Tuesday, October 11, 2016

MKUTANO WA PILI WA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAFU NGULIWA LEO ZANZIBAR.

she2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Daniel F.Kigeda wakati alipofika kuufungua Mkutano wa Pili wa kikao cha tano cha Bunge la tatu la Afrika Mashariki uliofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi “B”Unguja,[Picha na Ikulu.] 11/10/2016.
 jia02
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Daniel F.Kigeda mara alipowasili katika  ufunguzi wa  Mkutano wa Pili wa kikao cha tano cha Bunge la tatu la Afrika Mashariki leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi “B”Unguja,(katikati) Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe,Zubeir ali Maulid,[Picha na Ikulu.] 11/10/2016.
 she1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Daniel F.Kigeda(kulia) na Spika wa Baraza l;a Wawakilishi Zanzibar Mhe,Zubeir Ali Maulid (kushoto) baada ya Kuufungua Mkutano wa Pili wa kikao cha tano cha Bunge la tatu la Afrika Mashariki uliofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi “B”Unguja,[Picha na Ikulu.] 11/10/2016.
 jia1
Baadhi ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipokuwa akitoa hutuba yake katika  ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa kikao cha tano cha Bunge la tatu la Afrika Mashariki uliofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi “B”Unguja,[Picha na Ikulu.] 11/10/2016.
 jia2
Baadhi ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipokuwa akitoa hutuba yake katika  ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa kikao cha tano cha Bunge la tatu la Afrika Mashariki uliofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi “B”Unguja,[Picha na Ikulu.] 11/10/2016.
 jia3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  alipokuwa akitoa hutuba yake katika  ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa kikao cha tano cha Bunge la tatu la Afrika Mashariki uliofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi “B”Unguja,[Picha na Ikulu.] 11/10/2016.
 jia4

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipokuwa akitoa hutuba yake katika  ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa kikao cha tano cha Bunge la tatu la Afrika Mashariki uliofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi “B”Unguja,[Picha na Ikulu.] 11/10/2016. 
 jia5

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto mbele) Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Daniel F.Kigeda(katikati mbele) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif AliIddi (kulia mbele) na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe,Zubeir Ali Maulid,wakisimama pamoja na Wabunge wa Bunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,wimbo wa Taifa nchi za Jumuiya ukipigwa baada ya kumalizika ufunguzi wa  Mkutano wa Pili wa kikao cha tano cha Bunge la tatu la Afrika Mashariki leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi “B”Unguja,[Picha na Ikulu.] 11/10/2016.
 jia6

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mbunge Shrose  Bhanji mara baada ya    ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa kikao cha tano cha Bunge la tatu la Afrika Mashariki uliofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi “B”Unguja,[Picha na Ikulu.] 11/10/2016.
 jia7

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wabunge mbali mbali wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa kikao cha tano cha Bunge la tatu la Afrika Mashariki uliofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi “B”Unguja,[Picha na Ikulu.] 11/10/2016.


SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI, LHRC YATOA MAONI.

Mkurugenzi mtendaji Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu,(LHRC) Dr. Helen Kijo-Bisimba,
 .............................................
Ndugu wanahabari.

Leo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinaungana na dunia nzima kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, siku ambayo ilipitishwa na  Umoja wa mataifa mnamo  Oktoba 11, 2011. 

Kauli mbiu ya kitaifa kwa mwaka huu ni ‘‘Mimba na ndoa za Utotoni zinaepukika, Chukua hatua kumlinda mtoto wa kike’’. 

Hivyo basi katika kuadhimisha siku hii Kituo kimeangazia mtoto wa kike hapa Tanzania na changamoto anazokumbana nazo. 

Kwa mujibu wa takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, idadi ya watoto wa kike kati ya umri wa miaka 0-17 hapa Tanzania ni  11,263,891 idadi ambayo ni sawa na asilimia 48.8 ya watoto wote chini ya miaka 17, ambapo Tanzania bara  kuna watoto wa kike 10,943,846 na Tanzania visiwani idadi  yake ni laki 320,045.

