Saturday, March 18, 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA WAZIRI WA AFYA WA KENYA LEO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu.
...................................

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekubali ombi la Serikali ya Kenya la kuwapatia madaktari 500 kufuatia upugufu wa madaktari uliotokana na mgomo nchini humo.

Akizungumza  leo  na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema kutoka na maombi yaliyotolewa, serikali imeandaa utaratibu kwa madaktari wa kitanzania kuwasilisha maombi yao katika tovuti ya wizara ya afya pamoja kufuata taratibu zingine kama watakavyoelekezwa.

Alizitaja sifa za anayetakiwa  kuomba nafasi hiyo kuwa ni shahada ya kwanza ya udaktari,  mafunzo ya vitendo pamoja na kusajiliwa na Baraza  madaktari la Tanganyika na  kutuma maombi hayo katika barua pepe; maombiyakazi@moh.go.tz  kabla ya Machi 27saa  10 jioni.

Aidha, waombaji wanatakiwa kuambatanisha wasifu wao, nakala za vyeti vya taaluma na  matokeo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha kuhitimu mafunzo kwa vitendo pamoja na cheti cha usajili  kutoka Baraza  madaktari la Tanganyika.

“Tanzania hatuna upungufu wa madaktari isipokuwa Serikali haina uwezo wa kuajiri madaktari wote wanaohitimu, kwa kuwa kwa mwaka kuna wahimu 1200 wa shahada ya kwanza ya udaktari na uwezo wa kuajiri ni 450 tu” alisema Ummy.

Hata hivyo, Waziri Ummy alisema kuwa ajira hizo hazitawahusu watumishi wa umma, hospitali teule za halmashauri na mashirika ya hiari ambao wanalipwa mshahara na serikali. Madaktari watakaokidhi vigezo na sifa watapewa mkataba wa ajira wa miaka miwili.

Nchi ya Kenya inakabiliwa na upungufu wa madaktari kutokana na mgomo ulioanza mwezi Desemba mwaka jana, ambapo madaktari hao wamekuwa wakaidai nyongeza ya mshahara na marupurupu mengine.
 
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akizungumza kuhusu Kutangaza ajira za Madaktari wapatao 500 ambao watakwenda kufanya kazi nchini Kenya. Ajira hizo zitawahusu Madaktari ambao hawajaajiriwa Serikalini(hawapo katika utumishi wa umma au taasisi za serikali. 
 
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo na Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Dkt. Cleopa Mailu Ikulu jijini Dar es Salaam.

UJENZI WA BARABARA ZA JUU UBUNGO, JPM KUWEKA JIWE LA MSINGI.

UBU1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kushirikiana na  Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Jim Yong Kim wanatarajiwa kuweka   jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za juu (Ubungo interchange)  eneo la  Ubungo jijini Dar es Salaam Machi 20 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inasema kuwa mradi wa ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya Ubungo yatagharimu  takribani shilingi bilioni 188.71 ambapo una  lengo kupunguza msongamano wa magari katika barabara za Morogoro, Nelson Mandela na Sam Nujoma.

“Mradi huo ni sehemu ya uboreshaji usafiri Jijini Dar es Salaam yaani (Dar es salaam Urban Transport Improvement Project), utakaogharimiwa kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia na mchango wa Serikali ya Tanzania” .

Aidha, taarifa hiyo ilisema kuwa, mradi huo utahusisha pia awamu ya tatu na ya nne ya ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka (Bus Rapid Transit- BRT), katika barabara ya Nyerere kutoka katikati ya jiji la Dar es Salaam hadi Gongo la mboto na barabara ya Bagamoyo kutoka katikati ya jiji hadi Tegeta.


Friday, March 17, 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AFUTA AGIZO LA KUFUNGA NDOA KWA SHARTI LA CHETI CHA KUZALIWA.

vye
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari Mkoani Dodoma kuhusiana na kufuta agizo lililotolewa jana na Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu Wananchi wanaohitaji kufunga ndoa kuanzia mwezi Mei mwaka huu kuwa na vyeti vya kuzaliwa. Rais Mhe. Dkt. 

Magufuli ameagiza utaratibu wa awali uendelee kutumika kwasababu wananchi wengi wa Tanzania hawana vyeti, hivyo wangekosa haki hiyo ya kufunga ndoa. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana. PICHA NA IKULU.
 vyetin

LUKU KUZIMWA JUMAPILI KWAAJILI YA MAREKEBISHO.

luku_umeme
SHIRIKA la Umeem Tanzania, (TANESCO), linawataarifu
wateja wake na umma kwa ujumla kuwa Jumapili Machi 19, 2017 kuanzia saa 4 usiku.

mfumo wa ununuzi wa umeme kupitia LUKU utazimwa hadi Jumatatu Machi 20, 2017.

