Sunday, August 7, 2016

WANAHABARI WATAKIWA KUANDIKA HABARI ZA UHAKIKA.

LOI2

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akielezea jambo mara baada ya kutia saini katika kitabu cha wageni ofisini kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Padre Raymond Sabas (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari Kanisani jana Jijini Dar es Salaam. Kulia Mwenyekiti wa Bodi ya Tumaini Media Padre Joseph Matumaini.
 .............................................................................


Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel amewataka wanahabari nchini kuandika na kuripoti habari  kwa jamii ambazo zina ukweli na zinazotoa elimu kwa jamii kuhusu maendeleo.

Prof. elisante Ole Gabriel ameyasema hayo wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Upashanaji Habari Kanisani  yaliyofanyika jana Kurasini Jijini Dar es Salam ambapo amesema wanahabari nchini wanapaswa kutumia vyema taaluma yao na maadili ya uandishi wa habari.

Aidha Katibu Mkuu huyo amesema kuwa ni vyema wanahabari kwenda na mabadiliko ya teknolojia kwa kuitumia vizuri  katika masuala ya kutoa habari kwa jamii bila kuathiri Utamaduni na amani iliyopo nchini.

“Kuweni makini katika matumizi ya teknolojia katika kile mnachotaka kuandika ili mlinde Utamaduni wetu,yale yanayokwenda kwa jamii muyachuje na lazima muyajue vizuri na kwa usahihi ili kuepuka matokeo hasi kwa jamii”.Alisema Prof.Elisante Ole Gabriel.

Kwa upande wake Padri Joseph Matuamaini ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tumaini Media amesema kuwa vyombo  vya habari lazima viwe na Sera na Dira ambayo inaeleweka kwa watazamaji ili iwe rahisi kuelewa ujumbe wanaoufikisha.

“Vyombo vya habari vya kidini kuweni na huruma kama Baba wa Mbinguni ,lazima mufikishe ujumbe kwa jamii kuhusu Utukufu wa Mungu na umuhimu wa amani ili kuondoa hofu kwa wananchi”.Alisema Padri Matumaini.

Padri Mtumaini ameongeza kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa Serikali kuhamia Dodoma ili kuondoa hofu iliyoingia moyoni mwao kuwa itadhorotesha maendeleo.

Rais alipotangaza Serikali kuhamia Dodoma wananchi waliingiwa na hofu,lakini hakuna sababu ya kuogopa bali tuamini kuwa ni hatua nzuri ya kuleta maendeleo na kutimia kwa ndoto ya muda mrefu ya Taifa letu.

Maadhimisho hayo  yalibeba pia ujumbe wa Baba Mtakatifu Papa Francis mabao umesisitiza namna bora ya kutumia mawasiliano  katika kutangaza mambo mazuri ya Mungu kwa jamii.
 LOI3

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akisisitiza jambo alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari iliyofanyika katika ukumbu wa Ofisi za Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki  jana Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa TEC Padre Raymond Saba, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya TEC Bw. Bernard James na Mwenyekiti wa Bodi ya Tumaini Media Padre Joseph Matumaini.

 LOI7

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akisalimiana na Mke wa Waziri Mkuu mstaafu Mama Regina Lowassa wakati wa maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari Kanisani iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki  jana Jijini Dar es Salaam.
 LOI8

Mwenyekiti wa Bodi ya Tumaini Media Padre Joseph Matumaini akifafanua jambo alipokuwa akiwasilisha ujumbe wa Baba Mtakatifu Papa Fransisko kuhusu maadhimisho ya 5O ya siku ya Mawasiliano duniani jana Jijini Dar es Salaam.
 LOI10

Baadhi ya washiriki katika maadhimisho ya 50 ya Upashanaji Habari Kanisani yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) wakifuatilia mada zilizowasilishwa katika maadhimisho hayo jana Jijini Dar es Salaam.

