Posts

RC MAKALLA: MRADI WA MWENDOKASI KILWA ROAD MBAGALA KUKAMILIKA MARCH 2023*.

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* amewapongeza *TANROAD* kwa hatua walizochukuwa kumsimamia Mkandarasi kutoka kampuni ya *SINOHYDRO* anaetekeleza Awamu ya pili ya mradi wa *Ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya mwendokasi Kilwa road.* Akizungumza wakati wa *ziara* ya kukagua Miradi ya maendeleo Wilaya ya Temeke, *RC Makalla* amefurahi kuona Ujenzi huo umefikia *Asilimia 52* ambapo amemtaka *Mkandarasi kuongeza bidii* ili kazi ikamilike kabla ya *mwezi March mwakani*  ili lengo la *Rais Samia Suluhu Hassan* kutoa huduma bora ya usafiri iweze kutimia. Kutokana na *mwenendo Mzuri* wa Mkandarasi, *RC Makalla* ameelekeza kuwepo kwa utaratibu rafiki utakaofanya Shughuli za Ujenzi zinazoendelea *zisiathiri Shughuli za Wananchi* ikiwemo kusababisha *foleni, vumbi na hata kuzuia uzalishaji viwandani.* Hata hivyo *RC Makalla* amewaelekeza *TANROAD na TARURA* kumpatia *taarifa ya mgawanyo wa Majukumu* yao hususani kuweka makubaliano ya nani anapaswa kusimamia *Mifereji na Mitaro.* K...

MFALME WA MOROCCO ARIDHIA KUFUNGULIWA KWA MSIKITI WA MOHAMED WA SITA ULIOJENGWA TANZANIA.

Image
  Msemaji wa Mufti wa Tanzania,Katibu wa Baraza la Ulamaa Sheikh Hassan Chizenga alipozungumza na wanahabari jijini Dar es salaam. ........................................ NA MUSSA KHALID Mfalme wa Morocco Mtukufu Muhammed wa sita ameruhusu kufanyika ufunguzi mdogo wa msikiti wa Mohamed wa sita na Mpya wa Makao Makuu unaotarajiwa kuchukua waumini zaidi ya 6000 uliojengwa Kinondoni road jijini Dar es salaam.   Akizungumza Leo jijini Dar es salaam Msemaji wa Mufti wa Tanzania,Katibu wa Baraza la Ulamaa Sheikh Hassan Chizenga amesema msikiti huo ulijengwa na Mfalme wa Morocco ikiwa ni zawadi iliyotolewa kwa waislamu wa Tanzania utafunguliwa kesho April,15 Mwaka huu.   Shekh Chizenga amesema kuwa hatua hiyo ilifikiwa baada ya Juhudi za viongozi wakuu wa nchi Katika awamu Mbili zilizopita Dkt Jakaya Kikwete na Hayati Dakt John Magifuli kujenga Mahusiano mazuri na Morocco jambo lililopelekea Mfalme Huyo kutembelea Tanzania na kufikishiwa ombi Hilo la ujenzi wa msikiti...

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI 14 APRIL 2022.

Image
 

ASILIMIA 26 YA WATU WAZIMA WANASHINIKIZO LA JUU LA DAMU.

Image
  Na WAF- DOM  MGANGA Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe amebainisha kuwa asilimia 26 ya watu wazima wenye umri wa miaka kati ya 25 hadi 64   wana shinikizo la juu la damu, hali inayosababishwa na mtindo wa maisha ikiwemo ulaji wa vyakula vya mafuta mengi, matumizi ya pombe kupita kiasi na kutofanya mazoezi.   Dkt. Sichalwe amebainisha hayo leo Aprili 13, 2022 wakati akifungua Mradi wa Healthy Heart Africa tukio lililofanyika katika zahanati ya Makole Jijini Dodoma.   “Tumefanya utafiti mwaka 2012 na kukagundua kwamba asilimia 26 ya watu wazima kati ya miaka 25 na 64 wana shinikizo la juu la damu na tatizo hili linatarajia kuongezeka kwa kiasi kikubwa endapo hatutachukua hatua.” Amesema Dkt. Sichalwe.   Aliendelea kusema kuwa, tafiti zinaonesha kuwa, zaidi ya asilimia 75% ya Wagonjwa hao wenye shinikizo la juu la damu hawatumii tiba yoyote, huku akiweka wazi kuwa zaidi ya robo tatu kati yao hawajui kama wana shinikizo la juu la damu.  ...

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI

Image
 

MAGAZETI YA LEO JUMATANO 13 APRIL 2022.

Image
 

SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA CDC KUDHIBITI MAGONJWA

Image
  Na WAF- DOM Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa nchini Tanzania (Centre of Diseases Control – CDC) Dkt. Mahesh Swaminathan katika Ofisi za Wizara Jijini Dodoma. Waziri Ummy Mwalimu ameishukuru CDC kwa kuendelea kuwa mshirika wa Karibu wa Serikali na Wizara ya Afya kwa kutoa ushirikiano na msaada katika mapambano dhidi ya Magonjwa mbalimbali ikiwemo Ugonjwa wa Virusi Vya Ukimwi, Kifua Kikuu, Malaria pamoja na UVIKO-19. “CDC amekuwa mshirika wetu wa karibu katika mapambano dhidi ya magonjwa mbalimbali na katika kutekeleza afua za kuboresha ubora wa huduma za afya nchini Tanzania.” Amesema Mhe. Ummy Mwalimu. Waziri Ummy Mwalimu ametaka ushirikiano zaidi katika kuboresha na kuongeza huduma za maabara za afya ya jamii pamoja na kuboresha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa ili kuwezesha Serikali kuchukua hatua stahiki mapema zaidi na kuokoa maisha ya wananchi. Waziri Ummy Mwalimu ameishuku...