Friday, June 8, 2018

WAFICHUENI WANAOWAPA MIMBA WANAFUNZI.

Wanafunzi wa shule za Bagamoyo wakiwa kwenye maandamano kuadhimisha wiki ya Elimu.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Alphonce Amuli, akiongea kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo.
.....................................
Wazazi na walezi wilayani Bagamoyo wametakiwa kutoa ushirikiano ili kuwafichua wale wote wanaowapa mimba wanafunzi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga katika hutuba iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Alphonce Amuli wakati wa maadhimisho ya wiki ya Elimu.

Alisema watoto wengi hukatisha masomo kwasababu ya kupewa mimba lakini juhudi za kukomesha vitendo hivyo zinakwama kutokana na wazazi au walezi kutotoa ushirikiano kwa vyombo vya sheria ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao.

Aliongeza kwa kusema kuwa serikali imetunga sheria kali katika kuhakikisha vitendo vya kuwapa mimba wananfunzi vinakomeshwa ili watoto wa kike wapate elimu ambayo ni haki yao ya kikatiba.

Akizungumzia swala la elimu Amuli alisema kufuatia viwanda vinavyoendelea kujengwa wilayani Bagamoyo watoto wanapaswa kupewa elimu itakayowanufaisha katika soko la ajira na ile ya kujiajiri.

Aidha, alisema serikali kwa kutambua umuhimu wa elimu inatoa elimu bure kwa wote na kutoa fedha zitakazosadia upatikanaji wa elimu bure ili kila mtoto apate elimu.

Aliongeza kuwa walimu wakuu wanapaswa kusimamia vizuri fedha za elimu bure ikiwa ni pamoja na kuzipeleka kwenye matumizi stahiki ili lengo la serikali liweze kutimia.

Alisema kufuatia hali hiyo wazazi na walezi jukumu lao ni kuwapeleka watoto shule na kuwasimamia ipasavyo.

Awali akisoma Taarifa ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Afisa Elimu Msingi Peter Fussi alisema kufuatia utoaji wa elimu bure idadi ya wanafunzi  wanaoandikishwa shule za awali na msingi imeongezeka kutoka wanafunzi 25228 mwaka 2017 na kufikia 27508 mwaka 2018.

Hata hivyo fussi alisema Halmashauri ya Bagamoyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa ambapo mahitaji  katika idara ya elimu ya msingi ni vyumba 621 na kwamba vilivyopo ni 292 na hivyo kufanya upungufu wa vyumba vya madarasa ni 329.

Aliongeza kuwa idara ya elimu sekondari mahitaji ni vyumba vya madarasa 162 yaliyopo ni madarasa 124 ambapo pungufu ni madarasa 38.

Wiki ya elimu huadhimishwa kila mwaka ikiwa na lengo la kutoa fursa kwa shule, serikali na wadau mbalimbali kutathmini changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni  Uwajibikaji wa pamoja kwa elimu bora kwa watu wote.
 
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Alphonce Amuli akipokea maandamano ya wanafunzi yalipowasili uwanjani.
 Wanafunzi wa Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM)wakiongoza maandamano katika maadhimisho ya wiki ya elimu yaliyofanyika uwanja wa majengo Bagamoyo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya wiki ya elimu yaliyofanyika Bagamoyo Alphonce Amuli akikagua mabanda yaliyoandaliwa na shule mbalimbali kama anavyoonekana pichani akiwa katika banda la shule ya msingi Nianjema ambapo alijionea Teknolojia ya habari na namna ya masomo mengine yanavyofundishwa.

Alphoncee Amuli ni kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu ( ADEM) ambae alimuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga.
 
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya wiki ya elimu yaliyofanyika Bagamoyo Alphonce Amuli akikagua mabanda yaliyoandaliwa na shule mbalimbali kama anavyoonekana pichani ambapo alijionea namna ya masomo yanavyofundishwa.


Alphonce Amuli ni kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu ( ADEM) ambae alimuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya wiki ya elimu yaliyofanyika Bagamoyo Alphonce Amuli akikagua mabanda yaliyoandaliwa na shule mbalimbali kama anavyoonekana pichani ambapo akiwa katika banda la ADEM ambapo alijionea namna ya masomo yanavyofundishwa.

Alphonce Amuli ni kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu ( ADEM) ambae alimuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga
Sehemu ya wananfunzi walioshiriki maadhimisho hayo ya wiki ya elimu.
Wanafunzi wa shule ya Mwanamakuka wakionyesha umahiri wao katika maonyesho ya sarakasi

Thursday, June 7, 2018

UMITASHUMTA YAZINDULIWA CHALINZE



Sehemu ya washiriki wa UMITASHUMTA wa Halmashauri ya Chalinze.
 
