Wednesday, September 14, 2016

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI AFANYA MKUTANO NA WAKUU WA VITENGO NA IDARA

aki1
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza na wakuu wa Idara na vitengo  vilivyopo chini ya wizara  wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya kiutendaji katika wizara hiyo.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.Mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.aki2

Wakuu wa Idara na Vitengo wa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, wakati wa mkutano wa kujadili masuala  ya kiutendaji katika wizara  hiyo. Mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.aki3

Viongozi kutoka Idara za Wizara ya Mambo ya Ndani, kutoka kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Minja, Kamishna wa Operesheni Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Rogasius Kipali na Kamishna wa Fedha Jeshi la Polisi, Albert Nyamhanga, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara, Meja Jenerali Projest Rwegasira(hayupo pichani) wakati wa mkutano wa kujadili masuala  ya kiutendaji katika wizara hiyo. Mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

DC KIBAHA AWAPA SIKU 30 WAFUGAJI WALIOPO KATA YA KWALA KUONDOKA ENEO HILO.

images

Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

MKUU wa wilaya ya Kibaha,mkoani Pwani ,Assumpter Mshama ametoa mwezi mmoja kwa wafugaji wa kata ya Kwala kuondoka,katika kata hiyo kwani hakuna eneo lililotengwa kwa ajili yao.

Aidha alisema wafugaji waliopo kihalali katika maeneo mengine ya wilaya hiyo wanatakiwa kuheshimu wakulima na endapo yupo atakaeingiza mifugo katika shamba la mkulima atatakiwa kulipa ng’ombe kulingana na hasara iliyopo.

Assumpter ametoa pia siku 30 kwa wafugaji waliopo kisheria kuweka alama kwenye ng’ombe zao huku akivitaka vijiji vitenge maeneo ya wakulima na wafugaji.

Aliyasema hayo wakati akizungumza na pande hizo mbili ,katika ziara yake aliyoianza kutembelea vijiji na maeneo yenye migogoro ya wakulima na wafugaji wilayani hapo.

Akizungumza kwenye ziara yake Dutumi na Kwala ,alisema maamuzi hayo yatakuwa dawa na muarobaini wa tatizo hilo.

Assumpter alisema kwasasa barua rasmi zinaandaliwa kwa ajili ya kuwapatia wafugaji hao ikiwa ni taarifa na kumbukumbu.

Aliwataka maafisa mifugo kuitisha mikutano ya wananchi kutunga sheria ndogondogo zitakazobana makundi hayo.

Alisema serikali haiwezi kuvumilia kuona kundi moja linaumiza vichwa vya watu na kujigeuza wababe kuvunja amani na kujenga hofu ndani ya jamii.

“Kuanzia sasa ng’ombe ni halali ya mkulima ,ama watakaokamatwa  watauzwa na mfugaji kuchukuliwa hatua “
“Wasithubutu kunijaribu,najua wafugaji wanamtandao ndio maana wanaingia kila kukicha sasa kwa Kibaha basi inatosha ,sitaki kuona wafugaji wapya”alisema Assumpter.

Mkuu huyo wa wilaya alieleza kuwa yeyote mwenye kosa ni lazima achukuliwe hatua kama kuna mfugaji hata mkulina anamkosea mwenzie.
Assumpter alisema mfugaji atakaekamatwa ng’ombe zake na kuziacha kwa siku 7  watatakiwa kupigwa mnada.

Alieleza kuna kila sababu ya kuheshimiana na kuishi kwa amani kwa pande hizo zote mbili pasipo kujipa hofu na kutishiana amani bila msingi.
Akiwa Dutumi Assumpter alitoa siku saba kwa wafugaji walioingia bila utaratibu kurudi makwao walipotokea na kupisha ardhi ya mji huo.

Alisema utajiri wa wafugaji usiwe chanzo cha kudhalilisha wakulima ambapo serikali imeshachoshwa na wimbo wa migogoro hiyo usiokwisha.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha,Tatu Selemani aliasa baina ya makundi hayo kuheshimu mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Alisema kwa upande wa kata ya Kwala hakuna eneo la wafugaji hivyo ni lazima wahame.

