Saturday, October 27, 2018

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS MKURANGA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kutengenezea Gypsum Board kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Knauf kilichopo Mwanambaya Mkuranga Bw. Zachopolous Georgions. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua ujenzi wa barabara Mkuranga – Kisiju inayojengwa kwa kiwango cha lami ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya siku sita ya kukagua na kuhimiza shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya mpango wa kuborsha barabra za Mkuranga kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (katikati) wakati akikagua ujenzi wa barabara Mkuranga – Kisiju inayojengwa kwa kiwango cha lami ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya siku sita ya kukagua na kuhimiza shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani kulia pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia moja ya vifungashio vinavyotumika kufungashia vigae vya marumaru (tiles) alipotembelea kiwanda cha Goodwill Ceramic ltd kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Robin Huang. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ya vigae (tiles) moja alipotembelea kiwanda cha Goodwill Ceramic ltd kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Robin Huang. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MAGAZETI YA LEO OKTOBA 27 2018.

Friday, October 26, 2018

KAMARI BAGAMOYO ZAWAKERA WAZAZI NA WALIMU. WANAFUNZI WASHIRKI MICHEZO HIYO.

Michezo ya Kamari imekuwa kero katika mitaa ya Bagamoyo hali inayopelekea mmomonyoko wa maadili kwa vijana wenye umri mdogo.
BAGAMOYO KWANZA BLOG imejionea mashine hizo za Kamari zinazojulikana kama Kamari za Mchina au DUBWI, katika mitaa mbalimbali ya mji wa Bagamoyo.
Akizungumza na BAGAMOYO KWANZA BLOG Ofisini kwake, Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Nianjema iliyopo Kata ya Nianjema Halmashauri ya Bagamoyo, Renatus Godfrey Kisenha amekiri kuwepo kwa mchezo wa kamali jirani na shule yake hali inayopelekea wanafunzi kushiriki mchezo huo.

Kwa kweli ndugu Mwandishi hilo swala lipo tena hapa shuleni kwangu mashine hiyo ya Kamari ipo jirani na shule hali inayopelekea hata watoto wa Darasa la kwanza kushiriki mchezo huo wa kamari.

Alisema kitendo cha watoto kushiriki mchezo huo kinapelekea kuwa wezi kwa wazazi wao na walezi wao na muda mwingi akili zao zinafikiria kucheza kamali.

Aidha ameiomba Serikali kuangalia upya leseni za michezo hiyo ya kamali ili kulinda maadili ya vijana hasa wale ambao bado wapo shuleni wanahitaji utulivu wa akili kujisomea.

Mzazi mmoja ambae hakutaka jina lake liandikwe amekiri kushuhudia wanafunzi wa shule ya msingi wakicheza Kamari na kusema kuwa wanafunzi wadogo wa Darasa la kwanza wana mudu kucheza kwasababu gharama yake ni shilingi mia mbili tu. 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nianjema C. Shukuru Mzuri amesema kamali imekuwa kero sio tu kwa vijana wenye umri mdogo bali hata watu wazima ambao ni wake za watu hutumia fedha za matumizi ya chakula kuchezea kamali na kukiri kupokea kesi kutoka kwa waume zao juu ya tabia hiyo.

Alisema mara kadhaa amekuwa akipokea kesi za wanando kufuatia mke kushiriki kwenye kamari na kutumia fedha za matumizi ya nyumbani.

Aaidha, aliendelea kuthibitisha wizi wa fedha unaofanywa na watoto kwaajili ya kwenda kucheza kamari.
Mwenyekiti huyo alisema katika kitongoji chake amemkabili mwenye mashine hiyo ya Kamari na imehamishwa kupelekwa mtaa mwingine.
Kufuatia hali hiyo Kiongozi wa dini, Amiri wa Taasisi ya Srajulmunir Islamic Center ya Mjini Bagamoyo Sheikh Abdallaah, Kindamba, amesema kamali ni jambo lililharamishwa katika uislamu na kuiomba serikli kupiga marufuku aina zote za kamali ili kuwalinda vijana na mmomonyoko wa maadili na kuwajenga tabia ya kufanya kazi.

Sheikh Kindamba alisema kitendo cha kuruhusu Kamari kila mtaa kinawafanya vijana waone kumbe unaweza kupata fedha bila ya kufanya kazi na badala yake ukicheza Kamari unapata fedha.

BAGAMOYO KWANZA BLOG inafanya juhudi ya kuwapata viongozi wa serikali ngazi za juu kuzungumzia hili.

CHOO CHA SHULE CHATITIA ARUMERU.

Jengo la choo cha shule ya Msingi ya Seliani katika kijiji cha Olevolosi kata ya kimnyaki Wilaya ya Arumeru limetitia  katika tukio hilo ameokolewa  Mwanafunzi Mmoja wa Kiume aliepata majeraha sehemu na bado  jitahada za kuondoa kifusi kilichochanganyikana na matofali ambacho kimezama katika Shimo la choo kilichokuwa na matundu 20 zinaendelea.



Katika kukabiliana na Changamoto Iliyotokea Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro akiambatana na Katibu Katibu tawala wa Wilaya na viongozi wa Halmashauri ya Arusha walifika kwenye eneo la tukio na kuanza kazi ya kuratibu jitihada za uokoaji wakishirkiana na vikosi vya uokoji na Zimamoto pamoja na mamia ya wananchi wa kata ya kimnyaki.

Katika shughuli hiyo ya uokoaji walifanikiwa kumuokoa mwananfunzi Mmoja akiwa amejeruhiwa usoni na kukimbizwa katika hospital ya Seliani kwa matibabu zaidi ambapo mpaka sasa vikosi vya uokoaji vinaendelea na jitihada za kufukua kifusi pamoja na matofali yaliyozama katika choo hicho Cha shule chenye matundu 20 ambacho ndio choo pekee Kinachotumiwa na zaidi ya wanafunzi 1,121 wa shule hiyo.

Katika Eneo la tukio kwanza irejeshwa hali ya Amani na kutuliza taharuki za wananchi ambao baadhi Wana watoto wanaosoma katika shule hiyo  vikosi vya ukoaji vinaendelea na zoezi la kutafuta wanafunzi wengine Kutokana na kutokupatikana kwa Taarifa za awali zinazoonyesha idadi ya Wanafunzi ambao huenda walikuwa kwenye choo hicho.


Awali kwa upande wao baadhi ya wananchi waliungana na Mkuu wa Wilaya katika kuchanga Fedha kwa ajili ya kuanza Mikakati ya Ujenzi wa choo kingine ili kutokwamisha masomo ya wanafunzi kazi ambayo ilifanywa na Mkuu wa Wilaya pamoja na viongozi wa Kanisani na halmashauri na kuitikiwa kwa wingi na wananchi waliotoa Fedha zao.

Awali Mhe Muro alilazimika kumtembelea majeruhi ambae amelazwa katika hospitali ya seliani na kumjulia hali uku akiongozana na viongozi mbalimbali.
 
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama, Mhe. Jerry Muro akiwa eneo la tukio kushiriki shughuli za uokoaji.