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwangaakizungumza wakati wa uzinduzi wa UMITASHUMTA wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Said Omari Zikatimu, wa tatu ni Afisa Elimu msingi Zainabu Makwinya na wa mwisho ni Afisa Elimu Taaluma Miriam Kihiyo.
................................................
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga amewataka vijana wa shule za msingi kusoma kwa bidii ili vipaji walivyonavyo wavitumie wakiwa na elimu.

Majid aliyasema hayo wakatai wa uzinduzi wa mashindano ya  Uendeshai wa Michezo ya Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) uliofanyika katika viwanja vya shule ya Lugoba Halmashauri ya Chalinze.

Alisema michezo inaibua vipaji kwa watoto lakini ni vyema vipaji hivyo vikatumika sambamba na elimu kwani mwenye elimu hutumia vizuri kipai chake.

Aidha aliwataka walimu kuwasimamia watoto mashuleni katika kuhakikisha wanapata elimu bora sambamba na kudumisha michezo ambayo itawajenga ki afya na ukakamavu wa miili yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Edes Lukoa amewataka vijana wa shule za msingi kuwa na bidii katika michezo ili kukuza vipaji vyao kwaaili ya maendeleo ya baadae.

Alisema wachezaji wakubwa wa michezo mbalimbali duniani wameanza wakiwa wadogo hivyo na wao wasikate tamaa na badala yake waongeze juhudi.

Aidha, aliwataka kuwa na nidhamu kwa walimu wao ili waweze kuelewa kile wananchofundishwa na hatimae kufaulu vizuri katika masomo yao pamoja na michezo.

Awali akisoma Taarifa mbele ya mgeni rasmi Afisa Elimu Taaluma Halmashauri ya Chalinze Miriam Kihiyo alisema Halmashauri ya Chalinze itatoa timu moja itakayoshiriki katika mashindano ya kumtafuta mshindi wa Mkoa.

Alisema michezo itakayoshindaniwa ni Mpira wa miguu, Mpira wa pete, Mpira wa Mikono na Mpira wa wavu.
 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Saidi Omari Zikatimu akizungumza katika uzinduzi wa UMITASHUMTA.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Edes Lukoa akizungumza katika uzinduzi wa UMITASHUMTA.

  Afisa Elimu Taaluma wa Halmashauri ya Chalinze Miriam Kihiyo akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Risala.
 
 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Edes Lukoa akiwa gorini kwaajili ya kudaka mpira kuashiria uzinduzi wa UMITASHUMTA katika Halmashauri ya hiyo.


 Vijana kutoka timu ya Msata na Chalinze wakichuana katika mechi ya ufunguzi iliyofanyika katika viwanja vya shule ya Lugoba.

SERIKALI YA BAGAMOYO YAFANYIA KAZI MAOMBI YA WANANCHI KUHUSU MSITU WA ZIGUA.

Kaimu meneja wa TFS Chalinze Jonathan Mpangala (katikati) akiwaonyesha wajumbe wa kamati siasa wilaya ya Bagamoyo mipaka ya msitu wa Zigua katika kijiji cha kwa Mduma.
  
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga wa kwanza kushoto akizungumza na wnanchi katika kijiji cha kwa Mduma.
 ..........................................
Serikali wilayani Bagamoyo imepokea ombi la wnanchi katika kijiji cha Kwa Mduma kata ya Kibindu la kutaka kuongezewa eneo la makazi kutoka msitu wa Zigua.

Kauli hiyo imetolew na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga wakati wa ziara ya kukagua mipaka ya Msitu wa Zigua.

Mkuu huyo wa wilaya alisema lengo la ziara hiyo ambayo imewajumuisha kamati ya siasa wilaya ni kupata uelewa wa pamoja kuhusu hitajio la wananchi wa kwa Mduma na kuona namna gani wanaweza kuwasilisha maombi ya wananchi hao ngazi za juu.

Alisema kufuatia ukweli kwamba sehemu wanayodai ni muhimu kwakuwa tayari kuna zahanati ambayo inawahudumia wananchi hao, serikali ya wilaya inachukua ombi hilo na kuwasilisha kw Mkuu wa Mkoa ili kuona namna ya kurekebisha mipaka ya TFS katika kijiji hicho.

Kaimu meneja wa TFS Chalinze Jonathan Mpangala lisema  katika harakati za kuondoa wavamizi ndani ya msitu wa zigua zipo baadhi nyumba kijiji cha kwa Mduma hazikubomolewa kutokana na kusikiliza maoni ya wananchi wa kijiji hicho.

