Monday, September 12, 2016

SWALA YA EID BAGAMOYO, ILIYOSWALIWA BONG'WA.

Waislamu mjini Bagamoyo, wakiswali swala eid katika viwanja vya  Istqaama  leo.

Waislamu wilayani Bagamoyo wametakiwa kusherehekea siku kuu yaEidi kwa utulivu na amani huku wakizingatia mafundisho ya  mtume Muhammad Swalallaahu Alayhi wa Salaam.

Wito huo umetolewa na katibu wa baraza la Ulamaa la Taasisi ya SirajulMunir Islamic Cente (SIMIC) ya mjini Bagamoyo, alipokuwa akitoa  hutuba ya swala yaeidi iliyoswaliwa  katika  viwanja vya  masjidi Istiqaama eneo la Bong'wa Bagamoyo mjini.

Alisema uislamu umefundisha  m ichezo mbalimbali, hivyo ni vyema  katika ya sikukuu waislamu wakifanya  michezo mbalimbali iliyoruhusiwa katika uislamu.

Aliongeza  kwa  kuwataka wazazi wawape watoto mafundisho ya namna ya  kufurahi katika siku kuu ili kuepuka katika kufanya  mambo yanayokwenda kinyume na uislamu ikiwa ni  pamoja na aina gani yamavazi yanayopaswa  kwa  watoto pamoja  sehemu zinazofaa kwa  watoto kutembelea.

Alisema  katika sikukuu hii waislamu wanakumbuka historia ya nabii Ibrahim  ambae  alionyesha umahiri m kubwa katika kumtii mwenyeziMungu yeye na familia yake, hali iliyopelekea kutii  amri hata ya  kumchinja  mwanae.

Aliendelea kusema  kuwa, uislamu katika kugawa haki na majuku kwa watu umezingatia uadilifu na sio usawa ieleweke kwamba  katika uislamu uadilifu umepewa umuhimu wake na hii ni  pamoja na kufuata  sheria zote za  mwenyezimungu.

Waislamu wa Bagamoyo na Tanzania kwa ujumla leo wanaungana na waislamu duniani kote kushereheka siku kuu ya  kuchinja ambayo inaadhimishwa mara baada ya kukamilisha ibada ya hija ambayo ni nguzo ya tano katika uislau inayotekelezwa  kila mwaka huku Maka SaudiArabia.




Sunday, September 11, 2016

RAIS DKT.MAGUFULI AAHIRISHA ZIARA NCHINI ZAMBIA

mag
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha ziara ya siku tatu nchini Zambia ambapo pamoja na mambo mengine alikuwa ahudhurie sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe.Edgar Chagwa Lungu ili aweze kushughulikia tatizo la tetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya watu 16 ,mamia wakiwa wamejeruhiwa na nyumba kadhaa kubomolewa mkoani Kagera.

Kufuatia kuahirisha ziara hiyo Mheshimiwa Rais Dkt.Magufuli amemtuma Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kumuwakilisha katika sherehe hizo za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu
Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu zinatarajiwa kufanyika keshokutwa tarehe 13 Septemba, 2016 katika Jiji la Lusaka.

Jaffar Haniu
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi
Dar Es Salaam
11 Septemba, 2016