwa bohari ya madawa zitajaziwa na mshitiri na hilo ndilo lengo kuu “alifafanua Theresia .

Kwa mujibu wa Theresia, baada ya kusaini mkataba huo halmashauri hazitakiwi kutumia wazabuni wengine na badala yake zitatakiwa kununua kwa mzabuni aliyepatikana kisheria kupitia mchakato uliofanywa na OR-TAMISEMI mwaka 2017.

Nae mfamasia wa mkoa wa Pwani Elias Mabonesho ,alielezea mfumo huo ulianzia Dodoma kama majaribio na kwasasa uko katika mikoa ya Morogoro ,Shinyanga na sasa Pwani .

Anasema ,mfumo utasimamiwa na ofisi ya katibu tawala wa mkoa kupitia ofisi ya uratibu wa mfumo wa mshitiri mmoja chini ya Mganga mkuu wa mkoa akisaidiwa na mfamasia ambae ndie mratibu huu .

Kwa upande wa wakurugenzi na waganga wakuu wa wilaya ,akiwemo mkurugenzi wa Mafia ,Erick Mapunda alisema ,kwa mfumo wa Jazia tatizo la ukosefu wa dawa linakwenda kuwa historia

CDF- WANAUME MNAWAJIBU WA KUMTETEA MTOTO WA KIKE.

Afisa Ushirikishaji Wanaume wa Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) Bw. Kiswigo Ibrahim Mwan`gonda akiongea na washiriki  kuhusu dhumuni la kongamano hilo mapema jana jijini Dar es salaam.
 

Na Selemani Beta.
Imeelezwa kuwa wanaume wanawajibu wakumtetea mtoto wa kike dhidi ya vitendo vya kikatili vina mzunguka, hiyo ni kutokana na ukweli kuwa wana uwezo wa kukataa vitendo hivyo kwakupaza sauti zao lakini pia kukataa kutoa ruhusa kwawamama wanaojishughulisha navitendo vyakikatili.

Akizungumza katika bonanza maalum la michezo lenye dhamira yakutoa elimu kwa wanaume, Afisa Ushirikishaji Wanaume wa Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) Bw. Kiswigo Ibrahim Mwang'onda amesema wanaume wakiamua wanaweza.

Bw. Mwang’onda amesema kwamuda mrefu mapambano yakumtetea mtoto wa kike dhidi ya ukatili vilikuwa vinahusisha wanawake wenyewe sasa wameamua kutoa elimu hiyo kwa wanaume ili nao waweze kusaidia kumlinda mtoto wa kike.

Lengo la bonanza hili ni kuwakutanisha na kuwaunganisha wanaume kupitia michezo na kuwahakikisha wanaume wanapata ujumbe kuwa wao wanajukumu kubwa la kuhakikisha wanalinda na kuthamini haki za mtoto wa kike.” Aliongeza Mwang’onda.

Aliendelea kusema kwakuwa wanaume ni sehemu kubwa ya tatizo la ukatili wa kijinsia na ndio watekelezaji wakubwa wa ukatili huo wameamua kukaa nao ili kutafuta suruhisho la kudumu kuhusiana na tatizo hilo ili kuhakikisha watoto wa kike wanaishi katika jamii yenye haki na usawa.

Kwa upande wake Mgeni rasmi katika bonanza hilo, Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bi. Joyce Maketa amesema hali ya ukatili kwa watoto wa kike imeendelea kupungua katika wilaya ya Ilala sababu ikitajwa kuwa nimipango thabiti iliyowekwa na Serikali ya awamu ya tano Chini ya Jemedari Rais John Pombe Magufuli.

Aidha afisa huyo alisema kuwa amefurahishwa na bonanza hilo lililoandaliwa na CDF pamoja na ISDI kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswidi (SIDA) kwa kuweza kuwakutanisha vijana wa kiume nawanaume ili wawe mabalozi wazuri wakutetea nakupigania haki za mtoto wa kike ambazo atazipoteza kama hatopewa ulinzi stahiki na jamii inayomzunguka. 

Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Ilala Joyce Maketa(kushoto) akifuatilia kwa karibu bonanza, (katikati) CDF kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ISDI Bw. Jonas Tiboroha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ISDI Bw. Jonas Tiboroha akielezea kwa ufupi shughuli zinazofanywa na shirika hilo.

MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 05, 2018.