Alisema nyumba hizo ni pamoja Zahanati, nyumba ya Mganga na nyumb 8 za watu binafsi ambapo vikao vimefanyika ngazi ya wilaya ili kuona namna kurekebisha mipaka upande huo wa kijiji cha kwa mduma.

Aliongeza mchakato unaendelea kuanzia ngazi ya kijiji, wilaya nakanda ambapo ofisi ya kanda itawasilisha mapendekezo hayo ngazi Taifa.

Nae Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo Abdu Rashid Zahoro amesema Chama cha Mapinduzi wilaya kitashirikiana na serikali kuona namna bora ya kurekebisha mipaka ya msitu huo.

Alisema CCM wilaya imejionea hali halisi ya malalamiko ya wananchi hao na kwamba wameona haja ya kuwashughulikia malalamiko yao ili eneo hilo libaki kwa makazi ya watu na shughuli za kibinadamu kama watakavyoona inafaa serikali ya kijiji.
  Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo Abdu Rashid Zahoro akizungumza na wananchi wa kijiji cha kwa Mduma.
 
Kaimu meneja wa TFS Chalinze Jonathan Mpangala (katikati) akiwaonyesha wajumbe wa kamati siasa wilaya ya Bagamoyo ramani ya msitu wa Zigua katika kijiji cha kwa Mduma.
 
 Wajumbe wa kamati siasa wilaya ya Bagamoyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya, wakati walipotembelea msitu wa Zigua katika kijiji cha kwa Mduma.
 Kaimu meneja wa TFS Chalinze Jonathan Mpangala (wa pili kushoto) akiwaonyesha wajumbe wa kamati siasa wilaya ya Bagamoyo mipaka ya msitu wa Zigua katika kijiji cha kwa Mduma.
 

Tuesday, June 5, 2018

JAFO APIGA MARUFUKU MAMLUKI KUSHIRIKI UMISSETA NA UMITASHUMTA



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amewataka Wakuu wa Mikoa kuhakikisha kuwa mikoa yao inapeleka wachezaji wanafunzi watakaoshiriki mashindano ya UMISSETA iliyoanza leo katika viwanja vya chuo cha Ualimu Butimba kilichopo jijini Mwanza.

Aidha amewataka waamuzi watakaochezesha mashindano hayo pamoja na yale ya UMITASHUMTA kuhakikisha kuwa wanachezesha michezo hiyo kwa kuzingatia kanuni na sheria bila kuwepo upendeleo ili washindi wa michezo yote wapatikane kwa haki.


Akizungumza  na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Waziri Jafo alieleza kuwa mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) yaliyoanza leo yatafanyika yataendelea hadi hadi Juni 15 mwaka huu.


Mashindano ya UMISSETA yatafuatiwa na michezo ya UMITASHUMTA ambayo yatafanyika katika viwanja hivyo hivyo kuanzia tarehe 17 juni 2018 hadi tarehe 29 juni 2018.


Waziri Jafo alieleza kuwa michezo hiyo inatarajiwa kufunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa katika uwanja wa CCM Kirumba hivi karibuni.


Kwa mujibu wa Mhe.jafo, jumla ya wanamichezo 3,360 watashiriki mashindano hayo wakitokea mikoa 28 upande wa Umisseta, 26 Tanzania Bara na miwili ya Zanzibari, huku Umitashuta mikoa 26 ya Tanzania Bara tu.


Kwa upande wa Umisseta michezo itakayochezwa ni pamoja na soka kwa wavulana na wasichana, netiboli kwa wasichana, wavu kwa wasichana na wavulana, mpira wa mikoni, mpira wa kikapu, riadha maalumu(watu wenye ulimavu).


Mingine ni Riadha ya kawaida, mchezo wa bao kwa wavulana, sanaa za maonyesho (kwaya, ngoma, mashairi, ngonjera) na mpira wa meza.