MADIWANI CHALINZE WAJIPANGA KULETA MAENDELO KATIKA HALMASHAURI HIYO MPYA.

Wa kwanza kushoto ni Diwani wa viti maalum Tarafa ya Miono, Mh. Sijali  Mpwimbwi, wa pili kushoto ni Diwani wa viti maalum Tarafa ya Chalinze, Mh. Mwanakesi Madega, wa tatu ni Diwani  wa kata  ya Kimange, Mh. Hussein Hading'oka, anaefuata ni Diwani viti maalum Tarafa  ya Kwa Luhombo Mh. Tunu Mpwimbwi, kutoka kulia wa kwanza ni Diwani wa kata ya Msata, Mh. Cham Semiono wa pili kulia ni Diwani wa  kata  ya Lugoba, Mh. Rehema  Mwene na wa tatu kulia ni Diwani wa kata ya Kibindum,Mh. Mkufya  Ramadhani Mkufya.
.....................................................................................
Halmashauri mpya ya Chalinze imejipanga kusimamia Bajeti ya Halmashauri hiyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha fedha zilizotengwa  kwaajili  ya wanawake na vijana zinafika kwa walengwa
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa  Halmashauri  ya Chalinze Mh. Saidi Zikatimu wakati  wa kikao cha kufunga taarifa ya robo ya nne ya mwaka 2015/16. katika ukumbi wa Halmashauri  ya Chalinze.

Halmashauri ya chalinze ambayo imeanzishwa kutoka Halmashauri ya Bagamoyo, imemaliza bajeti iliyoandaliwa na Halmashauri ya Bagamoyo ambapo sasa Chalinze itaanza bajeti inayojitegemea kama Halmashauri mpya na hivyo kufanya wilaya ya Bagamoyo kuwa na Halmashauri mbili, Halmashauri ya Bagamoyo na Halmashauri ya Chalinze ndni ya wilaya moja ya Bagamoyo.

Akielezea mikakati ya Halmashauri hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze  Mh. Saidi Zikatimu alisema Halmashauri ya Chalinze kupitia Madiwani wake imejipanga  kuhakikisha Bajeti iliyopangwa inatekelezeka kwa kusimamia vizuri mapato na matumizi ya Halmashauri hiyo.

Aidha, alisisitiza kuwa madiwani wa Halmashauri hiyo mpya, wamejipanga kusimamia  utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Halmashauri na kuongeza kuwa kila fedha itapelekwa kwenye  matumizi yake yaliyopangwa na si vinginevyo.

Alisema, katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao  kwa maslahi ya wananchi, Baraza hilo  litahakikisha fedha zote zilizotengwa kwaajili ya wanawake na watoto zinafika kwa walengwa.

Aidha, Mwenyekiti huyo huyo wa halmashauri alimshukuru Mbunge wa Jim bo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete, kwakuwa fedha za mfuko wa jimbo  zimeshafika kwenye vikundi na kuanza kuzifanyia kazi.

Katika kikao hicho cha Baraza la Madiwani piya wamejadili uhaba wa walimu uliopo katika shule za Halmashauri hiyo ikiwa ni  pamoja kuwapa uhamisho bila ya sababu za msingi ambapo wamemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kutoa taarifa kwa baraza la madiwanni kwa mabadiliko ya walimu ili kwa pamoja waweze kuangazia sehemu yenye uhitaji wa walimu na kuepuka walimu kuchagua sehemu za mjini na kuacha shule za vijijini zikiwa hazina walimu.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze ambae ni mjumbe wa Baraza la madiwani, Mh. Ridhiwani Kikwete alimtaka Mkurugenzi kuacha  kuwapangia walimu kwa upendeleo na badala yake kwa pamoja washirikishane kuona sehemu zenye uhitaji wa walimu.

