Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* amewapongeza *TANROAD* kwa hatua walizochukuwa kumsimamia Mkandarasi kutoka kampuni ya *SINOHYDRO* anaetekeleza Awamu ya pili ya mradi wa *Ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya mwendokasi Kilwa road.*
Akizungumza wakati wa *ziara* ya kukagua Miradi ya maendeleo Wilaya ya Temeke, *RC Makalla* amefurahi kuona Ujenzi huo umefikia *Asilimia 52* ambapo amemtaka *Mkandarasi kuongeza bidii* ili kazi ikamilike kabla ya *mwezi March mwakani* ili lengo la *Rais Samia Suluhu Hassan* kutoa huduma bora ya usafiri iweze kutimia.
Kutokana na *mwenendo Mzuri* wa Mkandarasi, *RC Makalla* ameelekeza kuwepo kwa utaratibu rafiki utakaofanya Shughuli za Ujenzi zinazoendelea *zisiathiri Shughuli za Wananchi* ikiwemo kusababisha *foleni, vumbi na hata kuzuia uzalishaji viwandani.*
Hata hivyo *RC Makalla* amewaelekeza *TANROAD na TARURA* kumpatia *taarifa ya mgawanyo wa Majukumu* yao hususani kuweka makubaliano ya nani anapaswa kusimamia *Mifereji na Mitaro.*
Katika ziara hiyo *RC Makalla* pia ametembelea *Ujenzi wa Zahanati ya Toangoma* inayogharimu Shilingi *Milioni 250* na Zahanati ya *Kilakala* inayogharimu Shilingi *Milioni 250* ikiwa ni fedha zitokanazo na *Tozo za Simu* ambapo *amepongeza Halmashauri ya Manispaa ya Temeke* kwa kusimamia kikamilifu Miradi ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment