Friday, September 22, 2017

UFUNGUZI WA MSKITI ZANZIBAR.

DSC_6413DSC_6491

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Kituo Kikuu cha Sayansi na Utamaduni cha Sultan Qaboos,”Sultan Qaboos Higher Center for Culture and Science” Mhe.Habib Mohammed Al-Riyami mara alipowasili katika ufunguzi Msikiti Massjid Jaamiu Zinjibar uliopo  Mazizini Wilaya Magharibi ‘B” Mkoa wa Mjini Magharibi leo,uliojengwa na Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman
 DSC_6494
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Viongozi mbali mbali  mara alipowasili katika ufunguzi Msikiti Massjid Jaamiu Zinjibar uliopo  Mazizini Wilaya Magharibi ‘B” Mkoa wa Mjini Magharibi leo,ambao umejengwa na Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman
 DSC_6508
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Viongozi mbali mbali  mara alipowasili katika ufunguzi Msikiti Massjid Jaamiu Zinjibar uliopo  Mazizini Wilaya Magharibi ‘B” Mkoa wa Mjini Magharibi leo,ambao umejengwa na Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman,
 DSC_6641
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein alipofuatana na Viongozi mbali mbali wakiwemo Kituo Kikuu cha Sayansi na Utamaduni cha Sultan Qaboos,”Sultan Qaboos Higher Center for Culture and Science” wakati alipotembelea sehemu mbali mbali za Msikiti Masjid Jaamiu  Zinjibar baada ya kuufungua rasmi leo,ambao  umejengwa Mazizini Wilaya Magharibi ‘B” Mkoa wa Mjini Magharibi kwa Ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Watu wa Oman,
 DSC_6682
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kituo Kikuu cha Sayansi na Utamaduni cha Sultan Qaboos,”Sultan Qaboos Higher Center for Culture and Science” Mhe.Habib Mohammed Al-Riyami wakati alipotembelea sehemu mbali mbali mara alipofungua Msikiti Massjid Jaamiu Zinjibar uliopo  Mazizini Wilaya Magharibi ‘B” Mkoa wa Mjini Magharibi leo,uliojengwa na Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman
 DSC_6996
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipokea Shahada na Ufunguo kutoka kwa Mkuu wa Kituo Kikuu cha Sayansi na Utamaduni cha Sultan Qaboos,”Sultan Qaboos Higher Center for Culture and Science” Mhe.Habib Mohammed Al-Riyami kama ishara ya ufunguzi rasmi wa Msikiti Masjid Jaamiu  Zinjibar leo uliojengwa kwa Ushirikiano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Watu wa Oman katika maeneo ya Mazizini Wilaya Magharibi ‘B” Mkoa wa Mjini Magharibi,
Picha na Ikulu

ROLI LA MIZIGO LAPINDUKA KIWANGWA, BAGAMOYO.

 Gari la mizigo aina ya Isuzu lenye namba za usajili T 207 ARR likiwa na Mzigo limepinduka  eneo la Kiwangwa wilayani Bagamoyo Asubui ya leo Tarehe 22 Septemba 2017, mashuhuda wa ajali hiyo walisema hakuna mtu aliypoteza maisha katika ajali hiyo.
 
Wanachi wa eneo la Kiwangwa wilayani Bagamoyo wakiangalia ambalo limenduka leo Asubuhi, Gari hilo aina ya Isuzu lenye namba za usajili T 207 ARR likiwa na Mzigo limepinduka  eneo la Kiwangwa wilayani Bagamoyo Asubui ya leo Tarehe 22 Septemba 2017, mashuhuda wa ajali hiyo walisema hakuna mtu aliypoteza maisha katika ajali hiyo

 
 Wanachi wa eneo la Kiwangwa wilayani Bagamoyo wakiangalia ambalo limenduka leo Asubuhi, Gari hilo aina ya Isuzu lenye namba za usajili T 207 ARR likiwa na Mzigo limepinduka  eneo la Kiwangwa wilayani Bagamoyo Asubui ya leo Tarehe 22 Septemba 2017, mashuhuda wa ajali hiyo walisema hakuna mtu aliypoteza maisha katika ajali hiyo

KAMATI YA AMANI BAGAMOYO YATEMBELEA HOSPITALI.



Wadau mbalimbali pamoja na wananchi wilayani Bagamoyo wametakiwa kujitokeza kuchangia damu salama katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo, ili kukabiliana na upungufu wa damu hospitalini hapo.

Wito huo umetolewa na Kamiu Muuguzi Mfawidhi Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo, Saufa Khalifa, alipokuwa akizungumza mara baada ya kamati ya Amanai wilayani Bagamoyo kutembelea Hospitalini hapo.

Saufa alisema kwa sasa Hospitali hiyo inakabiliwa na upungufu wa damu, hivyo ni vyema wananchi wakajitokeza kuchangia damu ili kuiwezesha Hospitali hiyo kutoa huduma stahiki kwa wagonjwa wanaofika hospitali hapo.

Alisema wanamshukuru Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid mwanga kwa kutafuta wafadhili ambao ni Taasisi ya Kiislamu ya  Dhi Nureyn  inayojenga jengo la wodi ya wazazi na jengo la wagonjwa wa dharula na kuongeza kuwa, jengo la huduma ya dharula linahitaji uwepo wa damu kwa wingi ili hata kama wanaletwa wagonjwa wa ajali ambao wametokwa na damu nyingi waweze kuwekewa damu haraka iwezekanavyo.

Kwa upande wao viongozi wa kamati ya Amani wilayani Bagamoyo, ambao wamefika Hospitalini hapo wamesema watashirikiana na serikali katika kuhamasisha wananchi kuchangia damu salama.

Walisema kazi ya kamati ya amani ambayo inaundwa na dini zote ni kuwajenga waumini wao kiroho na kuweza kujitolea katika shughuli za kijamii na kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Kamati ya Amani wilayani Bagamoyo imefanya ziara katika Hospitali ya Bagamoyo kwa lengo la kuangalia wagonjwa na kuwaombea duwa pamoja na kukagua majengo yanayoendelea kujengwa Hospitali yanayojengwa na Taasisi ya Kiislamu ya Dhi Nureyn ya Mjini Iringa.
 Kamiu Muuguzi Mfawidhi Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo, Saufa Khalifa,akitoa maelezo kwa kamati ya Amani ya wilaya ya Bagamoyo iliyofika Hospitalini hapo.