RC MAKALLA: MRADI WA MWENDOKASI KILWA ROAD MBAGALA KUKAMILIKA MARCH 2023*.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* amewapongeza *TANROAD* kwa hatua walizochukuwa kumsimamia Mkandarasi kutoka kampuni ya *SINOHYDRO* anaetekeleza Awamu ya pili ya mradi wa *Ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya mwendokasi Kilwa road.* Akizungumza wakati wa *ziara* ya kukagua Miradi ya maendeleo Wilaya ya Temeke, *RC Makalla* amefurahi kuona Ujenzi huo umefikia *Asilimia 52* ambapo amemtaka *Mkandarasi kuongeza bidii* ili kazi ikamilike kabla ya *mwezi March mwakani* ili lengo la *Rais Samia Suluhu Hassan* kutoa huduma bora ya usafiri iweze kutimia. Kutokana na *mwenendo Mzuri* wa Mkandarasi, *RC Makalla* ameelekeza kuwepo kwa utaratibu rafiki utakaofanya Shughuli za Ujenzi zinazoendelea *zisiathiri Shughuli za Wananchi* ikiwemo kusababisha *foleni, vumbi na hata kuzuia uzalishaji viwandani.* Hata hivyo *RC Makalla* amewaelekeza *TANROAD na TARURA* kumpatia *taarifa ya mgawanyo wa Majukumu* yao hususani kuweka makubaliano ya nani anapaswa kusimamia *Mifereji na Mitaro.* K...