Hivyo basi nusu ya idadi hii ni wanawake na watoto  ikilinganishwa na idadi ya watanzania wote ambao ni milioni 44,928,923 ambapo  kati yao wanawake ni milioni 23,058,933.
 
Inasikitisha kuona kuwa mtoto wa kike hapa nchini bado amekuwa akikabiliwa na changamoto nyingi na cha kusikitisha zaidi mtoto huyu anaanza kubaguliwa kuanzia katika ngazi ya familia. 
 
Katika familia nyingi za kitanzania mtoto wa kike amekuwa akikosa fursa ya kupata Elimu ukilinganisha na mtoto wa kiume na katika mazingira mengine wazazi wamediriki hata kuwaozesha watoto wao wa kike kwa ajili ya kupata fedha ya kusomesha watoto wa kiume. 

Ukiangalia pia katika suala zima la Elimu ni ukweli usiofichika kuwa idadi ya wasichana wanaoshindwa kumaliza masomo kwa sababu za kupata mimba imekuwa ikiongezeka.

 Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la watoto duniani UNICEF kumekuwa na ongezeko la mimba mashuleni kutoka asilimia 23 hadi 26 yaani takribani watoto wa kike 8000 hapa Tanzania kila mwaka hukatisha masomo kwa ajili ya ujauzito. 

Vile vile idadi ya watoto wa kike ambao wamekuwa wakimaliza Elimu ya msingi lakini kutokupewa nafasi ya kujiendeleza kielimu hata pale wanapokuwa wamefaulu nayo pia imekuwa ikiongezeka na badala yake mabinti hawa wamekuwa wakilazimika kuingia katika ndoa katika umri mdogo.

Ndugu wanahabari, Hali hii ya Watoto wakike kutokupata fursa ya elimu husababisha ongezeko kubwa la watoto wa kike wanaosafirishwa kutoka vijijini na kuletwa mijini kwa minajili ya kuja kuendelezwa kielimu na matokeo yake mabinti hawa wamejikuta katika wakati mgumu kwa kufanyishwa kazi za ndani bila malipo stahiki na wakifanyiwa vitendo vingi vya kikatili na vya kuwadhililisha.

Hali hii imepelekea mabinti wengine kutoroka kutoka kwa waajiri wao na kuanza kuishi mtaani na hivyo kurubuniwa na kujiingiza katika biashara za ngono na wengine hata madawa ya kulevya.

Tumeendelea pia kushuhudia kuongezeka kwa vitendo vya ukatili wa kingono kama ubakaji na ulawiti kwa Watoto wa kike na cha kusikitisha zaidi vitendo hivi vimekuwa vikifanywa na Ndugu wa karibu sana wa Watoto hawa wakiwemo wazazi, walezi, majirani na hata walimu huko mashuleni. 

matukio haya yamekuwa hayafikishwi Katika vyombo vya Sheria kwani mengi huzungumzwa kifamilia na kuwaacha watuhumiwa wakiendelea na maisha yao.

Ndugu wanahabari, Tanzania pia ni nchi moja wapo yenye idadi kubwa ya ndoa za utotoni kwa takribani  ya asilimia 35 watoto wa kike hapa nchini huozeshwa nchini ya umri wa miaka 18 na hivyo kukatishwa ndoto zao za kujiendeleza kielemu na hata ustawi mzima wa maisha yao.

Inasikitisha zaidi kuona pia pamoja na juhudi mbalimbali za utetezi na ushawishi wa wanaharakati katika kupinga vitendo hivi viovu na mila kandamizi bado Ukeketaji umekuwa ni tatizo kubwa sana hapa nchini. 

Kwa mujibu wa takwimu za Viashiria vya Idadi ya watu na afya 2010, asilimia 14.6% ya wanawake Tanzania wamekeketwa na wengi wao ni watoto wa kike. 

Utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa mbinu mpya zimekuwa zikibuniwa ikiwemo  kukeketa watoto mara wanapozaliwa.

Vilevile, kwa mujibu wa taarifa ya haki za Binadamu ya mwaka 2015 inayotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kila mwaka ongezeko la matukio ya Ukatili kwa watoto ikiwemo watoto wa kike kupewa adhabu kali ambazo hazilingani na makosa waliyoyafanya, mfano unakuta mtoto anachomwa mikono moto kwa kosa la kuunguza mboga.

Kwa kifupi watoto wa kike wanapata athari mbalimbali ikiwemo;
1.      Kuendelea kudidimiza nafasi ya mwanamke katika Jamii na taifa zima kwa ujumla na kuendeleza mfumo dume kwani ukatili mwingi huanzia katika ngazi ya familia

2.      Kutokuendelezwa kielimu kwa mtoto wa kike na hii hupelekea kuendelea kuwa na idadi kubwa ya Wanawake ambao hawana Elimu na hivyo kuendelea kuwa tegemezi kwa wanaume na pia kushindwa kujikwamua kiuchumi.

3.      Idadi kubwa ya athari za kiafya zinazowapata watoto wa kike kwa ajili ya kujifungua katika umri mdogo ambayo husababisha wengine kupoteza maisha, kupatwa na fistula na maambukizi ya virusi vya ukimwi pamoja na magonjwa mengine ya zinaa.

4.      Malezi duni ya watoto kwa kuwa watoto hawa wanakuwa bado ni wadogo kuweza kukabiliana na jukumu kubwa la malezi na matunzo ya familia.

5.      Kuendelea kuongezeka kwa Ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwani watoto hawa mara nyingi huolewa na watu waliowazidi umri sana na hivyo kutokuwa na maamuzi yoyote katika nyumba.

Hivyo basi tunapendekeza yafuatayo:
1.      Katika ngazi ya familia wazazi na walezi kuthamini na kuwajali watoto bila ubaguzi wa jinsi zao. Watoto wote wapewe fursa sawa kielimu na kujiendeleza kimaisha. 
Wazazi kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vyote vya Ukatili hasa Ukatili unaoanzia majumbani,sambamba na hilo kutoa taarifa za matukio ya Ukatili wanayofanyiwa watoto na sio kutatua matatizo haya katika ngazi ya familia ilihali haki ya mtoto inapotezwa.

2.      Wito kwa Jamii kuwajibika katika kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vyote vya Ukatili. Kuthamini nafasi ya kila mtoto na kuona mtoto wa mwenzako ni wa kwako; pia kutoa taarifa ya matukio ya Ukatili katika maeneo wanayoishi na sio kufumbia macho na kuwaficha waovu.

3.      Serikali kuhakikisha kuwa sheria zilizopo zinasimamiwa na zinatekelezwa pale zinapovunjwa kwa kuweka mifumo iliyowazi na rahisi ya kupata na kufuatilia haki. 

Vile vile kubadilisha sheria ambazo bado zimekuwa ni kandamizi kwa mtoto wa kike ikiwemo Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 inayoafiki mtoto wa kike kuolewa katika umri wa miaka 15.

 Serikali itekeleze agizo lilitolewa na Mahakama Kuu Julai 8 2016 la kubadili kifungu na 13 cha sheria ya ndoa 1971 juu ya ndoa za utotoni
4.      Serikali kwa kupitia taasisi zake kama polisi na mahakama kuhakikisha kuwa Mashauri yanapolekwa Mahakamani yanasikilizwa bila vikwazo na kutolewa maamuzi kwa wakati stahiki maana ‘justice delayed is justice denied’ – ‘kuchelewesha haki ni kunyima haki’.