Tuesday, May 29, 2018

MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CCM (NEC)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein(kushoto) alipokuwa akizungumza na kumpongeza Dk.Bashiru Ali (kulia) mara baada ya kuteuliwa na kupata ridhaa ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC)kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa  ulioendelea leo katika Ukumbi wa   Kiwete Ikulu Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli(katikati),
Katibu Mpya wa CCM Taifa Dk.Bashiru Ali (kulia) mara baada ya kuteuliwa na kupata ridhaa ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa  ulioendelea leo katika Ukumbi wa   Kiwete Ikulu Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli(hayupo pichani),
 
Katibu Mpya wa CCM Taifa Dk.Bashiru Ali (kulia) alipokuwa akiwashukuru Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) mara baada ya kuteuliwa na kupata ridhaa ya   kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa  katika Mkutano ulioendelea leo katika Ukumbi wa   Kiwete Ikulu Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli(katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Nd,Rodrik Mpogolo
Wajumbe wa Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) wakinyanyua mikono juu kuashiria kuunga mkono uteuzi wa Katibu Mpya wa CCM Taifa Dk.Bashiru Ali wakati wa Mkutano ulioendelea leo katika Ukumbi wa   Kiwete Ikulu Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli(hayupo pichani)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein(kushoto) alipokuwa akimpongeza Dk.Bashiru Ali (kulia) mara baada ya kuteuliwa na kupata ridhaa ya Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa  ulioendelea leo katika Ukumbi wa   Kiwete Ikulu Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli(katikati)


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein(kushoto) alipokuwa akimuonesha kitu  Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli wakati wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa  ulioendelea leo katika Ukumbi wa   Kiwete Ikulu Jijini Dar es Salaam,

Picha na Ikulu.


RAIS DKT. MAGUFULI AANDAA FUTARI IKULU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijiunga na wageni mbalimbali kuchukua futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018.
 
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubeiry Ally akiswalisha viongozi na waalikwa mbalimbali swala ya Magharibi kabla ya futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha kufuturu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheik Aboubakary Zubeiry Ally  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
Waziri wa masuala ya Dini wa Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek akipakua futari akiwa ameongozana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Balozi wa Saudi Arabia nchini Mhe. Mohamed bin Mansour al Malik Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na akikaribisah wageni wake kuchukua futari na kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na akikaribisah wageni wake kuchukua futari na kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018
 Mawaziri Wakuu Wastaafu Dkt. Salim Ahmed Salim, Jaji Joseph Sinde Warioba na waalikwa wengine wakichukua futari Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018.
Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi akiwa na Jaji Mkuu Profesa Inbrahim Juma na  Kaimu Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikianowa Afrika Mashariki, Bw. Suleiman Salehe wakichukua futari
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) akifuatiwa na Inspekta Jenerali wa Polisi Simon Sirro, Inspekta Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa (wa pili kulia) na wageni wengine wakichukua futari iliyoandaliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018 
 

 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mama Janeth Magufuri, Mama Mary Majaliwa, Mama Anna Mkapa na Mama Khadija Mwinyi wakiongea baada ya kupata  futari iliyoandaliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018  
 Kamishna  Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (kulia) akiwa na Mama Evelyn Warioba wakiwa katika futari hiyo
Waalimwa wakibadilishana mawazo baada ya kufuturu Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Mei 28, 2018


TAARIFA KWA UMMA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA (NEC)

NAIBU WAZIRI SUBIRA MGALU AFAFANUA MIRADI YA UMEMEVIJIJINI INAYOENDELEA KUTEKELEZWA.

Serikali imesema itaendelea na usambazaji wa umeme vijijini kupitia miradi inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kasi zaidi ili vijiji vyote vilivyoingizwa kwenye Mradi vifikiwe na umeme.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni na Naibu Waziri wa Nishati Subira Hamisi Mgalu wakati wa kuchangia Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/19 ambapo amewahakikishia wabunge kuwa Serikali kupitia wizara ya Nishati imejipanga kwa kasi mpya ya utekelezaji wa Miradi hiyo.

Naibu waziri huyo wa Nishati alisema wizara imepokea changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa kusambaza umeme vijijini kwenye Miradi inayotekelezwa  kupitia Wakala wa Nishati Vijiini (REA) na kwamba tayari wizara imejipanga kuhakikisha changamoto hizo zinapatiwa ufumbuzi ili kazi isipate vikwazo.

Katika kuchangia Bajeti ya wizara ya Nishati wabunge walitaka kujua vijiji ambavyo havijafikiwa na umeme ni mkakati upi wa wizara kuhakikisha vijiji hivyo vinapata umeme kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Naibu waziri Subira Mgalu alifafanua kazi zilizofanywa na zile ambazo zinaendelea kufanywa kupitia REA na kuongeza kuwa hakuna kijiji ambacho kipo kwenye mpango kitakachorukwa kwenye utekelezaji.

Alisema wizara imepokea changamoto mbalimbali zilizojitokeza kwenye utekelezaji wa REA awamu ya kwanza ya pili na ya tatu na kwamba tayari wizara imeweka mpango mkakati wa kushughulikia kasoro zote zilizojitokeza.

