TaSUBa KITOVU CHA MAFUNZO TASNIA ZA SANAA NA UTAMADINI NCHINI-DKT. BITEKO
Amefunga tamasha la 42 la Kimataifa la Utamaduni Bagamoyo. Aipongeza Wizara kwa kutangaza utamaduni wa nchi. Sanaa iwe nyenzo kuunganisha wananchi Imeelezwa kuwa, Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ni kitovu cha mafunzo katika tasnia za Sanaa na Utamaduni nchini na Serikali imeendelea kuiboresha taasisi hiyo kwa kutoa fedha za kuboresha miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko alipomwakilisha Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kilele cha Tamasha la 42 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lililoandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na TaSUBa mkoani Pwani Oktoba 28, 2023. "Niwapongeze Wizara kwa kuitangaza nchi yetu kwa kupitia kazi mbalimbali za utamaduni, sanaa na michezo. Aidha nakupongeza Waziri na wafanyakazi wa Wizara yako kwa kazi kubwa mnayoifanya kila mwaka katika kuliandaa na kuliendesha Tamasha hili kwa kipindi cha miaka 42 ...