Kwa  upande wake Diwani wa Kata ya Kimange, Mh. Husein Hading'oka alisema umakini unahitajika katika swala la kuhamisha na kuwapangia walimu vituo vya kazi ili kuepuka kuweka walimu wengi katika shule moja na kuziacha  baadhi ya shule zikiwa hazina walimu wa kutosha.

Aidha, Baraza hilo limejadili swala la msamaha wa ushuru kwa wawekezaji wanaotumia kokoto kwenye machimbo ya Chalinze ambapo wamekataa misamaha hiyo kwakuwa  itavuruga Bajeti  ya Halmashauri.

Wkichangia hoja katika kikao hicho Madiwani hao  walisema swala la msamaha wa ushuru wa kokoto kwa wawekezaji wanaochukua kokoto katika machimbo ya Chalinze linahitaji  kuzingatia Mahitaji ya Bajeti ya Halmashauri ambayo tayari imeshapitishwa.

Walisema, endapo baraza litapitisha msamaha kwa baadhi ya wawekezaji walioomba kusamehewa itavuruga bajeti hiyo na kutaka  baraza hilo lisipitishe msamaha huo kwa mwaka huu na kama ikibidi liangaliwe kwa mwaka wa fedha ujao.

Kufuatia hoja hizo wajumbe wa baraza, Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Saidi Zikataimu aliridhia na kusema kuwa, pamoja na kuheshimu michango ya wawekezaji hao Halmashauri inaweza kutetereka mapato yake ikiwa watapitisha misamaha hiyo na kuwataka wawekezaji hao kuendelea kulipa ushuru kama kawaida kwa kuwa ni utekelezaji wa agizo la Bunge na serikalikwa ujumla katika swala la kukusanya ushuru  ili Halmashauri ziweze  kukusanya mapato ya ndani kwa ufanisi.

 Mwnyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Mh. Saidi Zikatimu wa kwanza kulia, katikati ni Katibu tawala wa wilaya ya Bagamoyo Mh. Erika Liyegela na wa kwanza kushoto ni Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete.
 Diwani wa kata ya Lugoba Mh. Rehema Mwene akitoa hoja katika kikao hicho.
Diwani wa kata ya Miono, Mh. Juma Mpwimbwi akitohoja kwenye kikao cha kufunga Taarifa ya robo ya nne ya mwaka  2015/16. Waliokaa kutoka kushoto ni Diwani wa kata ya Ubena, Mh. Nicholous George Muyuwa, anaefuata ni Diwani wa kata ya Kiwangwa Malota Kwaga.
   Aliyesimama ni Diwani viti maalum Msoga, Mh. Maria Moreto akitoa hoja kwenye  kikao hicho, waliokaa kutoka kulia ni Diwani viti maalum Tarafa ya Msata, Mh. Rehema Mno, anaefuata ni Mh. Cham Semiono, Diwani wa kata ya Msata na watatu kutoka kulia ni  Mh. Rehema Mwene Diwani wa kata ya Lugoba.
Aliyesimama ni Mh. Lekope Laini  Langw'esilo, Diwani kata ya Pera, akichangia hoja katika kikao hicho.
Aliyesimama  ni Diwani viti maalum Tarafa ya kwa Luhumbo, Mh. Tunu Mpwimbwi akichangia hoja katika kikao cha baraza la madiwani Chalinze.
   Mbunge wa jimbo  la Chalinze akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika jana katika ukumbi wamikutano wa Halmashauriya Chalinze.
Kutoka kushoto ni  Katibu Tawala wa wilaya ya Bagamoyo, Mh. Erika Liyegela, wa katikati ni  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Mh. saidi  Zikatimu na wa mwisho kulia ni M kurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze, Edes Lukoa.
Kushoto ni Diwani wa kata ya Bwilingu, Mh. Lukas Lufunga na kulia ni Diwani wa kata ya Msoga, Mh. Hassan Rajabu Mwinyikondo.