5.      Wito kwa vyombo vya habari kuendelea kutoa taarifa ya matukio ya Ukatili wanayofanyiwa watoto ili wale wanaofanya vitendo hivi waaibishwe na waadhibiwe kwa mujibu wa sheria; tunavitaka vyombo vya Habari visiishie tu kuripoti matukio haya pindi yanapofanyika bali hata kuendelea kufuatilia mashauri yaliyopo mahakamani ili kusaidia mashauri haya yafanyiwe kazi kwa wakati.

6.      Pamoja na hilo tunaviomba vyombo vya habari kuwa makini jinsi wanavyoripotia matukio haya ya Ukatili kwa watoto kwani utoaji wa taarifa hizi wakati mwingine umekuwa pia ukiendelea kuwavunjia haki watoto hawa kwa kutozingatia sheria inayotaka utoaji wa taarifa za watoto kutunza majina halisi ya watoto na hata sura zao.

7.      Na mwisho kabisa tunaomba viongozi wetu katika ngazi zote za kijamii na hata kitaifa kuibeba ajenda ya haki za watoto na hususani haki za watoto wa kike kama ajenda ya kitaifa ili kuhakikisha wanalindwa dhidi ya vitendo viovu na wana mazingira salama ya kukua na kuwa watu wema na mustakabali mzuri wa maisha yao ya sasa na ya baadae.

Tunawashukuru sana.

Wasalaam, Kituo cha Sheria na Haki za Binada


Dr. Helen Kijo-Bisimba Mkurugenzi Mtendaji

MKAZI WA KANYERERE MKOAN MWANZA ANASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MTOTO WAKE WA MIAKA 10

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 11-10-2016.
 
JESHI LA  POLISI MKOANI MWANZA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA PAUL JONES KINA, MIAKA 34, MZANAKI, MWENDESHA PIKIPIKI (BODABODA) MKAZI WA MTAA WA KANYERERE KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MTOTO WAKE WA KUMZAA JINA LINAHIFADHIWA, MWENYE UMRI WA MIAKA 10, MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE SHULE YA MSINGI TAMBUKA RELI.

TUKIO  HILO LIMETOKEA TAREHE 01.10.2016 MAJIRA YA SAA 23:00HRS KATIKA MTAA WA KANYERERE KATA YA BUTIMBA WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA,  BAADA YA KUPATIKANA KWA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA.

INADAIWA KUWA MTUHUMIWA TAJWA HAPO JUU ALIKUWA NA KAWAIDA (TABIA) YA KUMBAKA BINTI YAKE KWA MUDA MREFU, NDIPO WATU WAKARIBU MAJIRANI WALIWEZA KUTOA TAARIFA POLISI KUHUSIANA NA KITENDO HICHO, AIDHA BINTI ALIWEZA KUPELEKWA HOSPITALI KWA AJILI YA UCHUNGUZI NDIPO IKATHIBITIKA KWAMBA NI KWELI AMEBAKWA.

MTUHUMIWA WA KITENDO HICHO CHA UBAKAJI AMEKAMATWA YUPO NDANI, TAYARI JALADA LAKE LA MASHITAKA LIMEPELEKWA KWA MWANASHERIA WA SERIKALI, HIVYO MUDA WOWOTE KUANZIA HIVI SASA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, ILI HATUA ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAKE.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA, AKIWATAKA WATU WOTE WENYE KESI ZA AINA KAMA HIYO ZA KUBAKWA AU UNYANYASAJI WA KIJINSIA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI NA MAHAKAMA.

AIDHA, AMEWAKUMBUSHA MASHAHIDI WA KESI ZA AINA KAMA HII KUACHA TABIA YA KUMALIZANA KIENYEJI NYUMBANI HADI KUPELEKEA KESI NYINGI KUHARIBIKA BALI MASHAHIDI WANATAKIWA WAKATOE USHAHIDI MAHAKAMANI ILI HAKI IWEZE KUPATIKANA.

IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA