Friday, December 16, 2016

WAZIRI JENISTA MHAGAMA ATEM BELEA UJENZI WA SOKO LA NAFAKA KATA YA MAGOMENI BAGAMOYO.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na watu wenye Ulemavu, Mh. Jensta Mhagama kulia, akipokea Taarifa ya ujenzi wa soko la nafaka lililopo Kitongoji cha Maji coast, kata ya Magomeni, Bagamoyo mjini, katikati ni Mhandisi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Henrico Shauri, na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Najid Mwanga.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira  na watu wenye Ulemavu, Mh. Jenista Mhagama amemuagiza Mhandisi wa Halmashuri ya Bagamoyo, Henrico Shauri, kukamilisha  kazi zilizobaki ndani ya wiki mbili ili Soko hilo liweze kufunguliwa mwezi January 2017.

Waziri Jenista Mhagama alitoa agizo hilo  alipotembelea  ujenzi wa soko hilo  ambapo ameridhishwa na shughuli za ujenzi zilivyoenda na kusema kuwa hakuna sababu ya kuchelewa kulifungua soko hilo ili wananchi waweze kufaidika na uwepo wa soko hilo.

Alisema mpaka kufikia Tarehe 30 mwezi Desemba kila kitu kiwe kimekamilika ili mwezi January  liweze kufunguliwa, ambapo waziri mkuu anatarajiwa kulifungua soko  hilo.








Tuesday, December 13, 2016

MKUTANO MKUU WA WANABLOGU TANZANIA 2016 WATOA DIRA YA MAFANIKIO

Disemba 05 na 06 mwaka huu 2016 ulifanyika Mkutano Mkuu wa Waendeshaji/ Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii nchini kupitia umoja wao wa Tanzania Bloggers Network TBN, uliofanyika ukumbi wa PSPF Jijini Dar es salaam.

Siku ya kwanza ilikuwa mahususi kwa ajili ya semina kwa wanablogu hao juu ya namna ya kuendesha mitandao yao kwa ajili ya manufaa ya kijamii na yao pia. Siku ya pili ilikuwa mahususi kwa ajili ya mkutano Mkuu ambapo wajumbe wa mkutano huo waliwachagua viongozi wao ambapo Mwenyekiti wa TBN Joachim Mushi (aliyesimama juu) na wasaidizi wake walisalia katika nafasi zao.
#BMGHabari
Mkutano huo ulifunguliwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas, ambapo alitamka rasmi kwamba serikali inatambua mchango wa wanablogu nchini katika kuipasha jamii habari hivyo itaendelea kushirikiana nao akionya watendaji wa serikali hususani maafisa habari wa mikoni wasiotoa ushirikiano kwa wanablogu hao kuacha mara moja tabia hiyo.

Katika kilele cha mkutano huo, mgeni rasmi alikuwa Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, Nape Nnauye, ambaye alikiri umuhimu wa wanablogu nchini akisema kwamba, watatambuliwa rasmi kupitia kanuni za sheria mpya ya vyombo vya habari nchini ya mwaka 2016 na kwamba watapewa kadi za wanahabari (Press Card) ili kuwasaidia katika utendaji wao wa kazi.

Kauli iliyowafurahisha wengi ni ile ya Waziri Nnauye aliyowakaribisha wadau mbalimbali ili kufanikisha utoaji wa tuzo kwa wanablogu kwa mwaka ujao 2017 akisema wanafanya kazi kubwa hivyo ni vyema kutambua mchango wao kupitia tuzo.

BMG inawapongeza wote waliofanikisha mkutano huo, ikiwemo Bank ya NMB kwa ufadhiri wake, NHIF, PSPF, Kampuni ya bia Serengeti, Cocacola na TANAPA. Kwa pamoja tuienzi kaulimbiu ya mkutano huo, “Mitandao ya Kijamii ni Ajira, Itumike kwa Manufaa”.
 
Kutoka kushoto ni Katibu wa TBN, Khadija Kalili, Mwenyekiti wa TBN, Joachim Mushi, Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dk. Hassan Abbas na Meneja Mwandamizi wa Amana Huduma za Bima na Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili na mjumbe wa kamati tendaji TBN, Klantz Mwantepele.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo. Katikati ni Mwenyekiti wa TBN, Joachim Mushi na kushoto ni Katibu wa TBN, Khadija Kalili.
 Mwanablogu akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wenzake

Saturday, December 10, 2016

WAHAMIAJI HARAMU 81 WAKAMATWA BAGAMOYO LEO TAREHE 10 DESMBA 2016.


Raia wa Ethiopia  81 wamekamatwa Bagamoyo wakiwa katika katika harakati za  kusafirishwa kupitia  usafiri  wa Baharini.

Akitoa Taarifa  kwa waandishi  wa Habari  mkuu  wa wilaya ya  Bagamoyo,  Alhaji, Majid Mwanga, alisema watu hao  wamekamatwa kufuatia  ushirikiano na raia wema  ambao  walitoa taarifa  polisi  na kufanikisha  kuwakamata  watu hao  ambao  wameingia nchini bila ya  kufuata sheria.

Alisema  tukio hilo limetokea  leo Tarehe  10  Desemba,  kitongoji  cha    Mjimpya kata ya  Kisutu katika eneo la kingani ambapo watu hao walikutwa hapo.

Alisema vyombo vya ulinzi  wilayani  Bagamoyo vimejipanga kukomesha  vitendo vyote  vya  kihalifu ikiwa ni  pamoj a upitishaji  wa biashara za  magendo na  wahamiaji  haramu.

Aidha,  aliwataka wananchi  kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na Usalama  ili kufichua  maovu  mbalimbali yanayofanyika katika wilaya ya  Bagamoyo.

Akizungumzia  madhara ya  kuwaficha  wahamiaji haramu  ni  pamoja  na kukithiri kwa vitendo vya  kihalifu na kuambukizana  magonjwa kutokana na  kuwa waliongia bilaya   vibali hawakupitia kwenye ngazi za kuwahakiki ikiwa wana  magonjwa ya  kuambukiza au  la.
 
Mmoja wa  wahamiaji hao Shemsadin Wesorow, akizungumza kwa niaba ya  wenzake alisema  wametokea katika  Nchi ya Ethiopia  lengo  likiwa ni  kwenda  Afrika ya  Kusini  kufanya  kazi na kwamba hawakutoroka kutoka  kwao.

Alisema  alipigiwa simu  na  kaka yake ambae anamiliki Duka  kubwa huko  Afrika ya  kusini  ili aende  nae  akapate  kazi.

Akizungumzia ni kwa namna gani  wangeweza kuishi  huko hali ya wako  wengi,  Shemsadini  alisema kila mmoja kati yao ana ndugu  huko kwahiyo isingekuwa tabu  kuishi huko.

Alipoulizwa kuhusu idadi kamili  katika msafara wao alisema  wametoka 93 lakini waliokamatwa na  polisi ni 81 tu na 12 waliobaki wamekimbilia vichakani.

Aidha, ameiomba  serikali ya Tanzania iwasaidie  kurudi  nchini kwao  na kwani baadhi yao wamechoka kwa njaa huku wengine  wakiwa wanaumwa bila ya kupata matibabu  kutokana  na  mazingira ya kujificha  katika safari yao.





Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid  Mwanga.