Saturday, August 6, 2016

MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA PWANI, SUBIRA MGALU ACHANGIA MADAWATI 20 CHALINZE.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Pwani, Subira  Mgalu, kulia  akimkabidhi  madawati Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Mh. Saidi Zikatimu kushoto

Mbunge  wa viti maalum mkoa wa Pwani Mh. Subira Mgalu  leo amekabidhi madawati  20 kwa Halmashauri ya Chalinze ikiwa ni katika kuunga mkono kampeni ya Mh. Rais wa Jamhuri ya muungano kuhusu utengenezaji wa Madawati ya shule kwa nchi nzima.

Mh. Mgalu alisema ameamua  kutoa madawati hayo ili kuunga mkono juhudi za Rais ambapo kutokana na kuguswa ameamua kutoa msehemu ya Mshahara  wake ili kuchangia Madawati.

Akipokea Madawati hayo, Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze, Saidi Zikatimu, amemshukuru Mbunge huyo kwa mchango huo wa madawati na kumuagiza Afisa elimu msingi kuhakikisha madawati hayo yanafika kwenye shule yenye mahitaji huku akisisitiza kuyatunza.

Mh. Zikatimu alisema kufuatia wito wa Rais Magufuli katika utengenezaji wa  madawai madiwani wa Halmashauri ya Chalinze pamoja wataalamu wao wameweza kuchangia kwa namna moja au nyingine katika upatikanaji wa madawati  katika halmashauri hiyo mpya ya Chalinze iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Mbunge wa  viti maalum  mkoa wa Pwani, Subira Mgalu, kulia akizungumza mara baada  ya kukabidhi madawati katika ofisi za Halmashauri ya Chalinze, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze, Edes Lukoa, na wa pili kushoto niMwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Saidi Zikatimu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya  Chalinze, Mh. Saidi Zikatimu, akizungumza mara baada ya  kukabidhiwa madawati hayo na Mbunge wa viti maalum mkoa wa pwani, Subira Mgalu.
Madiwani wa Halmashauri ya Chalinze wakijaribu  kukalia madawati  hayo.
Waandishi wakifuatilia matukio  Halmashauri ya Chalinze.

Friday, August 5, 2016

RC. MAKONDA ATEMBELEA FFU DAR ES SALAAM



Mkuu wa Mkoa wa Dar Mh. Paul Makonda, amewataka  askari wa kikosi cha kutuliza Ghasia FFU jijini Dar es salaam kudumisha uzalendo  walionao katika kulinda  usalama wa raia.

Mkuu wa mkoa Makonda  ameyasema hayo wakati alipotendelea kikos hicho leo ambapo aliwasifia  kwa kazi nzuri wanayofanya ya  kujituma.

Makonda aliongezea kwakusema uzalendo wao hauko kwenye mshahara bali utaifa kwani hakuna mshahara unaoweza kununua uhai wa mtu.

Rc Makonda amewaahidi kuendelea kuwa pamoja nao na kuwaomba wafanye dar iwe kama dubai ambapo mtu anaweza kuacha mzigo wake na kesho akaukuta. Rc.Makonda anaamini dar inapaswa kuwa salama zaidi ili watu wafanye kazi bila hofu na hata majumba yasiwekewe mageti endapo tu usalama utakuwa mkubwa. 

Mwisho Mh.Makonda amewahakikishia askari hao wa FFU ukonga kuwapatia gari la wagonjwa ili liwasaidie askari katika hospitali yao huku akiahidi kufatilia ombi lake alilolitoa siku ya uzinduzi wa huduma ya polisi kwa wananchi pale viwanja vya Biafra mbele ya Mhe Rais Dkt.John Magufuli, ombi la Makonda lilikua juu ya asilimia 20% ya faini zinazotozwa na trafiki zibaki kwa askari ili kuboresha utendaji ikiwa pamoja na ukarabati wa Magari ya askari sambamba na mafuta ili polisi watakapohitajika wawe wanafika bila kuchelewa.