Aliongeza kwa kusema kuwa kutokana na malalamiko ya wabunge wengi kwamba kuna baadhi ya vijiji vimerukwa, vitongoji na baadhi ya taasisi za uma hazijafikiwa na umeme tayari hayo yote yanafanyiwa kazi kwaajili ya utekelezaji

Katika kuhakikisha hayo yanafanyiwa kazi, tayari wizara imekuja na orodha ya vijiji vipya 1541 ambavyo vinahitaji kufikiwa na miradi ya REA endapo Bunge litaidhinisha.

Alisema tayari mpaka sasa vijiji 545 vimefikiwa na umeme huku vijiji 502 miundombinu inaendelea kujengwa ili navyo vifikiwe na umeme.

Aidha, alisema serikali kupitia Benki kuu imeshafungua Barua za mikopo (Leters of Credit) za bilioni 268 kwa kampuni 18 na kuongeza kuwa hali hiyo itaongeza kasi ya utekelezaji wa miradi.


Naibu waziri Subira Mgalu alisema kuwa Miradi ya umeme vijijini ipo ya aina nyingi ikiwemo wa (Densification –Round I) ambapo Awamu ya Kwanza (Densification –Round I) ulianza mwezi Aprili, 2017 katika mikoa nane (8) ya Pwani, Tanga, Arusha, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe na Mara

Alisema hadi kufikia mwezi Mei, 2018 awamu hiyo imekamilika kwa asilimia 98. ambapo jumla ya vijiji 300 kati ya 305 vimepatiwa umeme pamoja na  kuwaunganishia umeme wateja wa awali 12,084 kati ya 53,000, ambao Gharama ya utekelezaji kwa awamu hiyo ni Shilingi bilioni 62.

Aidha, aliongeza kwa kusema kuwa, Mradi wa Densification awamu ya pili utahusisha vitongoji vilivyomo katika vijiji 4,090 vilivyosalia na unakadiriwa kugharimu jumla ya Shilingi bilioni 1,938. na kwamba Awamu hiyo itaanza kutekelezwa mwezi Julai, 2018.

Naibu waziri wa Nishati aliendelea kufafanua kuwa, baada ya kubaini mahitaji ya umeme ni makubwa upo Mradi mpya unaojulikna kama Mradi wa Usambazaji Umeme katika Vijiji vilivyopo Pembezoni mwa Miji (Peri-Urban Rural Electrification Program) ambao utasaidia kuwafikia watu wengi maeneo hayo.

Alisema Mradi wa Peri-Urban unalenga kusambaza  umeme katika vijiji vilivyopo pembezoni mwa miji ili kuboresha huduma za kijamii na kuhamasisha ujenzi wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa katika maeneo hayo.

Aidha, aliongeza kuwa, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wamekamilisha usanifu wa mradi wa majaribio utakaotekelezwa katika Mkoa wa Pwani na Wilaya ya Kigamboni Mkoani Dar es Salaam.

Mradi huo utavinufaisha vijiji/vitongoji zaidi ya 250 na kuwaunga wateja wa awali wapatao 37,000 na kusema kuwa Mradi huo unafadhiliwa na Serikali ya Norway kwa gharama ya Shilingi bilioni 83. na kwamba unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili,2019.

Alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli katika mpango wake ni kufikisha umeme vijiji vyote 7200 ifikapo mwaka 2020 hivyo wao kama viongozi katika wizara yenye dhamana ya Nishati ni kuhakikisha wanakwenda sambamba na malengo ya Rais Dkt. Magufuli.

Wakati huohuo Naibu waziri huyo wa Nishati alisema Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) imeonyesha nia ya kusaidia usambazaji wa umeme katika miji mikubwa ya Mwanza, Arusha Dodoma ambapo tayari upembuzi yakinifu unaendelea kuhusu miradi hiyo.

Aidha, Naibu waziri huyo wa Nishati ametoa wito kwa wasimamizi wa Miradi na Wakandarasi kote nchini kuwashirikisha wenyeviti wa serikali za mitaa, Wabunge, na Wakuu wa wilaya ili kuhakikisha Miradi hiyo inatekelezwa kwa uwazi bila ya upendeleo utakaypelekea manung'uniko kutoka kwa wananchi au wawakilishi wao ambao ni wabunge.

Alisema wananchi wanatakiwa kuchangia kuunganishwa umeme kwa gharama ya 27,000 tu na si zaidi ya hiyo na kwamba ameonya wale watakaokiuka maagizo hayo.
 
 Naibu Waziri wa Nishati Subira Hamisi Mgalu akitoa ufafanuzi Bungeni kuhusu utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.


imeandikwa na Athumani Shomari wa bagamoyokwanza.blogspot.com.