Sunday, February 5, 2017

SHEREH ZA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 40 YA CCM MKOA WA DODOMA ZAFANYIKA LEO.

FANA
 Katibu Mkuu wa CCM, Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akihutubia katika sherehe za Kilele cha Miaka 40 ya CCM mkoa wa Dodoma, zilizofanyika leo katika ukumbi wa CCM wa Dodoma Convertion Centre nje kidogo ya mji wa Dodoma.
 

Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula, akihutubia katika sherehe za Kilele cha Miaka 40 ya CCM mkoa wa Dodoma, zilizofanyika leo katika ukumbi wa CCM wa Dodoma Convertion Centre nje kidogo ya mji wa Dodoma. Kulia ni Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
 

Viongozi wakiwa meza kuu baada ya kuwasili ukumbini kuendelea na sherehe hizo
 

 Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole akihamasisha katika sherehe za Kilele cha Miaka 40 ya CCM mkoa wa Dodoma, zilizofanyika leo katika ukumbi wa CCM wa Dodoma Convertion Centre nje kidogo ya mji wa Dodoma.
 

Wanachama wa CCM wakiwa wamefurika ukumbini wakati wa sherehe hizo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akishauriana jambo na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa wakati wa sherehe hizo leo katika ukumbi wa CCM wa Dodoma Convertion Centre nje kidogo ya mji wa Dodoma.
 

Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimia wanacahama wa CCM wakati wa sherehe hizoleo katika ukumbi wa CCM wa Dodoma Convertion Centre nje kidogo ya mji wa Dodoma.

SHERIA ZA HUDUMA ZA HABARI NA KANUNI ZAKE KUTUMIKA RASMI TANZANIA.

AYO LEO 1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye akioongea na Waandishi wa Habari kuhusu siku rasmi ya kuanza kutumika kwa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 pamoja na Kanuni zake za 2017 katika Ukumbi wa Idara ya Habari Bungeni Mjini Dodoma 05/02/2017. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi.
...........................................

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametanga rasmi kuanza kutumika kwa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2017.

Nape Nnauye ametoa taarifa hiyo leo katika ukumbi wa Bunge, Mjini Dodoma alipokuwa akiongea na vyombo vya habari juu ya kuanza kwa sheria hiyo na kanuni zake.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 1 cha Sheria hiyo, ili ianze kutumika rasmi, Waziri wa Habari anatakiwa kuitangaza tarehe ya kuanza kutumika, hivyo napenda kuufahamisha Umma kuwa sheria hii imeanza kutumika tangu Desemba 31, 2016,” alifafanua Nape Nnauye.

Aliendelea kwa kusema kuwa kuanza kutumika kwa sheria hii ni jambo muhimu sana kwa tasnia hiyo kwa sababu inaihamisha taaluma ya habari kutoka fani ambayo mtu yeyote anaweza kujinasibu nayo hadi kuwa taaluma kamili yenye sifa mahsusi, maadili yanayojulikana pamoja na vyombo vya kusaidia kusimamia utekelezaji wake.

Vile vile amesema kuwa, sheria hiyo inaleta mfumo madhubuti wa kulinda haki za wanahabari kukusanya, kuhariri na kusambaza habari zao kwa uhuru.

Pia sheria hiyo imeweka wajibu kwa wale watakaokiuka misingi na maadili ya taaluma hiyo, hivyo ukurasa mpya wa haki na wajibu umefunguliwa kupitia sheria hiyo.

Aidha amesema kuwa, Wizara imechambua maoni mbalimbali kuhusiana na sheria hiyo ambapo moja ya maoni hayo ilikuwa ni kiwango cha elimu cha mtu atakayeruhusiwa kufanya kazi ya taaluma hiyo.

Ambapo wapo  waliopendekeza kiwango cha elimu kiwe cheti, wengine diploma, digrii na hata PhD na wengine walitaka awe mtu yeyote anayejua kusoma na kuandika.

Amesema kuwa Serikali imesimama katikati ya maoni hayo, na sifa ya chini kabisa kwa kuanzia itakuwa ni Diploma ya uandishi wa Habari. Hivyo Serikali imetoa kipindi cha miaka Mitano kuanzia Januari, 01, 2017 kwa waandishi ambao hawana sifa hizo kujiendeleza na kufikia kiwango hicho cha elimu.

Hivyo basi, Idara ya Habari MAELEZO itaendelea kutoa “Press Card” bila kuwabana wanahabari kwa kuangalia vigezo hivi vya kitaaluma bali dhamana ya waajiri wao.

Sheria ya Huduma za Habari, 2016 ilisainiwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli Novemba 16, 2016 na kuchapishwa kwenye gazeti la Serikali Novemba 18, 2016.