Tatu alisema,hakuna wafugaji waliopokelewa katika kata hiyo na kwamba wahamishe mifugo kwenye mikoa na maeneo mengine.

Alifafanua kuwa Dutumi kuna ng’ombe 4,195 na kulitengwa mpango wa matumizi bora ya ardhi kuaniza mwaka 2014 ambao uataisha mwaka 2024.  
Mfugaji kutoka Dutumi Samwel Robert ,alisema ng’ombe wengi wametokea ngambo na ni wafugaji wavamizi.

Alisema kundi hilo linatokea Kisarawe,wasukuma na Morogoro –Kilosa kwahiyo serikali iangalie hilo.

Tuesday, September 13, 2016

CHANGIA MAAFA KAGERA KUPITIA AKAUNTI NAMBA HIZI.

WAZIRI MKUU APOKEA ZAIDI YA BIL. 1.4 KWAAJILI YA TETEMEKO LA ARDHI LA KAGERA.

ub2
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Wafanyabishara na Mabalozi wa Nchi Mbalimbali hapa nchini kuwaomba wachangie katika kujenga na kukarabati miundombinu iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Alikutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 13, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
..............................


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea michango wa zaidi ya sh. bilioni 1.4 kutoka kwa mabalozi wa nchi za nje nchini Tanzania na Jumuia ya Wafanyabiashara wa Kitanzania kwa ajili ya kusaidia wananchi waliothirika na tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.

Tetemeko hilo lilitokea Jumamosi, 10 Septemba, 2016 na kusababisha vifo vya watu 17 hadi leo na wengine 253 kujeruhiwa. Pia limesababisha maelfu ya wananchi kukosa makazi baada ya nyumba 840 kuanguka na nyingine 1,264 zikipata nyufa yakiwemo majengo 44 ya taasisi mbalimbali za umma.

Akizungumza katika hafla ya uchangishaji fedha kwa ajili ya kusaidia wahanga hao leo (Jumanne, 13 Septemba, 2016) Waziri Mkuu amewashukuru kwa michango yao ya fedha na vifaa vya ujenzi ikiwemo mifuko 2,800 ya saruji. Amesema tetemeko hilo ni kubwa na halijawahi kutokea nchini.

Amesema tetemeko hilo limesababisha Serikali kuzifunga shule zake mbili za sekondari za Nyakato na Ihungo kati ya nne zilizoathirika vibaya na tetemeko hilo.

“Serikali itajitahidi kuhakikisha inarejesha miundombini iliyoharibiwa na tetemeko hilo katika kipindi kifupi ili wanafunzi na wananchi wengine waweze kuendelea na shughuli zao za kawaida,” amesema.

Waziri Mkuu amesema katika kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa haraka tayari Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Muhagama yuko mkoani Kagera akiongoza kitengo cha maafa kufanya thamnili kujua athari zilizosababishwa na tetemeko hilo.

Mawaziri wengine walioko mkoani Kagera wakiendelea kufanya tathmini hiyo ni pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako.

Amesema Kamati ya Maafa ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Kamati ya Maafa ya mkoa wa Kagera imefungua akaunti maalumu katika benki ya CRDB kwa ajili ya kupokea michango kutoka kwa watu mbalimbali. Namba za akaunti hiyo ya Kamati ya Maafa ya Kagera ni CRDB 0152225617300.

Pia Waziri Mkuu amewapongeza na kuwashukuru waheshimiwa Wabunge kwa kuamua kutoa posho zao za kikao cha leo kwa ajili ya kuchangia wahanga wa tetemeko hilo na kuwaomba wananchi wengine kujitokeza na kutoa michango yao.

Wakati huo huo viongozi wa makampuni ya mafuta ya GBP, Oil Com na Moil wameahidi kujenga shule mbili za Nyakato na Ihungo ambazo sehemu kubwa ya miundombinu yake imeharibika vibaya. Shule hizo zitajengwa katika kipindi cha siku 30.

Hafla hiyo iliyoongozwa na Waziri Mkuu ilihudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Suzan Kolimba na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi, Dk. Aziz Mlima.