Taarifa ya TANESCO iliyotolewa leo Machi 17, 2017 na
kusambazwa kwa vyombo vya habari imesema, lengo kuboresha mfumo huo wa LUKU katika kuhifadhi taarifa za Wateja, (Database).

Taarifa hiyo iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO
Makao Makuu pia imesema uboreshwaji wa mfumo huo utasaidia katika manunuzi ya umeme kupitia LUKU.

Aidha TANESCO imewaomba Wananchi hususan wateja wake ,
kufanya manunuzi ya LUKU ya kutosha kabla ya saa 4 usiku, Jumapili, na
inawaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza.
 

RIDHIWANI KIKWETE AFURAHI BAADA YA KUHOJIWA NA MAMLAKA YA KUPAMBANA NA KUZUIA DAWA ZA KULEVYA.

Ridhiwani-Kikwete
Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ameeleza kufurahishwa kwake baada ya kuhojiwa na Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya nchini.

Mbunge huyo amezungumza hayo jana jijini Dar es salaam baada ya kuhojiwa na Mamlaka hiyo, ambapo alisema roho yake imesuuzika kwani jamii imeamini kwamba hahusiki kwa namna yoyote ile na biashara hiyo haramu.

“nashukuru kwa kuhojiwa huku nimepata nafasi ya kueleza ukweli juu ya jambo hili ambalo lilishaanza kuleta taharuki katika jamii, sasa umma umejua kuwa siuzi wala sihusiki na dawa za kulevya roho yangu imesuuzika “alisema Ridhiwani.

Alisema vita ya dawa ya kulevya ni kubwa na inapaswa kupigwa na kila mmoja ili kuokoa kundi kubwa la vijana ambao wanaathirika kutokana na suala hilo na kwamba kuhojiwa kwake kumemfanya awe na amani.

“naunga mkono vita hii ya dawa za kulevya nchini kwani itasaidia kurudisha nguvu kazi inayopotea kutokana na matumizi ya dawa hizo za kulevya kwa mzazi ambaye mtoto wake ameathirika na matumizi ya dawa hizo anajua uchungu wake na hasara zake”alisema Ridhiwani.

Aidha aliongeza kuwa jamii inapaswa kusimama kwa kauli moja ili kuliokoa Taifa na nguvu kazi inayopotea ili Taifa liwe na vijana wanaojitambua na kutimiza wajibu wao katika kulitumikia taifa.

“Tunapoteza vijana wengi mno, Serikali imeamua kupambana nami kama Mbunge napiga vita uuzaji, utumiaji na usambazaji na kwa kuwa umma ushajua sihusiki na chochote basi naweza kuwa balozi mzuri wa kupiga Vita suala hili .”alisema Ridhiwani.

Akizungumzia suala la marafiki zake kuhusishwa na biashara hiyo haramu alisema kuwa sio marafiki zake bali ni watu anaokutana nao katika maeneo anayotembelea.

“kamishina ameaniambia walioonekana kufanya biashara hiyo sio marafiki zangu bali ni watu ninaokutana nao katika maeneo ninayotembelea wanakuja kunisalimia na kutaka kunizoea kwa ajili kuna watu wanaopenda kutumia watu kama sisi ili kujificha kutokana na maovu wanayofanya”alisema ridhiwani.

Ridhiwani alisema kuwa mchakato huo wa kupambana na dawa za kulenya nchini umekuwa ukiwachanganya wananchi kwani haieleweki ni nani anayehusika na kushugulikia suala hilo.

“huu mchakato umekua ukichanganya kuna watu wanaitwa kwa Kamanda Sirro na wengine wanaitwa kwa Kamishina Sian’ga mfano Msanii Vanessa Mdee ambaye ameitwa kwa Kamanda Sirro badala ya kwa Kamishina Sianga”alisema Ridhiwani.

Alisema kuwa watu wanahoji kwa nini wengine watangazwe hadharani na wengine kuitwa  kimya kimya na ameongeza kuwa ni vyema mamlaka zikajipanga ili kufanikisha vita hii na kufikia malengo yake ya kumaliza tatizo la dawa za kulevya nchini.