Msemaji wa Mufti wa Tanzania,Katibu wa Baraza la Ulamaa Sheikh Hassan Chizenga alipozungumza na wanahabari jijini Dar es salaam.
........................................
NA MUSSA KHALID
Mfalme wa Morocco Mtukufu Muhammed wa sita ameruhusu kufanyika ufunguzi mdogo wa msikiti wa Mohamed wa sita na Mpya wa Makao Makuu unaotarajiwa kuchukua waumini zaidi ya 6000 uliojengwa Kinondoni road jijini Dar es salaam.
Akizungumza Leo jijini Dar es salaam Msemaji wa Mufti wa Tanzania,Katibu wa Baraza la Ulamaa Sheikh Hassan Chizenga amesema msikiti huo ulijengwa na Mfalme wa Morocco ikiwa ni zawadi iliyotolewa kwa waislamu wa Tanzania utafunguliwa kesho April,15 Mwaka huu.
Shekh Chizenga amesema kuwa hatua hiyo ilifikiwa baada ya Juhudi za viongozi wakuu wa nchi Katika awamu Mbili zilizopita Dkt Jakaya Kikwete na Hayati Dakt John Magifuli kujenga Mahusiano mazuri na Morocco jambo lililopelekea Mfalme Huyo kutembelea Tanzania na kufikishiwa ombi Hilo la ujenzi wa msikiti.
Aidha Shekh Chizenga amesema kuwa msikiti huo ulikuwa ufunguliwe miaka miwili iliyopita hivyo kutokana na janga la Corona lilisababisha Mfalme wa Morocco kushindwa kufika nchini Kwa lengo la kufungua msikiti huo.
“Ufunguzi kamili wa msikiti huu utafanyika baadae kea kufunguliwa rasmi na Mfalme Mwenyewe Mtukufu wa sita siku za usoni pale mazingira na mipango ya tukio Hilo litakapo kamilika”amesema Shekh Chizenga.
Imeelezwa kuwa msikiti huo utakuwa ni miongoni mwa misikiti mikubwa Afrika Mashariki huku kwa nchi Tanzania ukiongoza kuingiza waumuni wengi zaidi ya 6000 hivyo waumini wa Dini ya Kiislamu wametakiwa kuonyesha ushirikianao kwa kujitokeza kwenye ufunguzi Pamoja kuswali ibada za jamaa Kwenye msikiti huo.
No comments:
Post a Comment