AJALI YA MOTO YAUA WANNE NGARA.
Alodia Babara Ngara. Watu wanne katika kata ya Rusumo wilaya ya Ngara mkoani Kagera wamepoteza maisha na wengine saba kunusurika kwenye nyumba baada ya chumba walichokuwa wamelala kuwaka moto kutokana na jiko la mkaa ambalo limesababisha madumu ya petroli yaliyokuwa yamehifadhiwa katika chumba hicho kushika moto na kulipuka. Kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Kagera Zabron Muhumha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa, tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Aprili 25, 2024 saa 04:00 alfajiri na kusababisha vifo vya vijana wanne waliokuwa wamelala kwenye chumba kimoja. Amesema jeshi la zimamoto na uokoaji kituo cha Rusumo kilipata taarifa ya tukio la moto wa kuunguza nyumba inayomilikiwa na Didas Dominick Kalido yenye vyumba vinne ambapo watu waliolala katika nyumba hiyo walikuwa 11 na miongoni mwa chumba kimoja cha nyumba hiyo walikuwa wamelala vijana wanne na wote walipoteza maisha na saba walitoka wakiwa na majeraha madogomadog...