Monday, October 22, 2018

WABUNGE WA BAGAMOYO WAHUDHURIA MAZISHI YA BABA MZAZI WA KATIBU MWENEZI CCM WILAYA.

MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa wa pili ksuhoto na Mbunge Jimbo la Chalinze Mwanasheria Ridhiwani Kikwete, (mwenye kanzu) wakishiriki mazishi yaa baba mzazi wa katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Bagamoyo John Fransic (Bolizozo) mwenye shati la njano na nyeusi pichani.
.............................................

 Na Omary Mngindo, Lugoba Bagamoyo.

MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa na Mbunge Jimbo la Chalinze Mwanasheria Ridhiwani Kikwete, Ijumaa ya Oktoba 19 wamewaongoza mamia ya waombolezaji katika kumzika Mzee Philipo Masenga, Baba wa John Fransic Bolizozo.

Bolizozo ambaye ni Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo, amefikwa na msiba huo Alhamisi ya Oktoba 18 ambapo alisema Mzee Masenga alikuwa anaugua kwa muda mrefu, na kwamba juhudi zilifanyika za matibabu lakini ahadi imetimia.

Dkt. Kawambwa na Ridhiwani kwenye mazishi hayo, wakiwa makaburini waliwaongoza mamia ya waombolezaji katika kuweka udongo kaburini, ikiwa ni safari ya mwisho ya Mzee Masenga wakifuatiwa na watu mbalimbali.

Kwenye mazishi hayo Wabunge hao wameambatana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Abdul Sharifu, Katibu Kombo Kamote na viongozi mbalimbali wa chama hicho kutoka ngazi za Kata na matawi.

Mbali ya hao pia Wenyeviti wa Halmashauri za Chalinze Said Zikatimu na Ally Ally wa Bagamoyo wameambatana na Madiwani kutoka kwenye Kata wakiwemo wa Viti Maalumu kwenye Tarafa mbalimbali wa majimbo hayo mawili.
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa akiweka mchanga katika kaburi.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mwanasheria Ridhiwani Kimwete nae akiweka udongo katika kaburi hilo (Picha zote na Omary Mngindo)

MBUNGE DKT. KAWAMBWA ASEMA WAKANDARASI WAWILI KUJENGA BARABARA YA MAKURUNGE,SAADANI HADI PANGANI.

 Mbungw wa jimbo Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Gama, Kata ya Makurunge alipokwenda kusikiliza cjangamoto zinazowakabiri wapigakura wake (Hawapo pichani).

Na Omary Mngindo, Makurunge Bagamyo.

MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo Mkoa wa Pwani Dkt. Shukuru Kawambwa, amesema kuwa barabara ya Makurunge, Saadani mpaka Pangani Tanga itajengwa na Wakandarasi wawili ili wakazi wote waanze kuona kazi hiyo.

Dkt. Kawambwa ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kitongoji cha Kifude, Kata ya Makurunge jimboni humo, akiwa kwenye ziara ya kupokea changamoto zinazowakabili wapigakura wake, kisha kuziwasilisha katika bunge lijalo.

Ziara ya Mbunge Dkt. Kawambwa iliyoanzia Ijumaa ya Oktoba 19 inayotarajiwa kukamilika Oktoba 30 mwaka huu,  alitoa ufafanuzi huo baada ya mmoja wa wakazi aliyejitambulisha kwa jina la Salum Juma kutaka kujua lini kazi hiyo itaanza, huku akiongeza kuwa wanahamu ya kuona kazi hiyo ikianza.

"Mheshimiwa Mbunge tunataka kufahamu ujenzi wa Barabara inayotokea Makurunge kupitia Saadani, Pangani Tanga lini utaanza?, tunahitaki kuona mabasi yakipitia Barabara hii kwani itatuongezea fursa kiuchumi," alisema Juma.

Akizungumzia kuhusu ujenzi huo, Dkt. Kawambwa alisema kwamba anaimani kubwa kuwa kazi hiyo itafanyika mapema iwezekanavyo, kwa Wakandarasi wawili kufanyakazi kwa wakati mmoja kwa maana ya eneo la Bagamoyo na Pangani Tanga.

"Nilipokuwa bungeni nimemuomba Waziri mwenye dhamana ikiwezekana kuwepo na Wakandarasi wawili wataoanza kazi kwa maana ya kianzia upande wa Bagamoyo na Pangani, akanihakikishia kuwa hilo litawezakana," alisema Dkt. Kawambwa.

Awali Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Stamili Bondo alimweleza Mbunge hiyo kuwa hivi sasa wanaendelea na ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi ikiwa na lengo la kuhakikisha watoto hawatembei umbali mrefu, huku akishukuru mchango wa shilingi laki tano kutoka mfuko wa Jimbo.

Akiwa katika Kijiji cha Gama Dkt. Kawambwa amepokea malalamiko ya fidia ya zaidi ya shilingi bilioni moja inayodaiwa kulipwa kwa wananchi awanaotakiwa kupisha mradi wa miwa uliochini unaosimamiwa na Kampuni ya Bagamoyo Sugar.

Baadhi ya wakazi Lukhia Yusufu na Hassan Lingwa kwa niaba ya wenzao wamelalamikia sakata hilo ambao wanedai wengine hawakuingizwa katika tathimini kutokana na kwamba wakati wa zoezi hawakufikiwa kutokana na kuwa kipindi cha mvua.

Dkt. Kawambwa ameahidi kuzichukua changamoto hizo kisha kwenda kuzifikisha kwa viongozi wa ngazi husika kwa lengo la kuzifanyiakazi, huku akiwaomba wanamchi hao kuwa watulivu.
 Wakazi wa Kijiji cha Gama wakimsikiliza Mbunge wao Dkt. Shukuru Kawambwa alipofanya ziara ya siku moja ndani ya Kata ya Makurunge. Picha zote na Omary Mngindo.

MAGAZETI YA LEO 22 OKTOBA 2018.

Saturday, October 20, 2018

MWAKYEMBE AFUNGUA RASMI TAMASHA LA SANAA BAGAMOYO LEO TAREHE 20 OKTOBA 2018.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa kufungua rasmi Tamasha la kimataifa la Sanaa Bagamoyo linaloendelea ndani ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)  ikiwa ni Tamasha la 37.
 
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa katika Ukumbi wa TaSUBa leo Tarehe 20 Oktoba 2018.
  
 Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Bagamoyo (DAS) Hamza Amri Athumani, na kulia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Dkt. Herbert Makoye.


 Kikundi cha Sanaa kutoka nchini Finland kikionesha ufundi wake ndani ya jukwaa la TaSUBa mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.


Sehemu ya umati wa watu waliofika kushuhudia ufunguzi wa Tamasha la 37 la kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo.